Nini hatima ya Zanzibar CHADEMA wakichukua nchi?

sajosojo

JF-Expert Member
Apr 14, 2010
1,017
619
Katika maswali ninayojiuliza sana ni kuhusu hatma ya Zanzibar hapo 2015 endapo CHADEMA waingia madarakani, maana CHADEMA haina sapoti ya kutosha ZANZIBAR.

Na kulingana na hizi vurugu za wazanzibar kutaka kujiondoa katika muungano, je watawaacha waende?
 
argument ambayo ni sahihi zaidi ni uwezekano mkubwa wa CUF kushinda uchaguzi Z;BAR 2015....hapo sasa unaweza kuuliza hatma ya muungano itakuwa vipi.lakini kwa CHADEMA kushinda uchaguzi without zanzibar ni wish fool think ,ni ile tamaa ya fisi yakufikiri eti siku moja mkono utadondoka atafune.......ni vizuri zaidi chadema wakubali kuwa wanaudhaifu mkubwa huko zanzibar na waanze mkakati wa kuingia huko kama ambavyo wamefanya kwa mikoa ya kusini at the same time washirikiane zaidi na CUF kuliko kuwatenga na kuwadharau......CCM wamegundua hilo mapema.
 
What for?????????????Hivi ZANZIBAR kama hawataki muungano tunalazimisha wa nini?LET THEM GO!!!!!! CDM tunataka maendeleo ya wananchi wetu sidhani kama muungano ni Kipaumbele kwetu kisaaaaaana mpaka tutumie nguvu kama iliyotumiwa na CCM tukazalisha wakimbizi.
 
Zanzibar inawakazi wangapi?hivi zanzibar wanapigaga kura za kumchagua rais za jamhuri ya muungano au?okey mbaya na hiyo maadam wao watachagua cuf/ ccm tunapiga mseto
 
Katika maswali ninayojiuliza sana ni kuhusu hatma ya Zanzibar hapo 2015 endapo CHADEMA waingia madarakani, maana CHADEMA haina sapoti ya kutosha ZANZIBAR.

Na kulingana na hizi vurugu za wazanzibar kutaka kujiondoa katika muungano, je watawaacha waende?

Pitia Hansard za Bunge uone Tundu Lissu alisema nini kuhusu Muungano feki
 
CHADEMA wanatakiwa wajipange upya kuhusu hili. Muugano wetu hauwezi kuvunjika eti tu chama fulani kimeshika madaraka. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa muhimu sana hususani katika suala la ulizi (kijeshi).
Kwahiyo tunatakiwa kuwa na mpango mkakati katika katiba kuwa: ili raisi achaguliwe:-
1. Awe amepata si chini ya kura asilimia 30% zanzibar na 30% bara katiak kura zote zilizopingwa.
Kuwe na awamu 3 za uchaguzi wa raisi nikimanisha kwamba:
1. Katika mabaraza ya wasomi.
2. Kura za majimbo.
3. Kura za watu magerezani, nje ya nchi.

Na kura zote zijumlishwe kwa asilimia sio kwa idadi
 
Katika maswali ninayojiuliza sana ni kuhusu hatma ya Zanzibar hapo 2015 endapo CHADEMA waingia madarakani, maana CHADEMA haina sapoti ya kutosha ZANZIBAR.

Na kulingana na hizi vurugu za wazanzibar kutaka kujiondoa katika muungano, je watawaacha waende?

Sijui ni mawazo finyu au mawazo makubwa hadi watu hawaoni point ipo wapi! :lock1:
So rahisisha mawazo uliyotoa au yawekee nguvu ya hoja ili tuelewe. Katika ishu ya Muungano ni wizi mtupu. Tunajua kwanini wanaubembeleza na kkwanini hawataki kuulipuua na ZnZ wanataka nini/... So CDM wakiingiia kitajulikana cha kufanya. Unajua CDM Huwa hawakurupuki.:lock1:
 
Back
Top Bottom