Nini hatima ya Halima Mdee na wenzake baada ya bunge kuvunjwa?

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,457
2,281
Wadau nawasabahi.

Uchaguzi ndio huo unakaribia. CHADEMA wameshinda pambano lao dhidi ya Halima Mdee na kundi lake kwa kuishawishi Mahakama Kuu kuthibitisha uhalali wao wa kuwafukuza Halima Mdee na kundi lake uanachama.

Pia, CHADEMA wametekeleza wajibu wa kikatiba kulijulisha Bunge na Tume ya Uchaguzi kuwa Halima Mdee na kundi lake sio wanachama wao kikatiba, hivyo hawastahili kuwa bungeni. Lakini bunge, serikali, na tume ya uchaguzi kwa pamoja wameamua kuvunja katiba kwa makusudi kwa kuendelea kuwalipa mishahara na posho kinyume na sheria kwa mujibu wa katiba. Kwani katiba inasema moja ya sababu za mbunge kupoteza ubunge wake ni "kufukuzwa uanachama na chama chake".

Hakika, bunge letu limeweka historia ya kuwa "Bunge lenye wabunge wasio na chama".
Najiuliza, nini hatima ya Halima Mdee na kundi lake baada ya bunge kuvunjwa?
Je, watajiunga na CCM?
Je, watajiunga na vyama vingine ila sio CHADEMA?
Je, CCM itawateua kama wabunge wa viti maalum?
Au watastaafu siasa?

Ngoja tusubiri 2025.
 
Kati yao kuna wengine walikuwa majembe ambayo yalikuwa ya kutegemewa lakini tamaa hizi zimewafanya wauze utu wao ili tu wawe wabunge huko Dodoma.Lakini wengine wamekuwa wabunge kwa miaka mitano au kumi bado walikuwa hawajapata hela za kutosha za kuwawezesha kufanya shughuli zingine za kujiingizia kipato mpaka walazimishe kuwa wabunge! Nonsense
 
Ndio maana Kuna watu we will never take seriously kitu tunachoambiwa na serekali. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeona haya yanayofanywa na bunge kwa kushirikiana na serekali akaona ni Sawa. Alafu kesho bunge au serekali ijitokeze iseme jambo fulani na kuwataka raia wafanye unahisi watachukulia serious?
 
Kati yao kuna wengine walikuwa majembe ambayo yalikuwa ya kutegemewa lakini tamaa hizi zimewafanya wauze utu wao ili tu wawe wabunge huko Dodoma.Lakini wengine wamekuwa wabunge kwa miaka mitano au kumi bado walikuwa hawajapata hela za kutosha za kuwawezesha kufanya shughuli zingine za kujiingizia kipato mpaka walazimishe kuwa wabunge! Nonsense
Mtaani pagumu
 
Najiuliza, nini hatima ya Halima Mdee na kundi lake baada ya bunge kuvunjwa?
Je, watajiunga na CCM?
Jibu hapa ni rahisi sana.
Ukijibu nani ndani ya CHADEMA alikuwa nyuma yao walipoingia Bungeni, utapata jibu la swali lako kama ifuatavyo:

Huyo aliyewawezesha kuingia Bungeni; na hajawahi kulisemea kwa uwazi jambo hili mbele za watu wakamsikia bayana, ndio msingi wa wao kuendelea kuwa Bungeni, pamoja na sarakasi zilizofanyika ndani ya CHADEMA kama ulivyo eleza hapo juu..
Hawa wabunge wataungana na 'sponsor' wao huyo, ambaye sasa anaonyesha wazi kuwa yeye na Samia wanaweza kufanya kazi pamoja. CHADEMA unayoisema ikileta ugumu kwenye mpango wa kufanya kazi na Samia, ataifutilia mbali kwa kuifukuza, au kutengana nayo.
Kwa hiyo usalama wa hawa wabunge upo vizuri tu, usifikiri hizo mbinu za mahakama zinazuia chochote.
 
Wadau nawasabahi.

Uchaguzi ndio huo unakaribia. CHADEMA wameshinda pambano lao dhidi ya Halima Mdee na kundi lake kwa kuishawishi Mahakama Kuu kuthibitisha uhalali wao wa kuwafukuza Halima Mdee na kundi lake uanachama.

Pia, CHADEMA wametekeleza wajibu wa kikatiba kulijulisha Bunge na Tume ya Uchaguzi kuwa Halima Mdee na kundi lake sio wanachama wao kikatiba, hivyo hawastahili kuwa bungeni. Lakini bunge, serikali, na tume ya uchaguzi kwa pamoja wameamua kuvunja katiba kwa makusudi kwa kuendelea kuwalipa mishahara na posho kinyume na sheria kwa mujibu wa katiba. Kwani katiba inasema moja ya sababu za mbunge kupoteza ubunge wake ni "kufukuzwa uanachama na chama chake".

Hakika, bunge letu limeweka historia ya kuwa "Bunge lenye wabunge wasio na chama".
Najiuliza, nini hatima ya Halima Mdee na kundi lake baada ya bunge kuvunjwa?
Je, watajiunga na CCM?
Je, watajiunga na vyama vingine ila sio CHADEMA?
Je, CCM itawateua kama wabunge wa viti maalum?
Au watastaafu siasa?

Ngoja tusubiri 2025.
Wanasubiri Mbowe awe mwenyekiti awaombee msamaha wagombee ubunge kupitia cdm, maana Mbowe anajua Siri ya wao kuwa bungeni.

Ama ikishindikana wale wanaofahamika watapewa vyeo huko serekalini, wengine watakimbilia kujaribu bahati zao vyama vingine.
 
Jibu hapa ni rahisi sana.
Ukijibu nani ndani ya CHADEMA alikuwa nyuma yao walipoingia Bungeni, utapata jibu la swali lako kama ifuatavyo:

Huyo aliyewawezesha kuingia Bungeni; na hajawahi kulisemea kwa uwazi jambo hili mbele za watu wakamsikia bayana, ndio msingi wa wao kuendelea kuwa Bungeni, pamoja na sarakasi zilizofanyika ndani ya CHADEMA kama ulivyo eleza hapo juu..
Hawa wabunge wataungana na 'sponsor' wao huyo, ambaye sasa anaonyesha wazi kuwa yeye na Samia wanaweza kufanya kazi pamoja. CHADEMA unayoisema ikileta ugumu kwenye mpango wa kufanya kazi na Samia, ataifutilia mbali kwa kuifukuza, au kutengana nayo.
Kwa hiyo usalama wa hawa wabunge upo vizuri tu, usifikiri hizo mbinu za mahakama zinazuia chochote.
Wewe kweli una akili sawa sawa?
Kwa hiyo kama kuna mtu mkubwa ndani ya Chadema (labda tuseme mwenyekiti) yupo nyuma yao, hiyo inatosha wao kuwepo bungeni kihuni kihuni vile?

Yaani huyo mtu ana nguvu, mamlaka na uwezo wa juu wa kuirubuni serikali ya CCM na bunge lake ili hao malaya wa Covid 19 waendelee kuwepo bungeni?

Huyo mkubwa wa Chadema unayedai yuko nyuma yao ndio aliwezesha yule mwanamke aliyekuwa gerezani kutolewa usiku usiku ili akaapishwe?

Huyo mkubwa wa Chadema unayemsema ndio akamuamrisha mpaka spika Ndugai kwenda kule garage ya ukumbi wa bunge kuwaapisha wale malaya wa covid 19?

Anza sasa kufikiri kwa akili yako, acha kukaririshwa vitu vya kijinga, kipuuzi na kipumbavu. Kwa akili hizo ulizonazo sasa JF hapakufai kabisa.
 
Wewe kweli una akili sawa sawa?
Kwa hiyo kama kuna mtu mkubwa ndani ya Chadema (labda tuseme mwenyekiti) yupo nyuma yao, hiyo inatosha wao kuwepo bungeni kihuni kihuni vile?
Hapana.
Mimi sijasema kuwa hao wabunge wapo bungeni kihalali. Hili unanitwisha lawama nisiyoikubali. Nisome tena vizuri utanielewa tu.
Mimi na wewe tupo upande huo huo mmoja kuhusu uhalali wao wa kuwa bungeni.
 
Kati yao kuna wengine walikuwa majembe ambayo yalikuwa ya kutegemewa lakini tamaa hizi zimewafanya wauze utu wao ili tu wawe wabunge huko Dodoma.Lakini wengine wamekuwa wabunge kwa miaka mitano au kumi bado walikuwa hawajapata hela za kutosha za kuwawezesha kufanya shughuli zingine za kujiingizia kipato mpaka walazimishe kuwa wabunge! Nonsense
Upo sahihi wamethibitisha Usaliti wa kiwango cha juu hata ukiwaoa watakusaliti kuna mmoja wao mume kamwacha
 
Anza sasa kufikiri kwa akili yako, acha kukaririshwa vitu vya kijinga, kipuuzi na kipumbavu. Kwa akili hizo ulizonazo sasa JF hapakufai kabisa.
LOooh!
Mkuu 'Zanzibar-ASP', leo naona unatafuta ugomvi tu na mimi bila ya sababu zozote. Jibu langu hapo linabaki lilivyo, bila kujali haya uliyo andika hapa.

Kundi la wale wanawake walioko Bungeni kinyemela, siyo kundi la watu wasiokuwa na akili kichwani, kama unavyodai akili zangu zilivyo. Wale wanawake, kama akina Mdee, yule wa Mara, n.k., siyo watu wa kutishwa tu na Magufuli na kuamua kufanya kama walivyo amua kufanya bila ya ushirikiano wa aina fulani toka ndani ya chama chao.
Sasa hapa pia usinilaumu kudhani kwamba huyo aliye nyuma yao alikubali kufanya kazi na mtesi wao mkubwa, Magufuli. Sababu zinaweza kuwa ni tofauti na hivyo.
 
Wanasubiri Mbowe awe mwenyekiti awaombee msamaha wagombee ubunge kupitia cdm, maana Mbowe anajua Siri ya wao kuwa bungeni.

Ama ikishindikana wale wanaofahamika watapewa vyeo huko serekalini, wengine watakimbilia kujaribu bahati zao vyama vingine.
Hao wamepewa ubunge na Magufuli Mbowe na Magufuli walikuwa paka na Panya mbowe hausiki na Usaliti wao
 
LOooh!
Mkuu 'Zanzibar-ASP', leo naona unatafuta ugomvi tu na mimi bila ya sababu zozote. Jibu langu hapo linabaki lilivyo, bila kujali haya uliyo andika hapa.
Kundi la wale wanawake walioko Bungeni kinyemela, siyo kundi la watu wasiokuwa na akili kichwani, kama unavyodai akili zangu zilivyo. Wale wanawake, kama akina Mdee, yule wa Mara, n.k., siyo watu wa kutishwa tu na Magufuli na kuamua kufanya kama walivyo amua kufanya bila ya ushirikiano wa aina fulani toka ndani ya chama chao.
Sasa hapa pia usinilaumu kudhani kwamba huyo aliye nyuma yao alikubali kufanya kazi na mtesi wao mkubwa, Magufuli. Sababu zinaweza kuwa ni tofauti na hivyo.
Ndio maana nimekujibu wazi kuwa anza kufikiri kwa akili yako na sio kwa akili ya kushikishwa. Ngoja nichambue.

1. Hakuna taratibu yoyote halali ndani au nje ya Chadema iliyowahi kukaa na kupitisha mchakato wa ubunge wa Covid 19, ukiondoa nguvu ya kipuuzi ya dola.

2. Vikao vyote halali ndani ya Chadema viliwakana na mwisho vikaitimisha kuwavua uanachama kwa kauli moja wabunge wote wa Covid 19.

3. Viongozi wote wa juu wa Chadema, ndani ya vikao na nje ya vikao walitoa kauli moja ya kuwakana na kuwakataa wabunge wote wa Covid 19.

4. Mchakato mzima wa kuwapa ubunge wa kihuni ulifanywa na utawala wa Magufuli kwa nguvu zote.

5. Kunde lote liwe la Covid 19 tangu waingie bungeni wamekuwa against Chadema na hapo hapo wamekuwa chawa wazuri wa CCM.

Sasa, katika hali hiyo, unapokuja na kutengeneza conspiracy theory ya kihuni kihuni hapa JF kuwa, wale wabunge wa Covid 19 wako pale bungeni kwa nguvu ya kigogo mmoja wa CHADEMA. How?
 
Back
Top Bottom