Nini cha kufanya ukimfumania mkeo redhanded huku bado unampenda!!!!!

lol pole lara 1 kwa yaliyokusibu, sasa mbona hutupi feedback bado maza yuko na simu yako? na ishu imeishaje? makubwa haya. Pole kwa bro na wifi yako pia ila kwanini bro wako hamuambii matatizo yake bi mkubwa? na anakuamini sana wewe ilhali hauko kwenye ndoa?

Maza yupo tu! Katoka kuchoma insulin kutuliza shuga, maana ilishuka ! We acha saivi ametulia ndo anaona uzito wa tatizo ulivomkubwa! Ukizingatia Maza anachowaza yeye ni mzee wa kanisa, sasa sura yake ataiweka wapi! N a inamuuma sana kuwa mwanae ni mume mwema kwanini yamkute haya mabalaaa! Ndoa ina 1 yr watu hata michango yao hawajaisahau! Na vyovyote itakavoisha lazima idhalilishe familia sana. Kuhusu kushauri kule kanishukuru manake angeenda mwenyewe kupata taarifa angeweza either afe kwa presha au angekuwa lupango kwa mudder case. Hapo ameshatoa angalizo hataki kusikia mtu akitaja jina la wifi!
 
a walk of shame!!jf balaa tupu

Walk of shame ni kwa mamaster wale wasioshikwa, na wanaopoteza ushahidi wote! Dhamira tu ndo inawasuta. Ila ukishikwa inakuwa WALK OF DEATH!!! LMAO! Unaweza kujikuta unauawa eti! Na ukinusurika kifo inabidi uchinje mbuzi na kuatambika haswaaa!
 
M2 unaeza ufe ukijtazama, me kwakwel ngja kwnz nifumanie thn hapo hapo ntajua cha kufanya
 
Ingawa roho itauma but dawa ni kupiga chini, once a thief always a thief, halafu anajionyesha kakubuhu siku 4 nje!!!!!!!!! hii haikubaliki
 
Refer to the heading.
Binafsi nikimfunania wife wangu redhanded kwa kuwa nampenda sana, sitomuua nitamtaliki bila kutoa uahai wake.
Kumwachia uhai wake ndiyo feva ambayo nitampa kwakuwa nampenda sana.

Kumuachia uhai ni jambo jema kwa sbb unampa nafasi ya kumlea mtoto(shez got a 2-years-baby).
 
Yaani sitaki hata itokee nadhani sitakuwa na hamu nae teeeeeeeena, sababu mie sijawahi toka nje ya ndoa yangu seven yrs now!! Aisee mungu ataniusamehe tu hata km ni ndoa ya kanisani sitaweza kula tena ile kitu nikijua kuna mtu alitema cheche zake pale khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Sio kutema cheche tu, hata kuivuruga kwa fujo maana anajua sio mali yake anafanya lolote awezalo.Duh!
 
Leo sina jibu, ila nikimfumania, basi LIWALO na LIWE! sitasubiri UPEPO upite!!
 
Huyo mke si mwaminifu na kwangu binafsi nitamtaliki tu yaishe hata Yesu alisema talaka ni kama umemkita mwenzako akizini
 
Sijui maana Bado kumfumania, kaka ako Naye *****, maanake inakuwaje Mlinzi na dada wajue halafu yeye asijue? Nyumba ilishamshinda mda mrefu sana.

QUOTE=lara 1;4642264]Nawasalimu wadau wa JF!

Mimi ni mzima na wikiend nilikua gonjwagonjwa imelala kitandani, si mwajua dozi na maji ya dhahabu haviendani.

Back to the main topic, waungwana mliioa na kuolewa nawapa BIG UP kubwa sana kwa kuachana na uzinzi usio wa lazima (watu mnapendana alafu hamuoani kazi kuzini tu! na kuongeza msururu wa dhambi wakati wa kitubio), na nyie mabachelor kama mimi, kama mna wapenzi oaneni, uzee waja, na ambao hamjabahatika nawaombea kwa mola muwapate wenzenu.


Mimi sijaolewa, wala mtoto hata wa kusingiziwa sina, ila born town kitambo, na cha kushangaza ndugu zangu na marafiki zangu wengi sana walioolewa/kuoa na waliojipasishia watoto wa watu/waliojipeleka kwa waume zao, wanaifanya mimi comfidant wao sana kwa kunieleza mambo mazito ya ndoa zao, na mimi ni mshauri mkubwa sana kwao. Hii hali maza wangu haipendi kinoma, anadai itanifanya niogope ndoa, hivo akijua mtu ananiomba ushauri anaenda kumpashua, atafute mwanandoa mwenzie amshauri. utasikia "Kama huipendi ndoa yako we sikiliza ushauri wa huyu mtoto, yeye hata kumpata mtu amuweke ndani bado atakushauri nini?" Hajaishia hapo kapiga biti ukoo mzima no mtu kuniomba ushari. Na mimi tumekubaliana nikimshauri mtu tena tunakosana jumlajumla, nikamuahidi kazi ya mama ushauri mimi basi!

Kweli mimi nina moyo wa kuacha hii kazi! ila naipenda sana haswaa part ya kupata maumbea ya ndani kwa watu, si mnajua tena watu unaweza kuwaona wako perfect kinoma, wanakurusha rohooo, ila wakija kukuconsult mazito ya ndani mwao unabaki unaguna tu! Nikiacha hii kazi nitakosa uhondo!( sitangazi kwa mtu ila nafaidi mwenyewe tu umbea)

Baada ya kutoa ahadi ya kutokushauri mtu tena, jana usiku mida ya saa 4, Kaka yangu kabisa kabisa kanipigia simu kuwa kamfumania mkewe wa ndoa ya mwaka! Ishu yenyewe ilikuwa hivi, Bro kasafiri kikazi, sasa akamwambia mkewe anarudi leo jpili, afu wanaaminiana kinoma, sasa kazi zikawahi kuisha, hivo akaona arudi jmosi amuwahi mamsap na baby girl (2yrs) ila hakumwambia mkewe wala nini.

Kufika getini mlinzi kamtolea mijicho kama kabanwa na mlango, kumfokea ndo kafungua geti, akahisi kuna ishu lazima! Hausgeli nae hamwangalii machoni, mke hayupo, kumuulizia beki tatu anababaika mara kaenda dukani, mara kamsindikiza mgeni, ming u saa 7 hiyo. Akwaita beki tatu na mlinzi akawaambia waseme ukweli lasivo asubuhi kazi basi! Mlinzi akaanza kutiririka bwana mkeo kaondoka hii siku ya 4 hajalala hapa! Beki tatu anaulizwa kweli? Kimyaaa! Akachukua simu zao, akawaambia wakalale.

Saa tano leo jpili Wife karudi kwa mbwebwe, hapo kashatuma sms kwa beki tatu apike pilau Mr. anarudi. Ile kufika namkuta Mr. kwenye kochi, si ndo presha kupanda na kushuka! Mume kamtega niambie ukweli wote bila kuficha nitakusamehe manake najua hujalala siku 4! Wifi nae sijui uoga, sijui ubwege, sijui ushamba hata sielewi, si KAFUNGUKA A to z. Bila kupindisha ukweli wowote na kuomba msamaha dobledoble! Kamtaja hadi bwana wake, wana uhusiano toka lini, na mengine kibao yenye kumteketeza zaidi.! Bro kuzama kwenye pochi si ndo kakuta THE PILLS AFTER hizi ndo zile dawa kama umecheza kavukavu ndo unameza kabla ya 72 hrs hupati mimba. Hivo inaelekea wifi hakutumia kinga huko kwenye uasherati wake.( Can u imagine na ukimwi wote huu!)

Basi bro akamwambia we ondoka, nisije kukua bure! Akanipigia njoo haraka, nikamwambia mie naumwa mwenzio kwani vipi!? Kama huji utakuta kaka yako nimejinyonga na usije kwenye mazishi yangu! Mtumeeee! Nikakurupuka kwenda kwake ndo kunielezea A to Z na kutaka ushauri. Nikakumbuka moyoni nishamwambia Maza mi sishauri tena, ila nikabullshit nikasema huyu kaka yangu wacha nimshauri.

Nikamwambia kweli hayo mambo ya aibu bro, tena yataudhalilisha uume wako haswaa, ila nyie mna ndoa ya kanisani, na najua unampenda mkeo, pamoja na yote hasira tu ndo zimekubana, HUU NDO WAKATI WA KUWA MWANAUME HASWAA! Mtizame mwanao 2yrs only, sote binadamu, yeye kateleza ila kuvunja ndoa si sahihi, istoshe wanawake wote wanaksoro. Na kwanza hukumkuta bikra, so we kaza roho. We mtext arudi, usimuulize chochote, endelea kuishi nae kama zamani dhamira yake itamla itammaliza.
Nikamsisitiza hili jambo asimwambie yeyote, tuwe tunalijua watatu tu mimi, yeye na wifi. Sababu wakijua watu wengine alafu asipomuacha atajiaibisha zaidi tu. Akanielewa akamtext nikamuacha wifi karudi yamepo.

Jioni Maza kaanza kunipeleleza kuwa mbona kaenda kwa Bro hakueleweki, Kama kuna jambo na haambiwi! niknyuti mi sijui lolote! Akaninganganiza wewe watakuwa wamekuomba ushauri!, niambie mimi mzazi wenu ujue, sio vizuri, hata kama umeshauri pamoja na kukutaza sitokasirika niambie! Si ndo nikafunguka!

Weeeee! Najuuuta! Maza akapaniki, yaani unamshauri mwenzio alee uzinzi aje kufa na ngoma? Utanizalia mtoto mkubwa kama yule wewe? Hivi unaona aliyofanya wifi yako mazuri? Msinichezeee! Haiwezekani, huyo muasherati aondoke na mengine mengi!

Na wewe (mimi) nilikwambiaje kushauri watu? Kwanini hukumshauri aniambie mimi mzazi wake? Sasa kukukomoa nyie si mmefanya siri ya watu 3 nawaambia ndugu na marafiki woteee, afu nasema ni wewe ndo umeuza mkanda! Tena natahadharisha wewe ni mmbea mkubwa watu waskwambie tena mambo yao! Ndo dawa yako hii! Hapo kanipora simu yangu na kujifungia chumbani! Sijui atawatext au atapiga.

Kichwa kinaniuma! Natamani ardhi ipasuke! Bi mkubwa ndo kawa kama Mbogo! Nawaza watu walioniambia mambo yao mazitomazito wakisikia habari hizi toka kwa mzazi wangu kabisaaaaa! Sijui nitaweka wapi lisura langu! Maskini my bro! na my wifi( japo simpendi kama nini toka kitambo!)

HII INAITWA POINT OF NO RETURN AU NO WAY OUT! I AM WAITING FOR A MIRACLE!!!![/QUOTE]
 
Mossadi punguza jazbaaaa! Mimi nimeleta hapa hili jambo linanishinda!, limenizidi! na watu wengi ninaowashauri wangekuwa ushauri wangu hauwasaiidii wasingengangania kurudi niwashauri zaidi na zaidi! Mimi sipendi kushauri ila ndo naombwa ushauri sasa nifanyaje kama naaminika? Wewe haya mambo omba Mungu akuipushie mbali! YAKIKUKUTA UNAWEZA KUOMBA USHAURI KWA MWANAO WA KUMZAAA!

''Yakikukuta unaweza kuomba ushauri kwa mwanao wa kumzaa''.
Unachosema hapo ni kweli kabisa. Hii kitu inapotokea unakuwa na mambo kadha ndani ya kichwa;
1. Kwa jinsi unavomuamini huyo mtu,huamini km kweli amefanya na unajitahidi kuisemea nafsi ''si kweli,hajafanya au alienda kwa mamake, shangazie au rafiki?
2. Sawa, alienda kwa jamaa,did they do it? Sometimes the inner voice tells you alienda lakn hakufanya. Pamoja na kuona hzo pills za kinga bado unajipa matumaini hilo tendo halikufanyika.
3. Unajilaumu km ww ndio cause ya yote hayo. Na kwamba labda usingesafiri(kama ilivyo kwa kakake Lara1)haya yote yasingetokea.
4. Unajipa moyo kwamba, hata ukimrudisha ndani hakuna mwingine ambaye anajua hyo story. Unaona km ni siri yenu ya ndani.
5.Kama unaamua kumrudisha ndani na kuamua kuanza maisha upya, mlinzi na hsegal lazima waondoke. Coz nyie linaowahusu mtafanya siri,lakn hao wawili watafanya ndio story ya kuwaambia majirani.
6.Katika maamuzi magumu km haya hutakiwi kusikiliza rafiki au ndugu anasema nn. Mara zote ndugu huwa na maamuzi ya haraka na jazba na kumuona aliyekosa ni mdhambi sanaaa. Lakini hawajui km ni kaka yao keshatoka nje ya ndoa mara ngapi. Na ku-maintain ur innocence hutosema mapungufu yako.
SASA;
1.Kama ilishatokea hata cku moja na wewe uli-cheat, hakuna haja ya kumuacha au kumfukuza hyo mwanamke. Pia usimuweke mawazoni hyo jamaa anayekuzunguka coz sthing bad might happen,u might even kill him if u're not psychologically strong.
2.Katika issue kama hii,funga macho,ziba maskio toa maamuzi ww mwenyewe km ambavyo ''inner voice'' inavokushauri usifuate ushauri wa mtu.
3. Kama umeamua kuendelea na mwanamke ktk situation kama hii,usifanye kosa la kurudiarudia kumsema hyo mkeo kwamba ''ndio maana unat..ovyo, we malaya tu'' nk. Ukifanya hivyo hakuna maisha tena hapo.
4.usifanye kosa la kumrudisha halafu ukaamua kwamba ss na mm nimkomoe kwa kutafuta ndogo(km ilikuwa haipo) thatz a grave mistake most people do.
Kumuacha hyo mwanamke ktk tension km hyo haitasaidia bali itafanya mambo kuwa worse kwa upande wako. How far are u sure that the next woman will be a perfect one for u? What abt ur kid? She can be a good wife but not a good mother.
It is just a professional advice to Lara1..
 
Ulichosema Tram Almasi ni kweli kabisaaaa! Ndo mtu unapojua ishu ya kusamehe 7*70 ni nzito sanaaa!
 
Sijui maana Bado kumfumania, kaka ako Naye *****, maanake inakuwaje Mlinzi na dada wajue halafu yeye asijue? Nyumba ilishamshinda mda mrefu sana.

Usiseme hivo Uttoh! Kaka yangu ni the best husband ever! Alimuamini mkewe 100% alafu kazi zake ni za kusafirisafiri, sasa alikuwa akirudi safari hapelelezi kama mkewe alijituliza au alikuwa anakitembeza! Hata kama ingeokea mtu kumwambia mkewe mzinzi bila kumfuma, na wifi kukiri kwa kinywa chake asingeamini katu katu tena mngegombana vibaya!

Wifi nae ni msaniii huyooo! Kwa kujifanya mke mwema hana mpinzani! Kila siku kunipigia kelele niolewe nazeeka! Kumbe nae ndoa yamshindaa!
 
Kwa hiyo ukimuacha unazani ni rahisi? KWANZA UNAONEKANA MAUJUZI YA 6 BY 6 HUNA NDO MAANA WIFE KAENDA KUKIGAWA HUKO NJE! Na hata ukimuacha your life will never be the same again!!! ACHENI TUU YAKIKUFIKA HAKUNA RANGI UTAACHA KUIONA!

Acha tu!!! Huyo Bro wangu ni mtata, kidume cha mbegu!!! Ila alikuwa mdogooooo kama piriton! Au kuku alinyeshewa mvua! Michozi tu inamtoka kama mtoto mdogo! kabaki WHY ME GOD! WHY ME! WHAT HAVE I DONE THAT IS SO WRONG TO DESERVE ALL THIS?, si mtu wa church ila maandiko aliyakumbuka! Hayo maneno kayarudia zaidi ya mara 100. Acheni tu ndo nikajifunza cheating za BF na GF sio za kwenye ndoa!

Akikufuma na yeye anakata dudu yote si ndio?

Du lara 1 umenikumbusha Natalia alipigwa Ban sijui kapotea wapi
nakubaliana na wewe kabisa kuwa Kaka yako kwenye 6x6 hajiwezi au Dushelelee ni ndogo, huyo Maza wenu usingemwambia kwani anayajua madhaifu ya kaka yenu ndio maana kachukia.
Kuna Nabii mmoja aliletewa mwanamke muasherati akiambiwa atoe Hukumu, kawaaambia na asiyefanya aliyoyafanya haya na ampige jiwe wote waliondoka na hawakumpiga yule mwanamke hata na yeye .................. ila alimuandikia msg kwenye mchanga na mwanamke akamshukuru
 
Last edited by a moderator:
Ulichokiandika hapa nikifananisha na username yako Mossad napata picha unafanya kazi sehemu fulani! Wale pia wanapenda umbea umbea.......
Hii kitu yako nimeisoma halafu inaonyesha japokuwa ulianza kwa kusema wewe huwa hutoi hizo siri za watu lakini ukweli ni kwamba wewe sio mshauri mzuri na unapenda sana umbea kujua matatizo ya watu halafu uyatangaze kama ulivyofanya kuja kuyatangaza hapa matatizo ya huyo bro wako. Pia Bi mkubwa wako ni kichwa sana, anajua weakness yako hiyo, akaamua kukukataza na alijua ww ni mgombanishi na muuaji, kama ni mimi nisingeweza kumshauri bro wangu aendelee kuishi na muasherati wa aina hiyo, ulivyoanza kuandika uliwashauri watu waoe/waoane ili kuepuka uzinzi halafu tena umemshauri bro wako aendelee kuishi na huyo mzinzi sasa ndo nini? Ushauri wangu kwako ni kwamba usiwe unapenda kujiingiza na kutoa ushauri wa matatizo serious kama hayo kwa wanandoa au wapenzi maana mwisho wa siku lazima wewe uje kuonekana mbaya na tabia yako ya umbea siyo nzuri kijana.
 
Back
Top Bottom