Nini cha kufanya ukimfumania mkeo redhanded huku bado unampenda!!!!!

Refer to the heading.
Binafsi nikimfunania wife wangu redhanded kwa kuwa nampenda sana, sitomuua nitamtaliki bila kutoa uahai wake.
Kumwachia uhai wake ndiyo feva ambayo nitampa kwakuwa nampenda sana.

Mimi kwakuwa nampenda sana sitataka kujiongezea jeraha lingine la kumuacha, nitakachokifanya ni kumgombeza kwamba alichokifanya ni kitu kibaya sana asirudie tena maana sipendi hiyo tabia na nitaendelea kuishi naye.
 
siku hyo hyo ndio nitajua cha kufanya. AMEN
Hii ni mbaya sn. Wewe unaonyesha waweza kum-Mwangosi mtu aisee!
Lazima uwe na contingency plan ya ishu kama hiyo in case inatokea. Maamuzi ya ghafla ni hatari sn!
Mimi binafsi kwavile sijawahi kukumbana na ishu ya aina hii nitatoa nafasi ya pili baada ya kumkoromea ajabu!...na sharti mojawapo la kumsamehe ni kumleta nyumbani yule jamaa mdokozi.
 
lol pole lara 1 kwa yaliyokusibu, sasa mbona hutupi feedback bado maza yuko na simu yako? na ishu imeishaje? makubwa haya. Pole kwa bro na wifi yako pia ila kwanini bro wako hamuambii matatizo yake bi mkubwa? na anakuamini sana wewe ilhali hauko kwenye ndoa?
 
Mungu anisaidie yasinitokee, kwani naweza kumpiga mpaka afe kama siyo kuzimia...nafikiri hii ni siku ambayo sitaisahau na hataisahau.......Me ameniuzi kabisa, yani nimeuzika....APEWE LIKIZO KWANZA, HAIPENDEZI...MKE WANGU ANALALA NJE SIKU NNE? AMEDHAMIRIA KABISA

Kuku akisha lala nje huyo si kuku tena anakuwa Kanga.
 
hapa lazima majibu yatakuwa
1.nitamuua
2.kwanini anidharau kiasi hiki
3.nitamuolea mke mwingine
4.malaya tu huyo niendelee kuishi nae ili iweje
5.namtimua ndani kwangu watoto naweka housegirl awalee
6.natafuta huyo jamaa yake lazima nimfanyizie
7.nampa talaka
8.ataendelea kuishi na mimi lakini nampotezea kama mwaka hivi
9.tutatengana vitanda
10.nampeleka kwa wazazi wake na kuwaeleza upuuzi aliofanya mtoto wao
KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHARISHA enh!wanaume bana!
 
Refer to the heading.
Binafsi nikimfunania wife wangu redhanded kwa kuwa nampenda sana, sitomuua nitamtaliki bila kutoa uahai wake.
Kumwachia uhai wake ndiyo feva ambayo nitampa kwakuwa nampenda sana.

Na akikufuma weye je?
 
Hii ni mbaya sn. Wewe unaonyesha waweza kum-Mwangosi mtu aisee!
Lazima uwe na contingency plan ya ishu kama hiyo in case inatokea. Maamuzi ya ghafla ni hatari sn!
Mimi binafsi kwavile sijawahi kukumbana na ishu ya aina hii nitatoa nafasi ya pili baada ya kumkoromea ajabu!...na sharti mojawapo la kumsamehe ni kumleta nyumbani yule jamaa mdokozi.

Mbavu sina kabisa hapa Eti (kum - Mwangosi) dah! watu mna masihara..
 
Naomba Mungu isinikute!!! Kama ni cheating ifanyike ila nisijue kabisa sembuse kulala nje siku 4 ambayo mimi sijawahi fikiria kufanya!!!! Mungu aepushie mbali kwa sababu nina hakika nitapalekwa Segerea!!!
 
Ushauri wangu kwa mleta mada lara 1, kimsingi hili litaisha ila ktk maisha yangu***nimewahi kukutana na usemi CHOCHOTE CHENYE MIGUU MIWILI DUNIANI HAKIPASWI KUAMINIWA***, LAKINI KTK SIRI HAKUNA MWANAMKE ANAYEWEZA KUTUNZA SIRI...KUMBUKA ENZI ZA DELILA NA SAMSONI....ME NAKWAMBIA HIVI UKITAKA USIHARIBU UHUSIANO WA WENGINE TENA USISEME, USIMWAMINI MWANAMKE KTK SIRI YEYOTE ILE...NEVER IN YO WHOLE LIFE....NINA EXPERIENCE YA KUTOSHA JUU YA HILI...
 
Kwa vile unampenda, wasiliana na Jeshi la Marekani ili wammalize kwa drone.

Utabaki na mapenzi yako na utakuwa umepata ufumbuzi/dawa ya wivu wako.

Kama hilo ni gumu, mrudishe ilikomtoa. Kama ulimpata baa, mrudishe baa uliyomuopoa. Kama kwa wazazi wake, warudishie ili wamfunze heshima na kusitiri nyeti zake.

Au "declare" open relationship!!!

Kama na wewe huwa unakosea siku nyingine (unaibia ibia) basi chukulia kuwa ngoma ni "draw". Wewe bahati yako huhitaji morning pills,ushahidi wa kuwa unaibia(unateleza, kufanya kosa, oh bahati mbaya...bla bla )

Huu ushauri wako wa 1&2 ni lazima umuache jumla jumla, bila hivo UTAJIAIBISHA KINOMAAAA! Jst i magine hapo umeleta DRAMA kibao za kumrudisha kwao afu mnayamaliza!!!!! Watu wanajua alimegwa! na wewe unaendelea kumega! WALE WASHKAJI ZAKO VICHECHE HAWAACHI KUJARIBU ZALI KWA KUMTOKEA!!!!! Lamsingi ni kuamua fasta UPO au UMEJITOA!
 
Yaani sitaki hata itokee nadhani sitakuwa na hamu nae teeeeeeeena, sababu mie sijawahi toka nje ya ndoa yangu seven yrs now!! Aisee mungu ataniusamehe tu hata km ni ndoa ya kanisani sitaweza kula tena ile kitu nikijua kuna mtu alitema cheche zake pale khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Kwa hiyo ukimuacha unazani ni rahisi? KWANZA UNAONEKANA MAUJUZI YA 6 BY 6 HUNA NDO MAANA WIFE KAENDA KUKIGAWA HUKO NJE! Na hata ukimuacha your life will never be the same again!!! ACHENI TUU YAKIKUFIKA HAKUNA RANGI UTAACHA KUIONA!
 
Kwa vile unampenda, wasiliana na Jeshi la Marekani ili wammalize kwa drone.

Utabaki na mapenzi yako na utakuwa umepata ufumbuzi/dawa ya wivu wako.

Kama hilo ni gumu, mrudishe ilikomtoa. Kama ulimpata baa, mrudishe baa uliyomuopoa. Kama kwa wazazi wake, warudishie ili wamfunze heshima na kusitiri nyeti zake.

Au "declare" open relationship!!!

Kama na wewe huwa unakosea siku nyingine (unaibia ibia) basi chukulia kuwa ngoma ni "draw". Wewe bahati yako huhitaji morning pills,ushahidi wa kuwa unaibia(unateleza, kufanya kosa, oh bahati mbaya...bla bla )

Wewe acha tu! Jst imagine kuanzia baada ya hilo tukio unaonekana MUME *****! Hakuna kikao cha baa hutojadiliwa! Hakuna mtu atakae kuomba ushauri coz yako yamekushinda yake ndo utayaweza? Hakuna kitu utakachosema kionekane cha maana! Your life will never be the same again!
 
Hii kitu yako nimeisoma halafu inaonyesha japokuwa ulianza kwa kusema wewe huwa hutoi hizo siri za watu lakini ukweli ni kwamba wewe sio mshauri mzuri na unapenda sana umbea kujua matatizo ya watu halafu uyatangaze kama ulivyofanya kuja kuyatangaza hapa matatizo ya huyo bro wako. Pia Bi mkubwa wako ni kichwa sana, anajua weakness yako hiyo, akaamua kukukataza na alijua ww ni mgombanishi na muuaji, kama ni mimi nisingeweza kumshauri bro wangu aendelee kuishi na muasherati wa aina hiyo, ulivyoanza kuandika uliwashauri watu waoe/waoane ili kuepuka uzinzi halafu tena umemshauri bro wako aendelee kuishi na huyo mzinzi sasa ndo nini? Ushauri wangu kwako ni kwamba usiwe unapenda kujiingiza na kutoa ushauri wa matatizo serious kama hayo kwa wanandoa au wapenzi maana mwisho wa siku lazima wewe uje kuonekana mbaya na tabia yako ya umbea siyo nzuri kijana.

Mossadi punguza jazbaaaa! Mimi nimeleta hapa hili jambo linanishinda!, limenizidi! na watu wengi ninaowashauri wangekuwa ushauri wangu hauwasaiidii wasingengangania kurudi niwashauri zaidi na zaidi! Mimi sipendi kushauri ila ndo naombwa ushauri sasa nifanyaje kama naaminika? Wewe haya mambo omba Mungu akuipushie mbali! YAKIKUKUTA UNAWEZA KUOMBA USHAURI KWA MWANAO WA KUMZAAA!
 
nawasalimu wadau wa jf!

Mimi ni mzima na wikiend nilikua gonjwagonjwa imelala kitandani, si mwajua dozi na maji ya dhahabu haviendani.

Back to the main topic, waungwana mliioa na kuolewa nawapa big up kubwa sana kwa kuachana na uzinzi usio wa lazima (watu mnapendana alafu hamuoani kazi kuzini tu! Na kuongeza msururu wa dhambi wakati wa kitubio), na nyie mabachelor kama mimi, kama mna wapenzi oaneni, uzee waja, na ambao hamjabahatika nawaombea kwa mola muwapate wenzenu.


Mimi sijaolewa, wala mtoto hata wa kusingiziwa sina, ila born town kitambo, na cha kushangaza ndugu zangu na marafiki zangu wengi sana walioolewa/kuoa na waliojipasishia watoto wa watu/waliojipeleka kwa waume zao, wanaifanya mimi comfidant wao sana kwa kunieleza mambo mazito ya ndoa zao, na mimi ni mshauri mkubwa sana kwao. Hii hali maza wangu haipendi kinoma, anadai itanifanya niogope ndoa, hivo akijua mtu ananiomba ushauri anaenda kumpashua, atafute mwanandoa mwenzie amshauri. Utasikia "kama huipendi ndoa yako we sikiliza ushauri wa huyu mtoto, yeye hata kumpata mtu amuweke ndani bado atakushauri nini?" hajaishia hapo kapiga biti ukoo mzima no mtu kuniomba ushari. Na mimi tumekubaliana nikimshauri mtu tena tunakosana jumlajumla, nikamuahidi kazi ya mama ushauri mimi basi!

Kweli mimi nina moyo wa kuacha hii kazi! Ila naipenda sana haswaa part ya kupata maumbea ya ndani kwa watu, si mnajua tena watu unaweza kuwaona wako perfect kinoma, wanakurusha rohooo, ila wakija kukuconsult mazito ya ndani mwao unabaki unaguna tu! Nikiacha hii kazi nitakosa uhondo!( sitangazi kwa mtu ila nafaidi mwenyewe tu umbea)

baada ya kutoa ahadi ya kutokushauri mtu tena, jana usiku mida ya saa 4, kaka yangu kabisa kabisa kanipigia simu kuwa kamfumania mkewe wa ndoa ya mwaka! Ishu yenyewe ilikuwa hivi, bro kasafiri kikazi, sasa akamwambia mkewe anarudi leo jpili, afu wanaaminiana kinoma, sasa kazi zikawahi kuisha, hivo akaona arudi jmosi amuwahi mamsap na baby girl (2yrs) ila hakumwambia mkewe wala nini.

Kufika getini mlinzi kamtolea mijicho kama kabanwa na mlango, kumfokea ndo kafungua geti, akahisi kuna ishu lazima! Hausgeli nae hamwangalii machoni, mke hayupo, kumuulizia beki tatu anababaika mara kaenda dukani, mara kamsindikiza mgeni, ming u saa 7 hiyo. Akwaita beki tatu na mlinzi akawaambia waseme ukweli lasivo asubuhi kazi basi! Mlinzi akaanza kutiririka bwana mkeo kaondoka hii siku ya 4 hajalala hapa! Beki tatu anaulizwa kweli? Kimyaaa! Akachukua simu zao, akawaambia wakalale.

Saa tano leo jpili wife karudi kwa mbwebwe, hapo kashatuma sms kwa beki tatu apike pilau mr. Anarudi. Ile kufika namkuta mr. Kwenye kochi, si ndo presha kupanda na kushuka! mume kamtega niambie ukweli wote bila kuficha nitakusamehe manake najua hujalala siku 4! wifi nae sijui uoga, sijui ubwege, sijui ushamba hata sielewi, si kafunguka a to z. bila kupindisha ukweli wowote na kuomba msamaha dobledoble! Kamtaja hadi bwana wake, wana uhusiano toka lini, na mengine kibao yenye kumteketeza zaidi.! Bro kuzama kwenye pochi si ndo kakuta the pills after hizi ndo zile dawa kama umecheza kavukavu ndo unameza kabla ya 72 hrs hupati mimba. Hivo inaelekea wifi hakutumia kinga huko kwenye uasherati wake.( can u imagine na ukimwi wote huu!)

basi bro akamwambia we ondoka, nisije kukua bure! Akanipigia njoo haraka, nikamwambia mie naumwa mwenzio kwani vipi!? Kama huji utakuta kaka yako nimejinyonga na usije kwenye mazishi yangu! Mtumeeee! Nikakurupuka kwenda kwake ndo kunielezea a to z na kutaka ushauri. Nikakumbuka moyoni nishamwambia maza mi sishauri tena, ila nikabullshit nikasema huyu kaka yangu wacha nimshauri.

Nikamwambia kweli hayo mambo ya aibu bro, tena yataudhalilisha uume wako haswaa, ila nyie mna ndoa ya kanisani, na najua unampenda mkeo, pamoja na yote hasira tu ndo zimekubana, huu ndo wakati wa kuwa mwanaume haswaa! Mtizame mwanao 2yrs only, sote binadamu, yeye kateleza ila kuvunja ndoa si sahihi, istoshe wanawake wote wanaksoro. Na kwanza hukumkuta bikra, so we kaza roho. We mtext arudi, usimuulize chochote, endelea kuishi nae kama zamani dhamira yake itamla itammaliza.
Nikamsisitiza hili jambo asimwambie yeyote, tuwe tunalijua watatu tu mimi, yeye na wifi. Sababu wakijua watu wengine alafu asipomuacha atajiaibisha zaidi tu. Akanielewa akamtext nikamuacha wifi karudi yamepo.

Jioni maza kaanza kunipeleleza kuwa mbona kaenda kwa bro hakueleweki, kama kuna jambo na haambiwi! Niknyuti mi sijui lolote! Akaninganganiza wewe watakuwa wamekuomba ushauri!, niambie mimi mzazi wenu ujue, sio vizuri, hata kama umeshauri pamoja na kukutaza sitokasirika niambie! Si ndo nikafunguka!

Weeeee! Najuuuta! Maza akapaniki, yaani unamshauri mwenzio alee uzinzi aje kufa na ngoma? Utanizalia mtoto mkubwa kama yule wewe? Hivi unaona aliyofanya wifi yako mazuri? Msinichezeee! Haiwezekani, huyo muasherati aondoke na mengine mengi!

Na wewe (mimi) nilikwambiaje kushauri watu? Kwanini hukumshauri aniambie mimi mzazi wake? Sasa kukukomoa nyie si mmefanya siri ya watu 3 nawaambia ndugu na marafiki woteee, afu nasema ni wewe ndo umeuza mkanda! Tena natahadharisha wewe ni mmbea mkubwa watu waskwambie tena mambo yao! Ndo dawa yako hii! Hapo kanipora simu yangu na kujifungia chumbani! Sijui atawatext au atapiga.

Kichwa kinaniuma! Natamani ardhi ipasuke! Bi mkubwa ndo kawa kama mbogo! Nawaza watu walioniambia mambo yao mazitomazito wakisikia habari hizi toka kwa mzazi wangu kabisaaaaa! Sijui nitaweka wapi lisura langu! Maskini my bro! Na my wifi( japo simpendi kama nini toka kitambo!)

hii inaitwa point of no return au no way out! I am waiting for a miracle!!!!

a walk of shame!!jf balaa tupu
 
Naomba Mungu isinikute!!! Kama ni cheating ifanyike ila nisijue kabisa sembuse kulala nje siku 4 ambayo mimi sijawahi fikiria kufanya!!!! Mungu aepushie mbali kwa sababu nina hakika nitapalekwa Segerea!!!

Acha tu!!! Huyo Bro wangu ni mtata, kidume cha mbegu!!! Ila alikuwa mdogooooo kama piriton! Au kuku alinyeshewa mvua! Michozi tu inamtoka kama mtoto mdogo! kabaki WHY ME GOD! WHY ME! WHAT HAVE I DONE THAT IS SO WRONG TO DESERVE ALL THIS?, si mtu wa church ila maandiko aliyakumbuka! Hayo maneno kayarudia zaidi ya mara 100. Acheni tu ndo nikajifunza cheating za BF na GF sio za kwenye ndoa!
 
Back
Top Bottom