Uchaguzi 2020 Ningekuwa Makonda ningesubiri mpaka 2025

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,916
24,674
Ndugu Paul Makonda Ukuu wa mkoa ndio ulikuwa unampendeza na kumpa mamlaka ya Nguvu kuliko huo Ubunge anaouhitaji,

Japokuwa Ukuu wa Mkoa ni nafasi inayotegemea mteuaji ameamkaje kwa siku hiyo(haikupi uhakika kwamba utakuwa ofisini siku ya kesho) lakini kwangu Ukuu wa mkoa ilikuwa ndio nafasi pekee ya kutamba kwake ukizingatia aliweza kula vizuri na boss wake hivyo kwa vyovyote vile alikuwa na uhakika wa kuwa tena mkuu wa mkoa kwa wakati mwingine tena.

Sujui target yake kwa sasa labda anautaka ubunge ili akawe waziri kwenye wizara flani sijui.

Lakini ata akiupata na kuwa waziri hatakuwa tena makonda yule aliyejitwalia mamlaka ya ukuu wa mkoa.

Alivyokuwa mkuu wa Mkoa kila kitu chini ya mkoa husika yeye ndio alikuwa mpangaji mwenyekiti wake chini ya kamati .
Kuanzia kwenye kamati ya ulinzi ya mkoa mpaka kwenye bajeti.

Sasa hivi anautaka ubunge ambao mamlaka yake yanaishia kwenye Jimbo tu ambalo akishachaguliwa na siku akitaka kufanya Mkutano na wananchi lazima aombe kibali kwenda kwenye kamati ya ulinzi ambayo mkuu wa mkoa ndie mwenyekiti wake

Na kama mkuu wake wa mkoa ni namna gani vipi anaweza kutoa Amri ya kukataza na ikatokea akakaidi anakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kufanya mkusanyiko bila kibali.

Binafsi naona Amekosea kuzichanga karata zake vyema ni bora Angebakia kuwa mkuu wa mkoa na baadae mara baada ya boss wake kumaliza muda wake wa uongozi kikatiba ndio angejitupa huko kwenye Ubunge,

Angefanya hivyo Kwa sababu ya kujilinda kwa wakati huo kwa kuwa ingekuwa vigumu kwake kujua boss mpya anaekuja atakuaje.

Sijui kwa yeye aliwazaje au ana mkakati gani lakini ingekuwa ni mimi ningesubiri mpaka 2025 ata kama mshahara haukidhi mahitaji.
 
Kumdharau mtu ilihali maisha yake yanakwenda vyema zaidi hata ya wewe ni kama kukosa cha kusema na kazi ya kufanya..MUNGU siyo mzee Jolijo hata amuache yule unaye mchukia
ila hapa umeongea kweli kabisa. binafsi kuna viongozi siwakubali kabisa kwa sababu zangu, lakini kila nikifikiria jinsi walivyonizidi katika maendeleo na hata katika kuzipata tu hizo nafasi walizonazo, inabidi nitulie tu na kujizuia kutoa maneno makali kama hilo.
 
Kazi rasmi ya Makonda haikuwa ukuu wa mkoa. Katika kazi yake rasmi Makonda amekuwa "burned" na USA, kwa hiyo inabidi aondoke.

Swali la kujiuliza ni kwamba, huyo anaekuja anachukua pia kazi rasmi ya Makonda?
Burned"" 😂😂😂😀 wote hao watoto wa baba mmoja
 
Akipata Ubunge anapata sifa za ziada ikiwemo kuwa Naibu Spika au Waziri Mkuu tofauti na Ukuu wa Mkoa.
 
Ukute boss wake ndiyo kampa go ahead, Mnyeti pia
nami ninaamini hv, anavyojua kujipendekeza kwa jiwe ataanzaje kufikia uamuzi mkubwa hivyo pasipo kumshirikisha?!

Jiongeze...hapo atahakikisha bashite anashinda kiti cha ubunge halafu cku moja jiwe anatoka hadharani anatuzuga kama vile hahusiki kwamba bashite angekosa ubunge asingempa teuzi nyingine!.
 
Ndugu Paul Makonda Ukuu wa mkoa ndio ulikuwa unampendeza na kumpa mamlaka ya Nguvu kuliko huo ubunge anaouhitaji,

Japokuwa ukuu wa mkoa ni nafasi inayotegemea mteuaji ameamkaje kwa siku hiyo(haikupi uhakika kwamba utakuwa ofisini siku ya kesho) lakini kwangu Ukuu wa mkoa ilikuwa ndio nafasi pekee ya kutamba kwake ukizingatia aliweza kula vizuri na boss wake hivyo kwa vyovyote vile alikuwa na uhakika wa kuwa tena mkuu wa mkoa kwa wakati mwingine tena...
Keep cool anaye chezesha mwanasesere ataicheza ngoma mwenyewe.
 
Back
Top Bottom