Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Upo sahihi kabisa, ndiyo maana kwenye sentensi yangu ya mwisho nimesema kwamba Kikwete ana mapungu mengi, lakini hili la uzio si hoja kabisa ya kuijadili kwenye level ya kujiuzuru. Ndiyo maana nasema tulete hoja nyingine zenye great impact kwa nchi na kwa watanzania kwa ujumla wao. Sasa hoja ya ukuta imeathiri nini katika uchumi au maisha ya watanzania?Mkuu ukiona mpaka mtu ameamua kuandika hivyo ni kuwa ameshayasikia na kuyaona mengi kuhusu utendaji kazi wa raisi wetu.Huu bila shaka ni kama mfano mmoja tu wa udhaifu unaoongelewa na watanzania wengi.
Naamini mleta mada ametafakari mambo mengi na inawezekana hili la uzio hapo jangwani limeamsha hisia zake alizokuwa nazo tangu siku nyingi.
Mwisho na wewe kama unafuatilia vizuri utendaji kazi wa huyu mkuu wa nchi utakubaliana na mawazo ya wengi kuwa huyu bwana ana mapungufu kiutendaji.