Ningalikuwa Kikwete, ningaliwateua mawaziri wengi kutoka Zanzibar

kama jinsi ambavyo hawawezi kula rushwa ndivyo hivyo hivyo hawawezi kufanya kazi. Ni wazanzibari wachache wamekuwa viongozi wazuri bara, wengi hamna kitu.

Teh teh teh,,,, huyu ndo akili yake inavyomwambia kuwa, kwasababu kiongozi hawezi kula rushwa basi hawezi kuongoza, anaeweza kula rushwa ndio kiongozi mzuri! He is really a great thinker!! Ihi ihi ihihihi
 
We sio mzima kimawazo kabisa. Yaani uwalete wazenji huku kwetu wafanye nini? Hao jamaa wote uliowataja nafasi zao hazina chance za kupiga mafungu ya maana lakini ndani ya uongozi wa CCM hakuna ambaye siyo mwizi inabidi utambue hilo. Mbona katika uliowataja hujamuweka Mwinyi au yeye ni kutoka Bongo? najua umem-skip kwasababu ukimuweka tu ktk hiyo list maovu yake yanawafunika woooote hata kama wangekuwa wasafi.
Hao unaotaka kuwaleta huku wachukue wapeleke kwa Boko-haramu au Al-shabaab huko usituletee balaa lako hapa wadini nyie.

Kwenu? Kwenu wapi kwani? Tanganyika? Tanganyika si mumeikana nyinyi wenyewe!! Au JMT ndo yenu? Wazanzibari wana haki ya kuwemo katika wizara za JMT! unless iwe serikali ya tanganyika.

Mbona hizo propaganda za zamani, boko haram sijui al shabaab, hivi wewe una elimu japo ya darasa la 7? Mana propaganda za ovyo sana, kwaiyo kwamba mkiwanyima wanachotaka ndo kutakuwa hamna boko haram? Akh! Umenifanya nicheke sana, hivi kweli mawazo yako yanakubalika na wengi? Maana nijuavyo mimi mtu ukimnyima jambo ndo huwa mkorofi ukimpa hutulia! Sasa wizara ya ndani kachukua mzenji boko haram al shabba fiyl al qaeda, nafikiri ana mpango wa kuripua zile tower za BOT na ameandaa mtu wa kuripua pantoni :D bwahahahaa
 
Kwa miaka mingi, wateule wa rais wa Muungano wakitokea Zanzibar basi kuhusu rushwa rais huwa hapati tabu.
Sijabahatika kusikia Mzanzibar ndani ya Muungano akiwa mlarushwa kama wanavyokuwa watz bara wanapoteuliwa.
Nngalikuwa Jk.ningaliangalia jambo hili kwa ukaribu zaid

1)Dk Omar Ali Juma
2)Dk Mohd Shein
3)Dk Gharib Bilali
4)Shamsi Nahodha - Mambo ya Ndani
5)Ali Ameir Mohd - Mambo ya ndani iliopita
6)Samiha Suluhu
7)Mahadhi Juma Maalim
8)Ali Seif Khatib
...
....
...
......
......
........na wengine wengi

HAPA NAAMANISHA WANAPOKUWA TANZANIA BARA. NAJUA WANAPOKUWA ZANZIBAR HUWA HAWANA HAYA WALA HAWAONI VIBYA KULA RUSHWA

Yakhe! umesahau skandali za Hassan Diria? Au ulikuwa kinda wakati huo?
 
Back
Top Bottom