Zanzibar 2020 Nguvu ya Dodoma katika maamuzi ya Urais wa Zanzibar (CCM)

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Katika mchakato wa kutafuta mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, Amani Karume, aliyekuja kuwa mgombea wa chama hicho na baadaye Rais wa Zanzibar, hakuwa mgombea aliyeungwa mkono na wengi visiwani humo.

Kulikuwa na kundi kubwa zaidi lililokuwa likimuunga mkono Dk. Mohamed Ghalib Bilal -aliyekuwa Waziri Kiongozi wakati wa utawala wa Dk. Salmin Amour na akidaiwa kuungwa mkono na bosi wake wa zamani.

Inafahamika kwamba Salmin alikuwa nampango wa kutaka kuongezewa kipindi kingine cha kuongoza kama Rais kinyume cha matakwa ya kikatiba. Baada ya juhudi zake hizo kupingwa hadharani, wafuasi wake walihamia kwa Bilal.

Taarifa zilizotoka Zanzibar wakati ule zilieleza kwamba katika wagombea waliojitokeza, Karume alishika namba nne katika mpangilio wa wagombea walioonekana kufaa zaidi kuongoza visiwa hivyo baada ya Salmin.

Hata hivyo, wakati wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM walipopiga kura mjini Dodoma, Karume alipata kura 111 dhidi ya kura 67 alizopata Bilal. Akatangazwa kuwa mgombea.

Ndipo dhana kwamba mgombea urais wa CCM Zanzibar huwa hatafutwi visiwani humo isipokuwa hupangwa na kupigiwa kura na wajumbe wa chama hicho ambao hufanyia mikutano yao katika Makao Makuu ya nchi - Dodoma.

Lakini, je ni kweli kwamba Rais wa Zanzibar huamuliwa Dodoma na kwamba kinachotokea huwa hakina maslahi na visiwa hivyo isipokuwa maslahi ya Tanzania Bara?

Dodoma kama 'machinjio' ya wagombea
Kuelewa dhana hii, ni muhimu sana kuelewa siasa za Zanzibar na kwa hakika kuelewa siasa za nchi nyingi za Afrika ambazo ni visiwa.

Kwa kawaida, kihistoria tangu nyakati za kutafuta Uhuru (Mapinduzi) hadi sasa, Wazanzibari si watu ambao huwa wanakubaliana moja kwa moja kwenye kila kitu.
Tuchukulie mfano wa tukio muhimu zaidi la kisiasa Zanzibar katika kipindi cha miongo sita iliyopita - Mapinduzi ya mwaka 1964. Hadi leo, ukizungumza na Wazanzibari, kuna mgawanyiko kuhusu nini hasa kilitokea na taathira yake.

Ukimsikiliza Maalim Seif Shariff Hamad; mmoja wa wanasiasa wakongwe visiwani humo na ukimsikiliza Ali Karume ambaye ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume utapata picha tofauti kuhusu mapinduzi haya kuanzia malengo yake na taathira zake.

Wazanzibari wengi wana tafsiri zinazokinzana kuhusu jambo hili moja la Mapinduzi.

Angalia suala hilo la Dk. Salmin Amour kutaka kuongeza kipindi kingine cha kutawala. Kwa upande mmoja; humohumo ndani ya CCM Zanzibar kuna waliokuwa wakiunga mkono nakuna waliokuwa hawaungi mkono.

Wakati ule, mwaka 2000, wanasiasa wawili walikuwa mfano tosha wa mgawanyiko huu. Ali Ameir Mohamed alikuwa akitajwa kama mtu aliyeunga mkono jambo hilo huku nyota mwingine wa siasa za Zanzibar wakati ule, Mohamed Seif Khatib, akipinga jambo hilo.

Kuna suala lingine zito la 'kuchafuka' kwa hali ya hewa visiwani Zanzibar kulikosababisha kujiuzulu kwa Aboud Jumbe ndani ya CCM na serikalini.
Huyu alikuwa Rais wa Zanzibar ambaye alilazimishwa kuachia wadhifa wake huo na nyingine zote za kwenye chama kwenye kikao kilichofanyikia - Dodoma.

Lakini, hadi leo, inajulikana kwamba wapo wanachama ndani ya CCM Zanzibar ambao hawakuunga mkono mambo yaliyokuwa yakifanywa na Jumbe kiasi kwamba ndiyo walioviarifu vyombo vya dola kuhusu kinachoendelea.

Kwa hiyo, hata jambo hilo la Jumbe ambalo nalo limekuwa likisemwa kama ni ushahidi wa kuonyesha namna 'Dodoma' inavyofinya maslahi ya wagombea; halikuwa jambo lililoungwa mkono na Wazanzibari wote.

Kwa hiyo, tatizo kubwa la Zanzibar si Dodoma bali ni mgawanyiko wa kisiasa ambao hutokea kwa karibu kila jambo kubwa linalotokea.

Hata mwaka 2000 wakati Amani Karume anamzidi Bilal, kulikuwa na mvutano wa makundi ya vijana na wazee; Karume akivutia damu changa kwenye chama na Bilal akiwa kipenzi cha wale wakongwe.

Dodoma na CCM Bara
Kama Edward Lowassa angekuwa Mzanzibari, ni wazi kwamba leo kitendo cha jina lake kukatwa Dodoma kingeweza kuchukuliwa kuwa ni ushahidi mmoja wapo kwamba mji huo haujali maslahi mapana ya kisiasa ya Zanzibar.

Lakini Lowassa ambaye alikuwa kipenzi cha wajumbe wa vikao vya juu vya CCM hakupitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Mwanasiasa huyo baadaye alihamia upinzani na kugombea urais Oktoba 2015 na kushindwa na rais wa sasa John Magufuli. Lowassa hatimaye alirejea CCM mwaka 2019.

Mwanasiasa mwingine ambaye anaweza kulalamika pia kuhusu Dodoma ni John Samuel Malecela; aliyepata kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na mwanasiasa ambaye kuna kipindi alipewa jina la tingatinga la kisiasa kutokana na umahiri wake wa kufanya shughuli za kisiasa.

Kati ya mwaka 1995 hadi 2005, Malecela - ambaye ni mzaliwa wa Dodoma, alinyimwa fursa mbalimbali za kuwania nafasi nyeti za uongozi kwa uamuzi uliokuwa ukichukuliwa kupitia vikao vya CCM vilivyofanyikia Dodoma.

Katika mahojiano na mwandishi wa makala hii, mtoto wa Malecela, Mwele, alieleza kwamba baba yake aliumizwa na matukio hayo lakini imani yake kubwa kwa chama ndiyo iliyomfanya abaki pasipo kuhama.

Malecela hakuwahi kulalamika hadharani kuhusu alichofanyiwa na chama chake wala 'roho mbaya' ya maamuzi ya Dodoma.

Je, nini hutokea Dodoma?
Ingawa Lowassa alionekana kuwa mwanasiasa aliye kipenzi cha wana CCM wengi mwaka 2015, vyombo vya kichunguzi vya chama hicho vilishauri chama kwamba mgombea ambaye angekipa ushindi wa uhakika ni mmoja tu; John Magufuli.

Katika uhai wake, chama hicho kimekuwa nautaratibu wa kufanya uchunguzi kuhusu watu wanaotafuta nafasi za juu za uongozi na mwishowe mtu anayeonekana na sifa za kushinda uchaguzi, ndiye ambaye hatimaye hupewa nafasi hiyo.

Kwa hiyo, vikao vya mwisho vya Dodoma huwa ni hitimisho tu la safari ndefu ambayo chama hukipitia katika kumtafuta mgombea anayefaa na atakayekiuza chama hicho.

Katika kueleza hili, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, alipata kusema kwamba kazi ya kwanza na muhimu kulizo zote ya chama cha siasa ni kushinda uchaguzi. Huyu ni mtu ambaye alikuwa Katibu Mtendaji wa kwanza wa CCM.

Kinyang'anyiro cha Zanzibar 2020
Ingawa CCM haijatangaza rasmi majina matano yatakayopelekwa Dodoma kwa ajili ya uamuzi wa vikao vya juu vya chama hicho; inaaminika kwamba makada watano; Dkt. Hussein Mwinyi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Dkt. Khalid Salum Mohamed, Shamsi Vuai Nahodha na Hamisi Mussa ndiyo waliopewa alama za juu na vikao vya Zanzibar.

Uchaguzi wa mwaka huu umezua mjadala kutokana na idadi kubwa ya wagombea walioonyesha nia ya kutaka kurithi nafasi ya Dkt. Ali Mohamed Shein. Wagombea 32 walijitokeza; rekodi katika siasa za Zanzibar.

Mshindi katika mchakato huu wa ndani ya CCM ndiye antarajiwa kushindana na mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo, Seif Shariff Hamad, anayetarajiwa kupitishwa na chama chake kuwania nafasi hiyo.


Pamoja na idadi hiyo kubwa, viongozi wa chama hicho hawakupata taabu kuchagua waliofaa. Taarifa kutoka ndani ya vikao vya Zanzibar ziimeonyesha kwamba kuna wajumbe ambao hawakuwa na nia hasa ya kutaka Urais lakini walitaka tu kutumia nafasi hiyo kujitangaza.

Wagombea hawa watano wana sifa na uzoefu tofauti katika siasa za Zanzibar; Mwinyi -mtoto wa Rais wa pili wa Tanzania; ni mwanasiasa mwenye uzoefu wa miaka takribani 20 kama mbunge na waziri katika Serikali ya Tanzania.

Profesa Mbarawa ni msomi aliyewahi kufanya kazi ndani na nje ya nchi kwa muda mrefu na amekuwa waziri kwenye serikali ya Rais Jakaya Kikwete na ya sasa ya Rais Magufuli.

Shamsi amewahi kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar kwa muda wa miaka kumi na amepata kuwa waziri wa wizara tofauti katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Khalid ni mchumi aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na Katibu Mkuu wa wizara hiyo na ni miongoni mwa wanasiasa wanaoelezwa kuwa na ubongo unaochemka katika masuala ya uchumi.

Mussa amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi kwa takribani miaka 16; akianza wakati wa urais wa Amani Karume na kuendelea na Dk. Shein. Anatajwa kama mmoja wa wachumi mahiri wa Zanzibar.

Hata hivyo, Dk. Mwinyi anatajwa kuwa mgombea anayekubalika zaidi miongoni mwa watano hao. Ndiye mgombea anayejulikana zaidi, mwenye mtandao mkubwa zaidi marafiki, asiye na kashfa ya kisiasa na anayeonekana amejiandaa muda mrefu kwa nafasi hiyo.

Amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM; chombo cha juu zaidi cha maamuzi cha chama hicho kwa muda wa miaka kumi na hivyo anajuana na wapiga kura wengi kuliko wenzake.

Shamsi anaonekana kuwa amepita katika siku zake bora- huku Khalid na Mussa wakiwa na jambo la kutojulikana sana na wajumbe wa Tanzania Bara kutokana na kufanya kazi zao Zanzibar kwa muda mrefu.

Hata hivyo, hiyo inategemea pia 'Dodoma' itakuwa na taarifa zipi za ziada dhidi ya wagombea hao watano.
Pasi na shaka yoyote; nikimnukuu Pius Msekwa, taarifa ya muhimu zaidi ikiwa; Ni nani atakipa ushindi chama hicho kwenye mchuano dhidi ya Seif Shariff Hamad.

BBC Swahili

_113265300_magufulindctshein.jpg
 
Kwa hulka na silka za waislamu na watu wa znz. Mwinyi Hana kujulikana Sana na kukubalika Sana visiwani huko.

Wa Zanzibar wanathamini zaidi mtu waliyekuwa nae katika shida na Raha na kwa hapo Mwinyi Hana ushawishi wote miongoni mwa isles voters weka Hilo sahihi.
 
Sidhani kama kura za wananchi ndizo huamua nani awe Rais wa Zanzibar.
Kwa hulka na silka za waislamu na watu wa znz. Mwinyi Hana kujulikana Sana na kukubalika Sana visiwani huko.

Wa Zanzibar wanathamini zaidi mtu waliyekuwa nae katika shida na Raha na kwa hapo Mwinyi Hana ushawishi wote miongoni mwa isles voters weka Hilo sahihi.
 
Na Kati ya watu Hawa 2 mmoja wao anakwenda kuwa raisi wa visiwani naye ni PHD holder Mzee Mbarawa.

Hapo with the growth of technology and information sharing we should not underestimate the Mighty Maalim Seif Sharif Hamad with his ACT wazalendo party.

Upo uwezekano wahafidhina na wajanja na makundi mwingine kwa kukomoa wakaamua kumpa ushirikiano nzuri Maalim ili achukue nchi hii inaitwa hero tukose wote apate adui yetu.
 
Kumbuka tume ya uchaguzi ipl chini ya ccm zanzibar na maamuzi yanatoka bara dodoma.
Na Kati ya watu Hawa 2 mmoja wao anakwenda kuwa raisi wa visiwani naye ni PHD holder Mzee Mbarawa.

Hapo with the growth of technology and information sharing we should not underestimate the Mighty Maalim Seif Sharif Hamad with his ACT wazalendo party.

Upo uwezekano wahafidhina na wajanja na makundi mwingine kwa kukomoa wakaamua kumpa ushirikiano nzuri Maalim ili achukue nchi hii inaitwa hero tukose wote apate adui yetu.
 
Kama ACT watakuwa makini kulinda kura zao hakuna mgombea wa ccm atakayemshinda maalim Seif!!! CCM hushinda kule visiwani kwa hila; wanapeleka wanajeshi kuwatisha wapiga kura, hata hivyo wizi wa kura nio mbinu yao kubwa.
 
Kwa hulka na silka za waislamu na watu wa znz. Mwinyi Hana kujulikana Sana na kukubalika Sana visiwani huko.

Wa Zanzibar wanathamini zaidi mtu waliyekuwa nae katika shida na Raha na kwa hapo Mwinyi Hana ushawishi wote miongoni mwa isles voters weka Hilo sahihi.
hii pia inamgusa Mbarawa....
 
Zenjibari haitaki Rais mzanzibara tukiwalazimisha sana na huyo Mwinyi wenu mlieshupalia aende akawajambie watamwaga mboga! miaka kumi itakuwa tabu tupu to colonize Zenjibari mimi ni kijani ninaeheshimu muungano nashauri tuwape kina yakhe heshma yao jamani kuwatawala tuwatawale hata Rais tuwape mgeni kwao?

kweli hiyo si haki, hapo tuwaingize hao watatu wakwao na tumtoe Mwinyi na Prof Ngalawa ni wakuja kwao ni wazanzibara na nafasi zao achukue Jecha na mwanamama mmoja ikamilike list ya watu watano!!Mwinyi ni mtoto wa Rais nchi hii haiongozwi kimila na haina hatimiliki ya Urais huyo hafai yatosha baba yake kuwa Rais manake ni mkimya sana kama zezeta flani na hata mkimpitisha kibabe itakuwa sheria sasa baba Rais mtoto Rais (monarchy) na mtoto wa Nyerere , Salmin Amour, Karume, Shein na JK na Magu wote nao watataka nao wapewe haki hiyo!!

Prof Mbarawa ni professa na siku zote huwezi kumuendesha profesaa kama ambavyo muungano unatakiwa uendeshwe na mamlaka za Dodoma huyo akiwa na rungu hatakubali!! professa yoyote huwa ni mjuaji sana huyo Ngalawa atafanya kuiongoza Zenjibari kuwa kazi ngumu mno na huwa binadamu kawaida akipewa cheo na pesa anabadilika anaota mapembe na masikio ghafla tu utaona yamezidi kichwa nani anamkumbuka Magu waziri na Magu Rais??huyo Ngalawa msijeshangaa akavunja muungano hata mkimuua si keshauvunja!! Rais wa Zenjibari lazima awe weak kwa namna yoyote sababu kamba hukatikia pabovu!!

wabara tuwe na akili za kileo hatuwezi kulazimisha mambo ya Nyerere kuwapa Rais wasiemtaka akawajambie na anaepingana na mila zao za kumchagua Rais mzaliwa na mkaazi wa Michenzani, Bububu, Tumbatu, Kiwengwa, Nungwi, Chakechake, Kojani, Jambiani, Mchamba wima, Fuoni, Mfereji wa Wima, Jang’ombe, Mji Mkongwe au Mwanakwerekwe huko Zenjibari, kwanza inapendeza waongozwe na mtu wao wanaeishi nae, wanaekunywa nae gahawa na halua, mwenzao waliezoea kujambiana nae bila kuleteana shida ati!! basi hata tukumbuke katika wagombea watano sisi wabara ndio tunachagua mshindi hiyo yatosha kuwa tumewaonea na kuwatawala basi tusiwaonee kina yakhe kupita mpaka , tuwape mamluki mmoja safi , mtu tunaemmudu, tuwape Rais mzee asie na elimu kubwa, Nahodha au Jecha tu watatulia!!

wajumbe wa NEC mambo yakiharibika Zenji msijesema wapambe wa chama wa pembezoni hatukusema!!
 
Kama ACT watakuwa makini kulinda kura zao hakuna mgombea wa ccm atakayemshinda maalim Seif!!! CCM hushinda kule visiwani kwa hila; wanapeleka wanajeshi kuwatisha wapiga kura, hata hivyo wizi wa kura nio mbinu yao kubwa.

Hakika kaka. CCM znz ni wepesi kama ushuzi unaonuka. bila ya tume ya baradhuli jecha Salum hawawezi kushinda. Jeshi la JWTZ na polizi, TISS na vikosi vyengine vya ulinzi huhamia znz kwani wanajua kule mtoto hatumwi chumvi dukani. Ukweli ni kwamba tokea 1995 mpka uchagzui wa 2015 CCM haijawahi kushinda kihalali kama si kutumia hila, nguvu ya dola na mazombie.

Wache waje na mbwembwe lakn ACT inawakaribisha. CCM watalia mapema
 
hii pia inamgusa Mbarawa....
Mbarawa anaonekana ni wa kuja zaidi. Hana hulka za kizanzibari na anayoonekana hafai kuishi ktk jamii ya znz. ukifuatilia tabai zake za ndani ( tunafunika k kombe) na wazenj wanazijua vyema ).

Nafikiri CCM znz wangesimama kidete kudai candidate aliyekulia na kulelewa znz. Mwinyi kazaliwa na kusomea Egypt kwa masomo ya msingi na skondari ya awali ingawa alihamia Tambaza baadae kwa A- level.

Ni mgeni kabisa wa maisha ya znz. ni wakati umefika wa kuwa na rais ambaye ni 'home grown candidate' na anayefahamu maisha ya watu wa znz. siyo kuletewa mtu aiseyejulikana.
 
Mbarawa anaonekana ni wa kuja zaidi. Hana hulka za kizanzibari na anayoonekana hafai kuishi ktk jamii ya znz. ukifuatilia tabai zake za ndani ( tunafunika k kombe) na wazenj wanazijua vyema ). Nafikiri CCM znz wangesimama kidete kudai candidate aliyekulia na kulelewa znz. Mwinyi kazaliwa na kusomea Egypt kwa masomo ya msingi na skondari ya awali ingawa alihamia Tambaza baadae kwa A- level. Ni mgeni kabisa wa maisha ya znz. ni wakati umefika wa kuwa na rais ambaye ni 'home grown candidate' na anayefahamu maisha ya watu wa znz. siyo kuletewa mtu aiseyejulikana.
uko sahihi.
Maalim Seif ndie kiongozi sahihi wa Zanzibar
 
Kuna sentense yako moja eti lowasa alishindwa uchaguzi 2015 , lowassa hakushindwa uchaguzi nakuweka sawa, uchaguzi ulihujukiwa kuna kila ushahidi kuwa upinzani ulishinda muulize magufuli
 
Back
Top Bottom