Ninaweza kumshitaki JK na msafara wake ? Naomba ushauri tafadhali

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Wana JF
Leo nzima nimekuwa na simanzi baada ya kupoteza biashara kisa nimechelewa appointment na wadau wangu .Nilikuwa na wafanya biashara walio kuja hapa nchini kuhusiana na mambo ya kilimo .Mkutano watu ulitakiwa kuanza saa 2 asubuhi .Mimi nimeondoka kwangu saa kumi na mbili na robo asubuhi .Kufika njia Panda ya Segerea kwenda mjini nikakuta foleni iliyo dumu kwa masaa mengi sana .Kuuliza naambiwa Kikwete was expected to land by BA toka UK .

Hakika tumeachiwa saa mbili tangia kumi na mbili na nusu .Watu wengi wamelalama mno.Kwenye foleni kulikuwa na wagonjwa , mahabuhusu nk .Wote hao walikaa kimya na kubanana kisa JK na msafara wake .I am now contempleting on what steps should I take .Kitendo hiki ni kibaya mno na kinazuia ufanisi na kupunguza kasi ya maendeleo .I lost much enough today na naombeni seriously ushauri wa kisheria nikafungue kesi kuomba mahakamba kuzuia kusimamishwa kwa magari wakati JK akiwa angani .He could also drive with us kwenye foleni .

Hawezi kuwa na nguvu kuliko sisi walipa kodi .JK na CCM namjua leo maisha mangapi ya watanzania yamepotea au nyie mnawatafuta madaktari na Chadema pekee na haya ya kufia kwenye foleni na kuchangia hasara katika maisha yetu hamuyaoni ?
 
Hebu kazana mkuu utakuwa umenisaidia na mimi nachukia misafara sana.
Haina tija
 
pole kaka, onana na mwanasheria wako akushauri jinsi ya kufanya, ila kumshtaki 'dhaifu' binafsi huwezi kwa katiba ya sasa. sanasana mwanasheria akiona kuna hoja uishitaki serikali kwa ujumla. inaboa kwelikweli na misafari ya kila siku
 
Kwa kitendo cha leo hakika I have lost much na Serikali haijui adha hii na watanzania hawasemi wanakaa kimya .Nimepoteza deal kubwa leo na partners wameondoka bila makubaliano maana I was late na wao walisha check out tayari kwa safari huko Kenya .Naomba ushauri wenu wa kina nimeamua kufungua kesi kuomba fidia na kupiga maruku misafara isiyo kuwa na tija kwa maisha ya mtanzania .
 
Watawala wetu ni wapenda sifa na wachoyo wa kupita kiasi. Unapofunga barabara zinazolipiwa na walipa kodi unaangusha uchumi. Kwa nchi zilizoendelea hapa ungeishitaki serikali na kulipwa unono. Ila kwa nchi yetu ambayo sheria zake ziko mifukoni mwa watawala na wenye nazo utapoteza muda wako. Dawa ya kuondoa hili ni kuchangia kwenye mchakato wa katiba kuondoa kipengee kamahiki kinachomfanya rais kuwa mungu mtu.
 
hey, endapo utahisi kuonewa na JK unaruhusiwa kufungua kesi kuishitaki serikali ambapo baada ya kuprove in the court kwamba ulipata loss 4 sure mdogo wangu watakucompasate ukisema umsamehe na kusubiri rais mwingine baada ya miaka miwili huwez jua pengine itakua bora huyu.
 
Bado viongozi wetu wanajiona miungu watu kwa kupotezea watu mda wao.Kuna tatizo sana katika nchi zetu za dunia ya tatu katika kujali mda.Nchi za wenzetu ukichelewa dk5 kwenye appointment ukimkuta mhusika ni bahati na itabidi uombe samahani.Pole sana mkuu kwa yaliyokusibu.Ngoja wenye ujuzi wa sheria wakupe muongozo
 
Nachukia sana hyo misafara ila ukishafungua kesi tu ujue maisha yako yapo hatarini mda wowote lazima waku-ulimboke!
 
Hata Dr Slaa akifanikiwa kuingia ikulu,prototal au itifaki kliswahili inapaswa kufuatwa.Kumbuka huu si utashi wa rais aliyeko madarakani, bali ni itifaki inayotumiwa dunia kute. Inauma lakini ndio ukweli.Nakumbuka wakati George.W.Bush alipotembelea Tanzania kwa mara ya kwanza ndege yake ilipotoka nchi ya Benin barabara ambazo msafari wa Bush zilifungwa kwa zaqidi ya masaa matano.Ndugu yangu hilo mbona ukuliona?
 
Nafikili jaribu. Sina precedent yoyote ya namna hii.Lakini inaleta sense kwa sababu kikawaida nafikili watu wanatakiwa kuambiwa kwamba njia fulani kutakuwa na msafara siku fulani muda fulani ili waweze kujipanga na kujua kwamba incase nina mgonjwa nifanyaje?.Hii ya kukulupuka tu asubuhi na kuwasimamisha watu kwa massaa kibao bila advance notice nafikili inweza kuwa litigated mahakamani kwa kumshtAki AG.JARIBU MAMBO MENGI YANAANZA KWENYE KUJARIBU.
 
Ukubwa wa msafara na muda wa kusubiri unaongezeka kwa kidili siku zinavyokwenda. Hii inaonesha kuwa hata rais mwenyewe hajifeel safe katika nchi hii ndoo maana siku hizi msafara ni mkubwa na unamwendo kasi sana na muda wa kusubiri ili apite unaongezeka. leo umekaa roughly two hours. Next time utakaa masaa 4. Nakumbuka kuna kipindi nilitoka mbeya kipindi cha msiba wa mama yake na speaker. Rais akiwa Iringa sisi tukaambiwa tupaki pembeni magari tukiwa Mafinga. Nani atatuhakikishia usalama na kutuokolea muda katika nchi yetu?
 
Kisiasa waweza kumshtaki, lakin kisheria hauwezi.
Kuna maxim moja inaitwa 'damnum sine injuria' maana yake kuwa ukipata loss bila violation of a legal right no action in court.
But ili niwahakikishie kuwa hili jambo lipo kisheria,angalia kifungu cha 43 cha The Road Traffic Act, ambapo imetajwa kuwa ni kosa ku-obstruct official motorcade.

Kwa kuwa ya tume ya katiba ipo mtaani,mi nafikiri tutumie hiyo fursa kuangalia hili suala liweje.
 
Kufungua tu kesi mahakamani siyo issue lakini kamwe huwezi kupata haki yako kwa sababu kufunga barabara wakati wa msafara wa rais ni taratibu inayotambulika kisheria,halafu ujue ya kwamba rais ana kinga ya kutoshtakiwa ndg yangu,ila pole sana
 
Hawa jamaa walau wangekua na busara kidogo hata ya kurekebisha muda wa msafara.kwa mfano:wanajua kabisa ofisi zinafunguliwa kuanzia saa moja mpaka saa tatu,kuanzia saa nne foleni inapungua,hivyo wangeweka muda huo,halafu..kuanzia saa kumi jioni pia kusiwe na msafara mpaka kuanzia saa tatu au nne usiku.Kiukweli kabisa kama umekaa dar,Misafara hii ina aathari kubwa sana kiuchumi hasa kwa wajasilia mali wanaotegemea kuchukua mizigo asubuhi na hasa kwa watu wa ki[pato cha chini,kama wanaokwenda feli na k'koo.nafikiri intelligensia italiangalia hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom