Ninatafuta mpenzi/mume nipo serious

Ahsante. Mimi siyo jiko.
baada ya unyumba, haki kubwa ya Mwanamme wa Kiafrika ni kupikiwa. Wewe unasema misosi tukapikiwe na mama zetu, we sio jiko... ni lazima ujuwe una interact na watu wa jamii gani.
 
yeah ni huyo niliona siku moja anatafuta mke,mpe nafasi you never know what the future holds
Hapana mkuu kwa yule a big NO. Wangu wa hulka yangu ya maisha yupo au niseme karibia nitampata!!!:p:p:p
 
baada ya unyumba, haki kubwa ya Mwanamme wa Kiafrika ni kupikiwa. Wewe unasema misosi tukapikiwe na mama zetu, we sio jiko... ni lazima ujuwe una interact na watu wa jamii gani.
Sawa nimekupata Tindikali. Ila kuwe na flexibility kwa sabatu tulioajiajiri au ajiriwa ni tofauti sana na mama wa nyumbani. Tunategemea sana wasaidizi wa majumbani na pengine tukiwa na nafasi kama hatujasafiri ndipo angalau weekend unakarangiza. Au unataka nikitoka mihangaiko na foleni za Dalisalama ninafika nyumbani saa nne usiku ndiyo ninaingia Jikoni?
 
Flexibility?

Jamaa mmoja ambae alitoka na mkewe mbali kwenye ufukara mpaka akawa tajiri mkubwa kuliko wote Tanzania, alimuacha mkewe na akatoa sababu za kwa nini ameamua kuwa na kimwana kipya. Alisema huyu mwanamke mbadala anampikia chakula kwa mikomo yake mwenyewe, anafua nguo zake bila kuogopa kuharibu makucha yake marembo, anampigia pasi kwa mikono yake mwenyewe. Na hii ni japo wanaweza kuwa na wafanyakazi na ma mashine ya kila aina duniani. Sasa kwa nini wewe ushindwe kunipikia siku zote?
 
SUBIRI WATAKUJA TU .. ..
KWA UPANDE WANGU VIGEZO ULIVYOVITOA SIPO KABISA..
UMRI .. SIPO
KUFIWA .. SIPO
KUTALIKIANA NA MY SWEETY - SIPO.

NIKUTAKIE KILA LA KHERI KWENYE UTAFUTAJI WAKO...
Asante sana.
 
Flexibility?

Jamaa mmoja ambae alitoka na mkewe mbali kwenye ufukara mpaka akawa tajiri mkubwa kuliko wote Tanzania, alimuacha mkewe na akatoa sababu za kwa nini ameamua kuwa na kimwana kipya. Alisema huyu mwanamke mbadala anampikia chakula kwa mikomo yake mwenyewe, anafua nguo zake bila kuogopa kuharibu makucha yake marembo, anampigia pasi kwa mikono yake mwenyewe. Na hii ni japo wanaweza kuwa na wafanyakazi na ma mashine ya kila aina duniani. Sasa kwa nini wewe ushindwe kunipikia siku zote?
Asante. Huyo jamaa ninamfahamu na huyo mke mpya pia. Mke mpya ana shughuli zake za kujiajiri kwa hiyo ni rahisi kujipanga. Mimi nimeajiriwa. Sasa unataka nifanyeje hapo? Asubuni ninaamka niwahi foleni saa 11, then kurudi home nifike saa tatu au nne. Hata kwa afya kupika chakula muda huu ule saa tano ni kutaka kufupisha maisha yako tu. Cha msingi unatakiwa kuelewana tu. Pale muda unpopatikana basi unapikiwa usiwe na shaka. Au wewe unamchukulia mkeo kama punda? Aamke saa 10 kukuandalia breakfast, arudi saa nne au tatu usiku alalale saa 5 a 6 usiku then anaamka tena saa 10. Be a human being. Kama una upendo na mkeo ni lazima utatafakari afya yake pia kama ambavyo yeye atakuwa anakujali. Ndoa si mateso wala karaha, ni furaha kwa wote. Kama havipo hivi mtaishi kwa shida sana, yaani ndoa ya mateso bila furaha. Ni ya nini hiyo?
 
Kila la kheri.

Ila ningeshauri msipime HIV tu, pimeni na sukari, pressure, prostrate etc. Maana utu uzima unakuja na mbwembwe nyingi
 
Kila la kheri.

Ila ningeshauri msipime HIV tu, pimeni na sukari, pressure, prostrate etc. Maana utu uzima unakuja na mbwembwe nyingi
Asante sana kwa kuongezea hayo magonjwa ambayo yamekuwa ni threat sana kwa binadamu wengi miaka ya karibuni. Nikimpata nitamshauri. Hayo mengine ni mepesi tena atakubali kwa haraka sana. Sheeed kubwa ni hapo kwenye herufi tatu "HIV". Ambapo hii ni moja ya kigezo kikuu. Na nikiona mtu anaanza kuduwaa nikifikia stage ya kupima afya ninapiga chini na kutimua vumbi.
 
kuna jamaa yetu ni mtu wa watu ana kila sifa unayoitaka except anapenda sana clubbing nadhani imesababishwa na yeye kukaa mamtoni muda mrefu,amekaa miaka 30,kama uko interested nikutumie ID yake umuendee PM
Hahahaa mkuu nimecheka sana bila shaka namfahamu muhusika wako
 
Hapo kuna kuzaa kweli,maana kitalaam kuanzia umri 45 kuna uwezekano mdogo sana kwa mwanamke kushika mimba,au akajifungua zezeta.ni wanasayansi ndo wanathibitisha hivyo. Samahani lakini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom