Ninaomba shida ya maji Dar iongezeke mara dufu zaidi

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,686
Dar ni Tanzania, Tanzania ni Dar. Hutaki hili basi utakuwa una matatizo makubwa ya kijinsia!!!

Ukitaka kuona watu wa makabila yote Tanzania hapa basi fika Dar,

Ukitaka kuona watu wa dini zote (unazozijua na usizozijua) basi nenda Dar,

Ukitaka kuona ofisi zote kuu za vyama vya siasa basi nenda Dar (tafadhali usitume picha ya ofisi kuu ya chama chochote hapa),

Ukitaka elimu iliyotukuka basi kimbilia Dar,

Ukitaka kujanjaruka kidogo na kujua kuongea basi kimbilia Dar. Polepole alifanya hivyo 1999 na leo sote tunamjua. Binafsi, watoto wangu nawaandalia makazi huko huku mimi nikihangaika huku mkoani......wakulie hukohuko.
n.k.

Kwenye mada!
Sababu ni hizi hapa;

1. Nao wafeel ile adha ya miaka na miaka ya ukosefu wa maji wanayokumbana nayo wazazi wao huko vijijini.

2. Labda wataamka ili kutuongoza katika kuzisema hizi shida, hii na nyingine, kwa wahusika maana kwa sasa hali ni mbaya mno. Ukiacha maji, mawasiliano sasa yamekuwa tatizo; 1GB imeshafika 3,000/= madakika yanamalizwa kiajabuajabu tu na wenye makampuni, umejiunga cha wiki leo hujaongea na mtu kesho unaambiwa kimekwisha. Siku si nyingi watu tutashindwa kuingia hata jf kufurahi maisha yatakuaje?

Kuandika kazi sana, kunahitajika vipaji vya kina mkuu Mshana, hivyo naishia hapa hapa!
 
Back
Top Bottom