Nina wasiwasi na mke wangu...

Mkeo yupo vizuri sana mkuu....

Mwanaume hutakiwi kuwa na mwanamke mmoja ....utakuja kufa na presha.. ukimiliki mwanamke we weka kichwani mwako kuwa hiyo papychi yake hupigi pekeako...

Utaishi kwa amani sana... Mwisho usipende kudadisi dadisi sana
 
Habar wana JF,
Naimani mko wazima.

Kiukweli nimekuwa na wasiwasi na safari ya wife, sijui kwanini lakini ni safari ambayo siielewi kabsa wakuu. Nina mashaka nayo coz naona mapicha picha tu.

Ni kwamba wife kasafiri juzi ijumaa kuelekea Singida lakini safari yake sielewi elewi kabisa, kwasabubu kwanza ni safari ya kushtukiza lakini pia mpaka now sielewi aim ya safari ni nini mpaka now.

Alhamisi amerudi kutoka kazini usiku tunalala ndiyo ananipa taarifa ya kuwa kesho Ijumaa anasafiri, nikamuuliza unaenda wap? Akaniambia kapigiwa simu na dada zake wamemuita ambao wanakaa Singida. Nikamuuliza kunatatizo akasema hapana, ila sijui wanashida gani na mimi ndiyo wamenipigia simu niende.

Kiukweli nilikuwa nimechoka nahitaji kupumzika, sikutaka ku complicate kitu, nikamjibu sawa nikalala. Then asubuhi nikajiandaa nikaenda kazini vizur. Niko job ananipigia simu kuwa ndiyo anatoka home anaelekea stendi kupanda bus. Iikuwa almost kama saa 7 hivi mchana nikamjibu haya na nikamuuliza kama kunakitu chochote anahtaji akasema hapana yuko powa.

Basi nikakata simu lakini kiukweli ghafla akili yangu ilishikwa na wasiwasi juu ya safari yake but sikutaka ku doubt anything nikapotezea. Baadaya kupita kama lisaa akanitumia message kuwa amepata basi but akifika Dodoma atashuka kuna ndugu yake anamchuka then wanaenda wote.

Daah, sikutaka pia ku doubt wala mambo mengi nikamjibu sawa, nikaachana naye nikaendelea na kazi zangu, but bado sikuona sababu ya yeye kushuka Dodoma. By saa 2 ndiyo ananiambia ndiyo wanaondoka Dodoma nikamjibu sawa safari njema tukaacha hivyo. Basi mi nikarud home usiku kwakuwa nilishapita somewhere nikapata chakula nikafika home niko good, nikaoga nikaingia kwa bed nikampigia ananiambia kashafika ila kachoka na safari nikamuacha nikapumzika.

Sasa leo Jpili tumeongea asubuh vizur tu na tukaagana baadae by saa 7 mchana ananiambia ndiyo anataka kurudi leo. Nikamuuliza mbona hukuniambia asubuhi na kwanini usingeondoka asubuhi? Sijaona cha maana anachonijibu, basi nikamwambia haya kama unarudi leo. Tuakaacha baada ya kama nusu saa ananipigia simu ananiambia kuwa yupo stendi, mara gari sijui hakuna, mara zimejaa, mara nimechoka nasikia usingizi, nikamwambia sasa siungebaki ili uondoke kesho asubuhi akasema sawa tukaacha.

Baadae ananitumia message eti amepata gari ila linaishia Dodoma kwaiyo atashuka Dodoma. Aloo nikasema kimoyomoyo hapo Dodoma hapo siyo bure, coz kwenda kashuka Dodoma kurudi baada arud kesho kama kweli kakosa usafiri na tumekubalina anarudi kesho mapema na sidhani kama kweli alikosa usafiri by that time ananiambia kuwa kapata usafiri.

Ila unaishia Dodoma so ataenda kulala Dom, sikutaka ku complicate nikamjibu sawa basi nikaachana nae. Ila cha ajabu baada ya hapo akawa kimya hakusema kama kafika au laa. Yaani ndo ananitumia text saa hii, saa 5 usiku kuwa alifika salama ila alishindwa kuniambia coz vidonda vya tumbo vilimshika akafikia kupumzika. Heheheh nacheka ila najua mwenyewe wakuu but sijamjibu na sitamjibu lakini namsubiri arudi kesho nikitoka kazini anieleze vizuri kuhusu hii safar yake.

Japokuwa mimi siyo mtu wa kumchunguza mwanamke na sipendi kabisa kuchunguza mtu sababu naelewa what’s gonna happen.

Wakuu kama kuna la kuniongezea karibuni sana, uwanja ni wenu.
Kijana huna mke, hapo alienda Dom Kwa Jamaa yake na usikute wako ofisi Moja, kuwa makini tu ila nakushauri kama una roho ndogo acha kumfuatilia usije ukaumia
 
Umeonyesha mapungufu mkuu! Unapewa taarifa usiku kuwa kesho nitasafiri? Pasipo sababu za Msingi nawe unaridhia? Tufanye limeshatokea.
Ushauri akifika dai risiti;Dar to Dodoma, Dodoma to singida, Singida to Dodoma &Dodoma to Dar esalam. Then unganisha doti. Litakafuatia ajibu maswali baada ya tiketi kuepo au kukosekana.
Siku nyingine usitoe ruhusisa ya masaa kadhaa kuwa kesho nitafanya ivi ama vile.
 
Ule muda aliokuwa anasema yuko Singida ulitakiwa kuwapigia nduguze hao waliomwita halafu kuwauliza vipi mgeni kafika salama ? Ingekuwa ni kweli wangesema ndio kafika salama halafu unawaomba wampatie simu huyo mgeni uongee naye manake unajifanya kila ukimpigia humpati.. Ukiona taarifa ni za kweli , unajifanya nimepatwa na wasiwasi sana labda kuna jambo baya limetokea nyumbani mpaka hapo utakuwa umeshapata 80% ya movie.
ila ukisikia tu mgeni gani ? Ujue ndo hivyo tena !
Kumbe hata wewe ungepigwa tukio mkuu yaani wakati anamwambia yupo singida itakuwa kweli yupo singida maana tayari mzigo umeshapigiwa dodoma na yeye anajulishwa kuwa ndo amepata Gari kutoka dodoma kwenda singida hivyo basi kidume kilikuwa Dodoma
 
Simu kapigiwa anaambiwa aende kuna ishu ila asiambiwe ni ishu gani hadi afike!!!! are you serious guys? inamaana hao wanaompigia simu hawajui kwamba huyo ni mke wa mtu na ili atoke lazima sababu ya msingi iwe wazi ndipo mwanaume utoe ruhusa anyway lakini labda hawana taarifa zako, ila kiukweli mwanangu umefeli kuruhusu mkeo aondoke kiholela, Wanalika kimasihara sana ila kama na wewe unakula wawatu pia basi sio kesi.
 
Back
Top Bottom