Nina mpenzi anataka kunioa lakini mimi simpendi, Nifanyaje?

Wenzako hutafuta hata wa kumvisha Pete tuu, hata akikimbia don't care, faraja IPO we unalimbia ndoaa

Hivi bado hujajua tu nyie mpo Billion 3 na wanaume wako billion 1.5 , subiri uje uolewe na nyuki akuletee maua
Nyongeza:

Katika hao billion 1.5 kuna;
-mashoga,
-mahanith,
-maplayboy,
-wagonjwa,
-etc...
Waoaji ni 1/3
 
Kwani nani alikuambia mwanamke anapenda,vitabu vya dini vinataka umtii mume wako,na mwanaume ampende mke wake.
Kazi yako ww ni kuwa mtii sio kupenda.acha kuingilia kazi za watu jukumu hilo la kupenda amepewa nwanaume na si mwanamke
 
Pole kwa tatizo hilo.

Lakini nafikiri tafsiri halisi ya neno 'mpenzi' ni mtu unayempenda. Bila shaka, kwako huyo si mpenzi, ila ni mtu mwenye mapenzi na wewe. 'Si dhambi kushindwa kumpenda mtu. Lakini ni makosa kuwa na mtu usiyempenda.' Hivyo basi, rekebisha hilo kosa, na umwambie ukweli, lakini umpe uhuru wa kuwa na mtu atakayekuwa sahihi kwake.

Jambo hili ni muhimu sana kwa sababu:


Kwanza, utakuwa umeokoa dhamira yako na hali ya kujilaumu, endapo ataendelea kuteseka kwa ajili yako.

Pili
, utakuwa umejipa nafasi wewe ya kukutana na mtu sahihi kwako, 'wakati' ukifika.

Naomba niongeze neno hapo:
Kwa kawaida, ukikutana na mtu ambaye ni sahihi kwako, unavyojisikia, ndivyo atakavyojisikia. Mioyo yenu itaongea lugha moja. Akiumia utahisi maumivu yake. Akifurahi utahisi furaha yake. Lako litakuwa lake, na lake litakuwa lako. Mapenzi ni safari, lakini si safari ya mtu mmoja. Ni lazima msafiri pamoja, mfike pamoja. Kwa hiyo lazima mioyo yenu iambatane ili muwe kitu kimoja.

Cha kufanya: Kwa sababu ni mtu anayekupenda, zungumza naye, kwa upole na hekima kubwa. Kuumia ni lazima ataumia, lakini itamsaidia kuujua ukweli ili ajipange namna ya kuishi bila wewe. Halafu, baada ya hapo, omba Mungu akusamehe kwa kutomwambia ukweli mapema, ili maumivu yake yasikutese pale ambapo utahitaji kupata mtu mwenye mapenzi ya kweli. Halafu mwisho, jipe muda. Usiangalie umri wako. Katika ndoa hakuna kuchelewa. Kila mtu ana haki ya kufurahi, amini na wewe unayo haki ya kufurahi pia.

Ninaamini kwa mchango huu na michango ya wengine,utapata kitu cha kukusaidia.
 
Dah.. unajua kuna ule usemi hakuna mtu anajua mwanamke anahitaji nini? Naona kama ni kweli.
 
We MSICHANA fikiria Mara 2 kabla hujamkataa mwanaume.
Idadi ya watu duniani =7.8 billion
Wanawake = 5.6 billion
Wanaumme =2.2 billion

Kati ya wanaumme 2.2 billion
1 billion= wameshaoa tayari
Million 200 =wapo jela na wengine machizi
Wanabaki billion 1

Kati ya hao billion 1
Million 500 = hawana kazi
Wanabaki million 500
Kati y hao
5% = mahanisi (gays)
3% = walokole
10% = jamaa zako
Waliobaki wana umri zaidi ya miaka 66

Sasa we endelea kukataa wanaumme utajioa mwenyewe.
 
Bado napata mkanganyiko ulikuwa nae vipi mpaka sasa ni wachumba ilhali wewe humpendi hebu Kuwa sawa ulimpendea nini?
 
Umeshatumia vingapi vyakwake?
Twambie ndio uje nahoja ya kuachana maana nyie sio watu wazuri sana, kipesa mpo mbele km tai.
 
Back
Top Bottom