Nimueleweje? msaada tafadhali

The Don

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,499
1,163
Mimi nina girlfriend ambaye nimedumu nae katika mahusiano kwa miaka kama minne na sasa yupo masomoni,kiukweli nampenda sana ila sijui upande wake japo anajitahidi kwa kiasi chake kuonyesha mapenzi ya dhati,tumepitia mengi yani shida na raha na mitafaruku ya hapa na pale,yani nilimjali kwa kila kitu mf. Pesa,msaada wa kimawazo nk,kutokana na kwamba bahati mbaya wazazi wake walikwishaaga dunia mda mrefu kidogo na kuwaacha ktk hali ngumu ya maisha kidogo,nilikuwa nachat nae km kawaida na alinambia anakuja tarehe moja mwezi huu wa sita,ila jana nimewasiliana na rafiki zake wawili kuwajulia hali walichonijibu sikuamini,wapo likizo yani wamerudi nyumbani jana wakiwa wote ila mpaka sasa hapatikani na hajanitafuta,naona jini kisirani kaingia kwa kasi sana kwani mimi kila nikisafiri nikirudi lazima nimtaarifu,je ananipima au ndo naibiwa? Msaada tafadhali kwani nashindwa kufanya chochote nifanyeje
 
Usifanye chochote, leo atakutafuta na mtaongea!
Na uliwapigia rafiki zake ili iweje?
 
Usifanye chochote, leo atakutafuta na mtaongea!
Na uliwapigia rafiki zake ili iweje?

Kaunga...Checks and Balances are very important.......Wengine mwatupanga foleni ati....ni vyema kubalance story....Laswy jipe muda...pengine simu imeishiwa chaji na sasa "inachajiwa" ....poengine imeibiwa.....au pengine unaloliwaza pia....Time will tell...
 
Kaunga...Checks and Balances are very important.......Wengine mwatupanga foleni ati....ni vyema kubalance story....Laswy jipe muda...pengine simu imeishiwa chaji na sasa "inachajiwa" ....poengine imeibiwa.....au pengine unaloliwaza pia....Time will tell...

Hizo checking zina madhara makubwa kuliko faida!
Asubiri aongee naye, atajua tu kama anachitiwa; kuspeculate kuna shida sana!
 
Ni mapema sana kusema lolote, kwa mda wote uliokuwa nae unatosha kuwa na kipimo hasi au chanya. So subiri utajua lililomsibu.
 
kama kweli huyo dada anakupenda.mimi niwe na mpenzi wangu ambae yuko mbali,nikishafika tu.basi nitamtafuta.marafiki zake wajue yupo,wewe usijue.mmh,maybe hana mapenzi kwako ya kiivyo tena.au mapenzi hayachukulii uzito ya kiivyo.anyway ni vizuri usubiri yeye mwenyewe akutafute.kama kuna mabadiliko,utajua tu
 
Hahahaha!! Kumbe wanaume wenye wivu bado mpo? Kama kutowasiliana nae kwa siku moja tu ushaingiwa na wasiwasi kuwa unaibiwa ina maana humwamini huyo mpz wako...remember that love is trust!!
 
Hivi kwa nini kwenye issue za mahusiano ya kimapenzi...ukiona warning signs ukaomba ushauri watu wanajifanya kukupa moyo kuwa hamna tatizo, sijui usiwe na wasi wasi, ooh sijui subiri kwanza!

Lets be realistic.....mwanamke kamdanganya mpenzi wake kuwa anarudi toka shule siku fulani, wakati kumbe amerudi siku nyingine, iwe kabla au baada ya siku aliyosema...fact ni kwamba kadanganya, na ana sababu ya kudanganya, ambayo hataki kukuambia. sa hata ukija muuliza mkikutana, juu ya nini akuambie ukweli wakati alishadanganya tayari!? Hata akikuambia ukweli sasa, kwa nini alidanganya in the first place!?

Dalili ya mvua ni mawingu...ana hulka ya uwongo huyo kwa motive anayoijua mwenyewe (NB: si lazima kuwa ukiongopa basi unacheat).
 
kama wamefika jana, kwa nini usitulie? subiri akupigie labda alichoka kwa safari? au simu iliisha chaji?
 
acha mapepe
jana tu unalalamika je angekaa mwezi bila kukutafuta?
yawezekana atakutafuta leo au inawezekana kwake umeshaxpire pia
sio lazima kungangania utaumia bure just wait
if you love someone let her free, if she comes back she is yours
if she doesnt, she never was
 
acha mapepe
jana tu unalalamika je angekaa mwezi bila kukutafuta?
yawezekana atakutafuta leo au inawezekana kwake umeshaxpire pia
sio lazima kungangania utaumia bure just wait
if you love someone let her free, if she comes back she is yours
if she doesnt, she never was
 
Mimi nina girlfriend ambaye nimedumu nae katika mahussana ila sijui upande wake japo anajitahidi kwa kiasi chake kuonyesha mapenzi ya dhati,tumepitia mengi yani shida na raha na mitafaruku ya hapa na pale,yani nilimjali kwa kila kitu mf. Pesa,msaada wa kimawazo nk,kutokana na kwamba bahati mbaya wazazi wake walikwishaaga dunia mda mrefu kidogo na kuwaacha ktk hali ngumu ya maisha kidogo,nilikuwa nachat nae km kawaida na alinambia anakuja tarehe moja mwezi huu wa sita,ila jana nimewasiliana na rafiki zake wawili kuwajulia hali walichonijibu sikuamini,wapo likizo yani wamerudi nyumbani jana wakiwa wote ila mpaka sasa hapatikani na hajanitafuta,naona jini kisirani kaingia kwa kasi sana kwani mimi kila nikisafiri nikirudi lazima nimtaarifu,je ananipima au ndo naibiwa? Msaada tafadhali kwani nashindwa kufanya chochote nifanyeje

kuwa mvumilivu kaka coz haturuhusiwi kuhumu, kama wako wako tu kama anajitambua
 
Cha msingi na sekondari, endelea kuwauliza hao mashosti zake ili ufahamu yuko wapi, labda ana aunt bt hakukutel mzeiya! I know inauma sana kaka! Pole saaana!
 
Back
Top Bottom