ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Nimrejeshee nini mamsapu!
Wakati ule tulipoanza mahusiano, yeye aliniambia amewahi kuwa na mahusiano na mtu mmoja tu ambae hata hivyo hakudumu nae muda mrefu. Nilipomtizama usoni, alionyesha wazi kabisa ni mwenye kauli ya uaminifu..kama kawaida ya wanaume nikamkazia macho na kumuuliza tena lakini akaisimama kwenye kauli yake moja tu " I swear, nakuambia na sina sababu za kudanngaya".!!..wakati huo mimi nilikwisha kuwa na mahusiano yaliyiosambaratika na zaidi ya wanawake sita (wote wakitegemea tutakuwa pamoja milele daima!! lakini wapi!). Sikumweleza undani mpaka miezi kadhaa ikakatika....wakati huo mmoja ya wanawake niliyokuwa nahusiana nae kabla tayrai alikuwa na ujauzito..dhamira ilinisuta, nikamweleza ma-msapu kuwa kabla hatujaendelea na uhusiano mimi nina mwanamke ana ujauzito lakini sidhani kama anatanifaa kuliko yeye..akalia sana baadae akasema" basi bwana mimi sitaweza, wewe endelea..." nilimsihi sana kuwa mimi sina tena uhusianao na yule mwanamke niliyempa mimba.
Baada ya siku mbili akaniambia hana jinsi, tuendelee..wakati tukikaribia kufunga ndoa, yule mwanamke niliyempa ujauzito akajifungua baby boy, awali ilikuwa vurugu kwa upande wa kwao wakitaka niwe napeleka matunzo ya mtoto, simu na sms zilikuwa haziishi kama sijapeleka matunzo. Mamsapu akanishauri nimchukue mtoto tuishi nae, nilisita nikijua labda ahatamlea vizuri kwa kuwa si wake..mtoto akiwa na miaka miwili na nusu tu nikamchukua...wakati huo pia mamsapu akanishauri nimchukue na mdogo tuishi nae ..nalo nilisita lakini yeye akalazimisha, siku moja niliporejea safari nikamkuta dogo katinga nyumbani na nyumba imekuwa na furaha ya ajabu sana ...Hakika sasa ni mwaka wa nane anaishi na mtoto wa mwanamke mwenzie na wa kwake kama wote kawa zaa mwenyewe , huwezi kujua kama kuna tofauti ya mama ..anamlea vizuri sana kiasi cha kwamba nami naona myo wake ni wa ajabu sana!.
Mama ya mtoto aliolewa lakini wakati alibahatisha kuja nyumbani akataka kuleta fujo akimtaka mwanae..mamsapu alighazabika sana kiasi cha kutaka kumrusha makonde kwa matamshi aliyomtolea...Hakika sijui nimrudishie nini mamsapu kwa ukarimu anaonitendea!!!.Najua ni wanawake wachache sana wanaweza kuwa na roho ya kutojali na kubeba jukumu linalotokana na dhambi za wengine huko nyuma ikiwemo kuishi na watoto wasio wao.
Yeye si mtu wa kabila la kwetu, wakati ule naingia nae katika pingu za maisha baadhi ya ndugu akiwemo mwanamke mwenzie (mama yangu mzazi) waliniambia pengine niwe makini anaweza asikubali kuishi na mtoto asie wake, asiwe mkarimu kwao na mimi pia nk..lakini sasa najua kumbe mkeo ni zaidi ya mtu mwingine yeyote, yeye ndie anaweza kukuhudumia hata ukiwa unashindwa kitandani, ndie anayeweza kuvumilia mapungufu yako, akakubali kuzoa matapishi yako ukiwa na afya au mgonjwa, akaivumilia harufu mbaya ya pumzi zako za ulevi, sigara, jasho, soksi au ubovu wa meno