Mamushka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2010
- 1,595
- 99
Habari za weekend people, nimekosa la kufanya nikaona niulize kwenu wadau Mimi naishi na wadogo zangu wawili wakike na wakiume wakiume anafanya kazi, wakike yuko chuo ila anafungua mwezi huu ataondoka. Sasa tuna house maid wetu ambaye mimi ndo nilimleta kutoka mwanza vijijini, tumekaa nae muda mrefu sana tu, na kwa vile kati etu hakuna anaeshinda home yani mimi na my brother kazini tunarudi jioni, na mdogo wetu pia alikua ana fanya field sehemu kwahiyo kurudi kwake pia ni jioni. Msichana ghafla kawa na tabia za ajabu sana, anakiburi, heshima ya kinafki, tukirudi ndo anakua busy na kazi muda wote wa mchana na usiku ni busy na African Magic , lakini kwakua kila mtu yuko busy na mambo yake na uchovu wa kazi pia tunampotezeaga tu. tunaishi nae kama ndugu imemfanya ajisahau sana. Jana mi nilijaribu kuongea nae vizuri tu nikamwambia jinsi alivyosahau kilichomleta hapa ni nini, nikamuonya pia kua mwangalifu na vijanavijana kwani hata usiku huwa anachelewa kulala akiwa busy na simu na snema za ki nigeria, kunapesa nilimpatia apeleke sehem flani akalipe maziwa hakufanya hivyo tokea tarehe1 nimemuuliza akadai ntapeleka kesho yani leo nikaingia zangu kulala. Leo alfajiri mdogo wangu wakiume aliskia milango inafungulia then kuangalia akaona binti anatoka na mabegi, akanigongea room kwangu nikamuona ndo anaishia getini, nikatoka nikawasha gari nikamfuata kwa hofu kwamba akipotea ntajibu nini kwao na niyatima huyo binti. Kwakua nilikua na gari na yeye kwa miguu sikufanikiwa kumpata ikanibidi nirudi home, nikaanza kazi za usafi ghafla naingia jikoni namuona anatoka chumbani kwa mdogo wangu wa kiume nakuja jikoni kuendelea na kazi, nilichofanya nilimuomba anipatie zile pesa, aliponipa nikamwambia naomba ukaniletee mizigo yako ulobeba asubuhi nikukague, then uondoke kwa uhuru kwani ndo maisha ulochagua. Nikamuuliza my brother alifuata nini room kwako? Akanijibu mi nilikua nimelala sikujua kama niyeye nimeskia mtu akiingia na kutoka. Kwenye sasaba mdogo wangu wa kike kampigia akapokea kujua ni mdogo wangu akakata cm, sanane mchana kaanza kumpigia mdogo wangu akiwa analia ana muomba aongee na mimi ili ni msamehe arudi anadai nimegundua nimefanya ujinga na nimemkosea sana dada sina pa kwenda, na mjomba wangu kanigombeza sana kwanini unaondoka kwa huyo dada anaekulea kama mdogo wake. Mimi nimeshindwa kuelewa ni wavlana wake wamemshauri then wamemkimbia? Au kunamtu alimdanganya atampa kazi then kamtosa? Mpaka dakika hii ana m beep my ccta amuombee kwangu ni msamehe arudi, dogo kamwambia njoo uongee nae mwenyewe. Anadai anaogopa nikimkamata ntamrudisha kwao na yeye hataki kurudi. Naombeni mnishauri ni fanyeje juu ya hili, ni mrudishe aendelee na kazi? Au akija nimpeleke kwao? Au ni fanyeje, Asanteni.