Kanikubalia lakini yuko busy sana

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Mapenzi ni upuuzi tu ngoja nifocus na maisha, kiukweli nimefunga nimeomba kwa Mungu mke wangu siku akifika nitamuona tu, yaani sitatumia nguvu nyingi kama ninayotumia kwa huyu binti.

Kiukweli binti ni mzuri binti wa Manyovu huko mnanira asili yake ni kama mtusi fulani kutoka rwanda, black beauty yaani mashallah, huyu binti nilikua namuona church tu nikajaribu kutupia nia, nilimwambia nia yangu ni kua mchumba wangu then mke wangu, mwanzoni akachomoa mimi nikafuta namba yake nikafocus na mambo yangu maana huwa sipendi kujipa pressure za kijinga, lakini nikimuangalia mapigo yake ni kama alikua ananitaka, kwasababu hawezi pitisha siku mbili ananicheck, ikabidi nitangaze nia kwa mara nyingine akanikubalia.

Ajabu ni kwamba tokea anikubalie, moyoni mwangu nimedevelop hisia za juu sana kwake, namuwazia sana kuhusu future yetu, lakini dogo ni mpuuzi, namtumia sms asubuhi anajibu jioni, nilimuweka wazi kwamba hiyo tabia sipendi na kama alifanya maamuzi ya kunikubalia bila kutafakari vizuri arudi kuchakata mawazo yake, lakini yeye anasisitiza ananipenda mno, kwa experience yangu watu wakipendana lazima mawasiliano yawepo, najiuliza huyu hata kama nikikomaa nimuoe huko mbeleni atakuja kunisumbua tu?

Nina marafiki wengine wa kike ambao sio wapenzi wangu lakini tunajuliana hali mara nyingi zaidi, lakini huyu sijui anawaza nini kichwani mwake au kwa sababu bado mdogo? Ana miaka 21 sasa hivi.

Nb, hana kazi yoyote ya maana inayomfanya awe busy.
 
Kidume unaamka asubuhi unaanza kutuma message kwa demu??!!! Mara ya mwisho kufanya kitendo hiki nadhani nilifanya nikiwa kidato cha tatu.

Focus mkuu, usiwe idle.
 
Kidume unaamka asubuhi unaanza kutuma message kwa demu??!!! Mara ya mwisho kufanya kitendo hiki nadhani nilifanya nikiwa kidato cha tatu.

Focus mkuu, usiwe idle.
Screenshot_20240315-092842_Messages.jpg

Penzi linapoanza mwanaume ndiye inabidi u-initiate mawasiliano.
 
Mwanzo wa Mahusiano
Mwanamke ukimopata weka siku nne za kumuanza wewe kumtumia sms, mtumie asubui ya umeamkaje na siku njema na usiku ya kuchati kidogo fanya hivyo ndani ya siku nne mfululizo kwa ku-adjust time.

Yaani Day one umemtumia "mambo" saa 2:00, Day two saa 2:30, Day three saa 3:00, Day four saa 4:00....Hizi time una adjust hili kumpa room ya yeye kukumza kukutumia sms muda kama ule unaomtumia.

Kama siku zote nne hizo hata ajajigusa kuanza kukutumia sms, siku ya nne usiku usimtafute, na siku ya tano asubui usimtumie text na siku mtumie "Goodnight" tu, siku ya sita yooote piga kimya ajakutafuta piga kimya mazima amna mwanamke humo.
 
Back
Top Bottom