Tegelezeni
JF-Expert Member
- Dec 31, 2009
- 268
- 124
Mke wangu nimedumu naye kwa miaka minne sasa, katika ndoa yetu tumebahatika kupata mtoto wa kiume mmoja, na baada ya mtoto kutimiza miaka mitatu, tuliamua tupate mtoto mwingine. Tumefanya majaribio kadhaa kwa takriban miezi tisa lakini mke wangu hakushika mimba. Tukaenda kwa wataalamu na baada ya kushauriwa na kupewa tiba, ndipo mimba ikashika, lakini ilianza na matatizo na akahitajiwa akae Bed Rest.
Wakati ujauzito wa mke wangu ulipotimiza miezi miwili, hivi karibuni akapata msiba wa kaka yake aliyemlea. Mimi sikuwepo mjini kwa sababu nilisafiri kikazi mikoani. Alinipigia simu kunipa taarifa za msiba na akanijulisha kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda kijijini kwao kwa mazishi. aliniaga kwamba na yeye atasafiri na mwili wa marehemu kwenda kuzika. Nilimshauri asisafiri kutokana na hali yake, na nilimuhakikishia kwamba nitakaporudi nitafanya utaratibu ili twende tukahani msiba. Alikataa katakata na akanioana mimi ni mbaya kwa sababu nimemkatalia kwenda kumzika kaka yake aliyemlea na kumsomesha. Nikamwambia aende lakini sitahusika na lolote litakalotokea akipata matatizo.
Ni kweli aliamua kwenda lakini akiwa njiani alipata matatizo na ikabidi akimbizwe hospitai ya karibu na ule ujauzito ukatoka. Hakumudu kuendelea na safari na wala hakuhudhuria mazishi ya kaka yake. Nimezipokea taarifa hizi kwa uchungu sana. Sasa najiuliza nikirejea nimfanye nini huyu mwanamke?