Nimfanye nini huyu Mwanamke?

pole naona bado una hasira naye....its okey it will go....its just a phase unayopitia just like anybody ambaye amepata loss anavyopitia....guilty,angry then acceptance.am sure your wife amefanya hivyo out of good will, she thought was strong enough kumzika kaka yake. na yeye ameumia kupoteza mtoto hivyo anakuhitaji kama faraja plz the earlier you accept this loss the better.
 
wanawake hata wao hawajielewi
tena wakikatazwa ndo hutaka kufanya
hasa wanapokuwa na uhakika wa Love and protection.

Wala usimgombeze
ana machungu ya kufiwa na mimba
ni fundisho kwa leo na siku zijazo.
Kweli bwana,mimi mwenyewe sometime huwa navurunda,nabakia kuregreat tu!
 
pole naona bado una hasira naye....its okey it will go....its just a phase unayopitia just like anybody ambaye amepata loss anavyopitia....guilty,angry then acceptance.am sure your wife amefanya hivyo out of good will, she thought was strong enough kumzika kaka yake. na yeye ameumia kupoteza mtoto hivyo anakuhitaji kama faraja plz the earlier you accept this loss the better.

Lakini lazima nimuonyeshe kwamba amenikosea, na hivyo lazima apate adhabu japo kidogo!
 
Naomba nikupe pole sana, lakini cha msingi msamehe maana unajua tena sie wanawake ni viumbe dhaifu sana. Tuko tofauti pia katika kufanya maamuzi.
 
Lakini lazima nimuonyeshe kwamba amenikosea, na hivyo lazima apate adhabu japo kidogo!

usiwe selfish,huyo mtoto si wewe peke yako tu uliyekuwa unamtafuta,na yeye pia.msamehe kama adhabu tayari keshaipata ya kupoteza mtoto.
 
Naomba nikupe pole sana, lakini cha msingi msamehe maana unajua tena sie wanawake ni viumbe dhaifu sana. Tuko tofauti pia katika kufanya maamuzi.

Unajua tulibishana sana kwenye simu na nilitumia muda mwingi kumuelimisha juu ya madhara ya kusafiri wakati alitakiwa awe Bed Rest, lakini yeye kwa kibri akajiamulia mwenyewe kusafiri bila kusikiliza ushauri wangu. huyu ni mwanamke jeuri na hahitaji huruma hata kidogo.
 
Halafu wewe itakusaidia nini?
Kumuonesha kwamba yeye ni insignificant
akileta mchezo unaweza kumuacha anytime?

Kama unamwacha mwache kabisa
vitisho vya kitoto vya nakununulia pipi/sikununulii pipi havina msingi saa hii

hasa kwenye issue sensitive kama hii
act as a man na sio 'show off ya mwanamme'

Nafikiria arudi kwao akapumzike kwanza, ili ashike adabu!
 
wala usimgombeze jaman , msamehe bure tena na yeye yuko kwenye kipindi kigumu kama nn, maana machungu yako ww yanapoishia ujue yake ndio yanapoanzia yan.
amini 2 huyu mtoto hakupangiwa na mungu(haikuwa riziki).
kuwa 2 na aman no wounder mtapata mwingine tena bila taabu yoyote.
kila la kheri kaka.
happy new year.
mpe pole mamito jaman.
 
Wanawake watiini waume zenu kwa yaliyo halali. Mke wa mtu hapaswi kutoka nyumbani kwake bila ya ruhusa ya mumewe. Akirudi kwanza afanye toba. Amemkosea Mungu wake kwa kukiuka amri halali ya mumewe. Pili msamehe amini kuwa Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi. Ana sababu zake za mimba hiyo kutoka. Usikasirike. Mshukuru Mungu kwa kila jambo. Muombe akujaalie upate mtoto mwema.
 
Nafikiria arudi kwao akapumzike kwanza, ili ashike adabu!
WE ACHA MASIHARA KWANI MTOTO ALIYEKUA AZALIWE ALIKU WAKO MWENYEWE? UKISHAMRUDISHA KWAO ITASAIDIA NINI MIMBA ITARUDI TUMBONI KWAKE? acha mambo ya ajabu mkanye kwa njia yyt lkn si kumfukuza
 
Tatizo lako kubwa linaonyesha ni shida ya watoto. Dawa yake mbandike mimba ya mapacha watatu au watano.
 
Nakuomba punguza jazba, mkeo anahitaji faraja sana ktk kipindi hiki ambacho ni kigumu kwake kumbuka yeye ni kiumbe dhaifu. Pengine MUNGU kaepusha shari kubwa zaidi ya hiyo ya kupoteza mtoto au pengine ninyi watunga mimba hamkutafuta mtoto kwa uongozi wa Mungu jichunguzeni. Wewe ni mwanaume umejaliwa ujasiri na busara kuliko yeye msaidie kuendelea mbele pia kumbuka mlango uko wazi kwake kwa sasa ni rahisi sana kushika mimba nyingine. Jitahidi kucontrol hasira ili mawazo mabaya yasipate nafasi na uuweke roho yako tayari kwa roho ya upendo na msamaha muda wote.
 
kwanza mke wako haelewi maana ya neno bed rest, pili wewe pia hukumsisitiza kukataa, ndio maana ulisema nenda sitahusika na mengineyo. kwa sasa yeye ameshapata adhabu ya kupoteza mtoto, usimwongezee nyingine,msamehe!
 
Halafu wewe itakusaidia nini?
Kumuonesha kwamba yeye ni insignificant
akileta mchezo unaweza kumuacha anytime?

Kama unamwacha mwache kabisa
vitisho vya kitoto vya nakununulia pipi/sikununulii pipi havina msingi saa hii

hasa kwenye issue sensitive kama hii
act as a man na sio 'show off ya mwanamme'

Lazima muelewe kwamba sia nia yangu kumtesa, lakini ni lazima a-face consequences
 
Pole sana na matatizo mkuu. Ila naona na wewe una kiburi sasa maana umeuliza umfanyeje huyo mwanamke na karibia wachangiaji wote wamekushauri umsamehe kwani naye hakujua na pia asingeweza kuyapenda yaliyomtokea. Wewe unakuja na jibu lako la kumpa adhabu ya kwenda kupumzika kwao kitu ambacho mimi binafsi naona sio sahihi, labda kama unasababu zako binafsi na haujazihusisha kwenye tukio hili. Mimi naona cha msingi ni kumsamehe, naye atakuwa amejifunza na kutambua kuwa kakuudhi, wewe mchukulie tuu na mpe pole na matatizo yote yaliyomkumba. Mtoto huyo ujue haikuwa riziki azaliwe na jitahidini mtafute mwingine, huwezi jua labda huko mbeleni angeweza kuhatarisha hata afya ya mama. Wewe mshukuru Mungu kwa yote na maisha yaendelee kama kawaida. Kila la kheri ila upunguze hasira mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom