Nimfanye nini huyu msichana

habari zenu wana jamvi.mimi nipo ughaibuni huku nasoma,sasa kuna msichana mmoja tuna uhusiano wa karibu miezi kumi sasa.kabla yangu mimi huyu msichana kashawahi kuwa na relationships mbili,wa kwanza waliachana kwa ugomvi sana na mpaka sasa ata wakikutana njiani ni kama maadui vile,ila huyu wa pili jamaa alikuja kusoma kwa semester moja then walikuwa wapenzi kwa karibu miezi miwili na nusu kisha jamaa akarudi kwao.ila kinachonitatiza mimi ni kwamba bado wana mawasiliano kwenye internet especially in facebook.miezi kama mitatu hivi iliyopita jamaa alimwambia msichana kwamba anataka kuja tena kusoma kwa summer time pekee ila alimwambia demu kuwa je akija wataweza kufanya mapenzi tena au la?basi msichana akawa amechanganyikiwa kweli ikabidi aje aniambie mimi maana anadai yeye jamaa anamchulia kama rafiki yake,mimi nikamwambia yeye uamuzi wake ukoje? demu akasema itabidi afikilie maana kachanganyikiwa hajui afanye nini ila mimi nikamwambia kwa kipindi hicho anachofikilia itabidi tuwe just friends na sio wapenzi demu akakubali japo kwa shingo upande.baada ya wiki moja na nusu demu akataka tukutane tuongee mimi sikuwa na kinyongo tukakutana then demu akasema kwamba anavyoona yeye jamaa anataka kumchezea tu then atamuacha kama alivyomuacha mwanzo then akaomba msamaa ili tuwe pamoja maana mimi ndio anaona mtu ninayemfaa sana kuja kuwa baba wa familia yake,mimi nikamsamehe japo kwa shingo upande,basi tukaendeleza uhusiano wetu kwa karibu miezi minne tunafurahi na kusahau yote yaliyopita.sasa tatizo linakuja yeye bado sometimes anaendelea kuchati na huyo jamaa yake japo huyu msichana ananiheshimu sana hana mambo ya kipuuzi,sasa last week alikuja kwangu kulala tukafanya mapenzi kama kawaida then kulala sasa katikati ya usiku demu akamuota jamaa yake huyo anaechati nae sometimes,asubuhi kuamka akaniambia ameota ndoto mbaya sana nikajaribu kumdadisi ila akusema kitu then next day akaja akniambia kuhusu hiyo ndoto ila imemchanganya sana kwa sababu yeye yuko na mimi tumelala pamoja sasa kwa nini amuote jamaa basi demu akawa kachanganyikiwa tena, mimi nikamuambia ile ni ndoto tu na si kweli demu akakomaa anadai inabidi afikilie ile ndoto inamaanisha nini maana ataki kuja kunibetray baadae maana ananipenda sana na mimi ni mwema sana kwake.akaenda kujadiliana na rafiki zake huko then akaja anasema eti ile ni ndoto tu na sasa hivi haipi sana uzito then tuendelee tu na uhusiano wetu kama kawaida.mimi ikabidi nisafiri kwa siku tatu kwenda kula bata then nikirudi nifikilie nini nitafanya,sasa leo ndio tunakutana tena sasa wadau mnanishauri nimwambie nini huyu msichana?nimuache au niendelee nae tu? ila demu mwenyewe ni mzungu ana 22 years old

kaka huyo anakuzingua tena kupita maelezo!kwako hajafika ila anapita tu.iko siku isio na jina atakuacha.ushauri wangu kwako ni hope for the best though prepare for the worst!
 
Kwani huko ughaibuni ulifuata shule au wanawake?you are finished!umeanzaje kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu asiye mkeo?huo ndio ukristo? au uislamu? au dini gani inakufundisha hivyo?
 
Kimbia kaka kimbia, au kama uamini kuwa unaibiwa mtest kwa hali kama aliyokufanyia uoneatavyo kimbia! teh! unakazi mkuu
 
Bwamdogo ulifata kusoma huko ugaibuni hukufata mapenzi, mshika mawili moja humponyoka tena lile na lamsingi,sasa basi soma kwabidiii ili uweze kuwapata wazungu wa hindi wa japani na kila mashaka ya dunia ya kike utayapata endapo umemaliza shule na unashahada yako nzuri,wasichana wako wengi huyo wala hajaelekea kama anakutaka anataka kukuonja2 akutoe jasho basi.
 
endelea kugonga kama kicheche tu,ila usiweke moyo wako hapo, ukimaliza ishu zako huko mmwage usonge front ! Hajitambui huyo demu!
 
Unababika kwa kuwa mzungu au nini. MOD and Invisible tunaomba mturuhusu kuwachapa vibao watu kama hao. Hivi kweli kusoma hujui kwa hiyo hata picha huzioni. Kaka kazi unayo: utaliwa demu wako mpaka basi
 
huyu mjamaa anaitwa gungwe kanifurahisha sana!wazungu hawafai!kwanza hawaogi,mswaki hawapigi!unawashobokea kitu gan?
 
Hali kama hiyo karibu kila mwanamke anaipitia; kudecide! Tofauti na huyo Mzungu, sisi wabongo tusingekuwa open hivyo ndoto n the like!

Sikushauri kuwa mbaguzi wa rangi, lkn tegemea uwazi Kama huo katika maisha yako na huyo yote; divorce ni nje nje with reason kama, ..."l was too young when l decided to marry u".... Uvumilivu kwao ni zero, ila wanategemea wewe uwe mvumilivu!
 
wazungu toka lini wana heshima? kwanza hujamkuna kabisa huyo mlami ndo maana unamduu usiku anamuota X wake. achanacna hiyo kitu soma kwa bidii kijana bongo wapo watoto wa kiafrika wazuri tu na wenye heshima watakutunza vizuri tu achana na hao walami wasojua kutunza mali zao
 
Inatia kinyaa kusoma ila bora umaskini mwinge wowote ule kuliko wa akili.
 
Hapo ulipo upo nchi ya watu,una stress ya kukosa mapenzi ya wazazi na ndugu wengune. usije ukajiongezea stress. mpe condicion akiafikiana then anakupenda endelea la amekataa achana nae. Mimi pia nilikuwa katika mazingira yanayofanana na yako,mwishowe I had to be strong nilitoa condicion na demu alirudi mwenyewe very stressed baada ya kushindwa kuishi bila mimi.nilimzingua kidogo kuona kama yuko serious it was right,then u need to be strong,wanawake bado wengi, zaidi ya hayo nje ya home hatupendani kivile ni kusaidiana tu kupeleka siku ziende.
 
thx kwa ushauri mkuu
we si unawajua man hawa watu wakiwa kwenye relationship wanasettle labda huyo wako ni point five mi navyowajua ukimtokea anakwambia ninaye boyfriend tena mkikutana na ex wake anakwambia huyo alikuwaga ex boy wangu sasa hizo story zako zote huyu labda ni zeruzeru tu atakuwa mbongo pure au kajijubua au kama ni mzungu may be from bad girls club so take care hi hayo tu mkuu
 
Yaani wewe kaka hivi hili ni swala la kujipa mawazo,embu muache upesi huyo msichana hakupendi,na anakuambia kidiplomasia kwa picha wewe huoni 2,nionavyo wewe ndio unamzimia huyo dada yaani unampa muda m2 wa kufikiria kuhusu kufanya sex na ex wake are u insane?stop it umenikwaza,ungekuwa kaka yangu ningekupa mangumi ya hatari,
 
Kwanza wewe unaonaje kati ya kumuacha au kuendelea naye....msimamo wako kwanza ni muhimu kabla ya kutoa ushauri
 
Mkuu huyo shost naona anakutega na kukuzingua ipasavyo. Nakushauri uachane nae, afta ol bongo madem wapo wakumwaga!
 
Back
Top Bottom