Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,969
"RAIS AONGEZE, ASIPUNGUZE MISHAHARA
SAKATA la mishahara minono ya vigogo katika mashirika ya umma, limekuwa sehemu ya mazungumzo kila mahali, hasa kwenye vyombo vya habari.
Mazungumzo hayo ambayo yamebeba mawazo tofauti, yametokana na kauli ya rais kwamba, amekusudia kupunguza mishahara ya baadhi ya eatendaji wakuu katika mashirika ya umma.
Rais hakutumia maneno mepesi,. Alisema, kwa mishahara yao minono , watendaji hao wamekuwa wanaishi kama malaika na kwamba ataishusha ili waishi kama shetani.
Haya ni maneno yasiyotarajiwa kutamkwa hadharani na kiongozi mkuu wa nchi.Hayapaswi kutoka Ikulu.
Kwa rais kutamka haya ni dalili kwamba anatumia ushauri wa watu wasiojua jinsi mishahara ya watendaji hao inavyopangwa, au uvumi wa wananchi masikini wanaodhani kwamba watendaji hao wanalipwa kiasi kikubwa mno wasichostahili.
Kumwambia masikini anayebangaiza mlo wa siku kwamba kuna watendaji wanaolipwa Sh. 36 milioni kwa mwezi, ni kujaribu kujenga uhasama kwa jamii.
Ni njia ya kuchochea masikini kuchukia mafanikio au watu waliofanikiwa.
Hata kauli yake kwamba anatamani watu waishi kama shetani , sio kauli inayopaswa kutolewa na kiongozi mkuu wa nchi, hata kama kuna baadhi ya wasikilizaji wake wanapigia makofi kauli hiyo.
Kupunguza mishahara ya watu ambayo imepangwa kwa mujibu wa taratibu zisizotegemea kauli yake, ni ubabe tu.
Taasisi zinazosimamia zina viwango vya mishahara ambavyo huwekwa na bodi kwa vigezo rasmi vinavyoongoza taasisi hizo.
Lakini kwa kauli za rais, ni wazi kuwa anawajengea wananchi hisia kwamba wakuu wa taasisi hizi “wanajipa mamilioni”.Anataka jamii iwaone kama wezi.
Sisi tunaamini kwamba wananchi makini hawawezi kubabaikia kauli za kibabe za rais ambazo zinachochea, zinaenzi na kutukuza ubabe.
Hatuwezi kuingia katika mkumbo wa kutukuza kila kauli anayotoa rais, huku tukijua kuwa kwa kufanya hivyo, tunajenga uhasama kati ya wenyenacho na wasionacho.
Na tunadhani kuwa rais angekuwa amelitendea haki taifa , angejibisha kuinua uchumi , ili mishahara ya wafanyakazi wote ipande badala ya kupunguza mikubwa iliyopo.
Hao wenye mishahara mikubwa siyo wezi. Ni watu waliowekeza katika elimu, ujuzi, uzoefu na stadi mbalimbali zilizowafikisha katika ngazi za juu kiuongozi."
Source: MwanaHalisi 04/04/2016