Wakili Mkuu wa Serikali Aliombe Taifa Radhi Kwa Kulitweza Mbele ya Rais

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Kauli zandiki ya Dr. Boniface Luhende Wakili Mkuu wa Serikali WMS kumtaka rais atengeneze bajeti nyingine mpya ya ziada ya kuanzisha Kituo cha Pamoja cha Kutoa Haki (One Stop Center) kwa walioikosa sehemu stahiki zinazopaswa kutoa haki husika siyo kauli ya kipapa ambayo haiwezi kupingwa.

WMS amelidhihaki taifa, rais na mamlaka ya rais kwa kauli hiyo mbovu inayolenga kuhujumu uchumi wa nchi na kuendeleza uzembe na ufisadi (ulaji) wa rasilimali za taifa kupitia kituo hicho alichopendekeza.

Wasomi na wataalam wa Tz wamerogwa na nani kiasi hiki cha WMS? Idara ya Mahakama ya Tanzania imefeli kiasi hicho? Watanzania walitarajia siku ile ile pale utumishi wake katika ofisi hiyo na wadhifa huo vingekoma kwa decree ya rais.

Wakati umma ukitambua, kuheshimu na kuvumilia haki yake ya kikatiba ya kutoa maoni; umma huo unajiuliza WMS anapata wapi ujasiri wa kupotoka na kuropoka mbele ya mteuzi wake bila hata kuhariri na kutathmini alichosema ambacho kimezua taharuki kubwa kwa umma kuhusu nia isiyo njema ya taasisi yake kutohurumia rasilimali chache za nchi ili keki ya taifa angalau igawanywe hata kwa uwiano mbovu.

Yafuatayo ni madhara ya kauli hiyo hatari ya WMS:-

1. WMS amethibitisha kuwa sekta ya sheria imeshindwa wajibu wake hadi inahitaji msaada wa One Stop Center.

2. WMS amethibitisha kuwa waliohukumiwa na Mahakama hiyo ambayo inaombewa msaada wa One Stop Center labda wameonewa.

3. WMS amethibitisha kuwa taasisi zote zinazohusika kwenye mchakato wa kusimamia sheria na kutoa haki zimepotoka, hazistahili kuwepo na watendaji wake wakuu wanahujumu taifa kwa kupokea mishahara na maslahi mengine wasivyovitendea haki (lame duck)

4. Kwenye hiyo no. 3 WMS amewachongea AG, CJ, PJ, SG, IGP na labda CGP kuwa utendaji wao haujalisaidia taifa hadi ikahitajika taasisi nyingine tena ya One Stop Center kuwapa msaada ili pengine pia kumpunguzia kazi Katibu Mwenezi wa CCM taifa anayelazimika kufanya kazi za hao watendaji kwa kasi na tija vinavyotarajiwa na WMS kwenye hiyo One Stop Center.

5. WMS amethibitisha kuwa kama Kituo cha Pamoja cha Kutoa Haki kitaanzishwa basi kazi kubwa kwa Katibu Mwenezi CCM taifa itapungua na atajielekeza kwenye kazi zingine za kukijenga chama hususan kipindi hiki cha chaguzi.

6. WMS amethibitisha kuwa umati mkubwa ule unaomzonga Katibu Mwenezi CCM taifa basi utahamia kuvizonga vituo hivyo vya pamoja vya kutoa haki (hususan haki iliyohujumiwa au iliyonyimwa) ili kupata kile ambacho Katibu Mwenezi CCM taifa amekuwa akiwapa.

7. Rais akitekeleza ushauri huo au ombi hilo la WMS ni dhahir shahir kwamba vyombo vya kusimamia sheria na kutoa haki vitakuwa vimefeli na havina kazi kwa sababu wateja wao watahamia kwenye vituo hivyo vya pamoja vya kutoa haki ili wakapate utendaji wenye ladha ya Katibu Mwenezi CCM taifa.

8. No. 7 hiyo ikitimia, WMS atakuwa amefanikiwa kuvifitinisha vyombo hivyo, vituo vya pamoja vya kutoa haki, Katibu Mwenezi CCM taifa na rais.

9. WMS amethibitisha kuwa hizo One Stop Centers zitakuwa zimetanua wigo wa rushwa maana hiyo ndiyo saratani ya sekta ya sheria nchini maana hata watendaji wa hizo One Stop Centers ni binadamu wale wale tena ambao watakuwa wameajiriwa kutokea kwenye taasisi (mainstream) za kusimamia sheria na kutoa haki. Vinginevyo wazalishwe Makonda wengi ndiyo wakaajiriwe kwenye hizo One Stop Centers kwa kuwa WMS amegundua kuwa watu wanamzonga Makonda kupata haki zao bila kutoa rushwa.

10. One Stop Centers za Forodha hazijaondoa rushwa na urasimu mpakani kama ilivyotarajiwa kwamba zingekuwa ndiyo mwarobaini wa rushwa na urasimu. Ufanisi bado haujafikiwa kwa viwango tarajali.
 
Back
Top Bottom