Nimewashangaa sana Lissu na Heche baada ya kusikiliza mjadala wa Royal Tour kwenye Club House ya Maria Sarungi

Mlitakaje?
Hv hio movie bila uwepo wa Rais kuna mtu angeangalia?

Bila uwepo wa huyo mzungu na profile yake kuna mtu angepay attention?

Gharama mshaambiwa sio za Serikali..na ht km zingekua za Serikali anachofanya mama ni kibaya?

Alternative views za watu kupewa hela sijui wakanunue ng'ombe?

Mi naona tu they r js trying to be relevant ila kwenye hili wamefeli

Hivi billion 9 kwa dakika 56 na billion 9 kuwaempower vijana kipi Cha Msingi?
 
Hawa viongozi kama kina Tundu Lissu na John Heche wanapaswa pia kuwa na Principles fulani za kusimamia!
Huwezi kuwa kila wakati unaongea ongea tu!
Hakuna mtu anayejua kila kitu na huwezi kuhojiwa na kila mtu!
Naona hizi Space na Club house zimeshusha sana credibility za hawa watu na kuwafanya irrelevant kabisa!
Nilicheka sana kwenye mjadala wa uhifadhi na uhamishaji wa Wamasai kutoka Ngorongora kulinda uhifadhi.
Mchungaji Msigwa akawa anatema madini huku Tundu Lissu ameng'ang'ania Wamasai waachwe ila wakati wa mvua wawe wanahamia milimani! Akatema pumba siyo za Nchi hii!
Nanukuu;
"Akatema pumba siyo za Nchi hii!"
 
Nina rafiki msomi na yuko Chadema kufa na kupona, amekuwa sana akiniambia kuhusu Club house inayoendeshwa na Maria Sarungi. Leo nikaamuwa nami nisikilize mjadala wa Royal Tour ambapo Mary Sarungi alikuwa akiwahoji Tundu Lisu na John Heche. Kwakweli baada ya kusikiliza mjadala na kusikiliza hoja zao kuhusu kupinga Royal Tour nimewadharau sana Lisu, Heche na Maria Sarungi mwenyewe.

I won't go into details ila nitataja hoja moja moja tu za Lisu na Heche ambazo kwanza nashangaa wanakuwaje viongozi wakubwa hivyo ndani ya chama kikubwa.

1. Lisu anasema SSH kaenda US kutangaza utalii wakati wakiti watalii wakija ni wageni wa private serious?????? Kweli huyu ilikuwa anaomba Urais mtu asiyejuwa kazi ya kutangaza attractions za nchi niza Serikali??? Private sector kazi yake ni grasp opportunities baada ya Nchi kujulikana. Sababu kubwa yakuwa na namba ndogo ua utalalii hapa nchini ni kwamba only deals with tradion markets instead of opening other avenues hivyo nchi haijulikani.

2. Heche nae anasema gharama zilizotumika kutengeneza Royal tour wangepewa vijana wakanunue ng'ombe wa maziwa wafuge kuliko kutengeza Royal tour??? Serious? Halafu huyu jamaa ni mwalimu alikuwa anafundisha sekondari anajaribu ku compare kutangaza utalii wa nchi na kuwapa vijana hela wakafuge. Sikatai vijana wetu kukopeshwa ila kama Nchi inaweza ikakopesha vijana wetu hela za Ngo'mbe na Royal Tour pia ikafanyia.

3. Maria mimi simjui ila kulingana na watu wanavyo muongelea sina shaka kwamba ni msomi na ana expousure. Kilichonishangaza ni alivyokuwa yuko impressed na bizzare analysis inayofanywa na viongozi wajuu wa Chadema.

Kumalizia. Lisu na Heche niliokuwa na wajuwa kujenga pale Bungeni siyo nyie. Inawezekana kuwa out of active politics na brains zenu zimekuwa drained au ni frustration na serious Maria comments za watu wazito kama hawa nizakutoa on air ili kulinda heshima ya platform.
Kwenye club house wanapaswa kualika watalamu wawili wa jambo husika Lisu na Heche hawajui kiwanda cha utalii hata kwa asilimia 2
 
A combination of both methods itumike

Wabongo wanaenda china kwa sababu za kibiashara sio kiutalii

WaTZ wengi naona utalii is just not in us hata kama tuna uwezo..
Sasa utategemeaje wajue mambo ya Seychelles na Maldives?
Kuna soko kubwa la Wamarekani weusi na ndugu zetu waliohamia Marekani na Ulaya lakini hatuwaoni. Tunawakazania tu wazee wakizungu wakati vijana wengi sasa hivi ndio wanasafiri.

Amandla...
 
Lissu Ni mzuri kwenye hoja za kisheria.

Kwenye Mambo mengine ni trash kabisa Kama Mdude.

Heche Hana tofauti na Mdude na hajui chochote zaidi ya kukaza fuvu kubishana na kupinga. Heche, Mdude, Lema wore akili ZINAFANANA.

Maria yeye anaongozwa kwa CHUKI Dhidi ya watu. Na ndio maana hata kabla ya mjadala yeye tayari huwa ana conclusion yake. Kama hukubaliani naye kwanza anakublock. Ni mtu fulani mwenye matatizo ya AKILI.

Mtu ambaye at least huwa anajenga hoja inaeleweka Ni Zitto ingawa kwasasa ana maadui wengi, kwahiyo hata atoe hoja nzuri vipi hawata muunga mkono kwasababu wanaona kama wanampa sifa na kumpandisha kisiasa gym wakati lengo la apotee na asisikike
Nanukuu tu
"Heche Hana tofauti na Mdude na hajui chochote zaidi ya kukaza fuvu kubishana na kupinga. Heche, Mdude, Lema wore akili ZINAFANANA."

Baba mtumishi Pep hii imekaaje mkuu?
 
Hivi billion 9 kwa dakika 56 na billion 9 kuwaempower vijana kipi Cha M

Naunga mkno kuwe na sera ya kuwezesha vijana tena wapewe hata zaidi ya bilioni 20 ila siungi mkono hoja kuipinga ku deploy 9 billion kwenye kutangaza utalii wa TAIFA. Kwasasa kwenye utalii tunawekeza kama 3billion kwa mwaka and our yield is USD2.5Billion kwa mwaka. Avator yako ni Economist sijui ni jina tu au ni mchumi kweli kama mimi
 
Wako sahihi!, kwani tungewawezesha vijana wetu wakajiajiri kama alivyopendekeza Heche mbona tungekuwa mbali sana,
Angalia umeme unavyosuasua wakati nishati hii imewaajiri vijana wengi, tunaweka siasa kwenye mambo ya msingi sana!
 
Mbona hawajaitangaza Burigi? Unatangazaje kitu kilichokwisha jitangaza?.
 
Sisi tunasema wapi?

Halafu huu muda unatumia kubweka bweka mitandaoni, ungeutumia kujifungua kuandika ili siku nyingine usiandike STIRLING
Halafu uwe na nidhamu ,wow ndio wanabweka watu wanaongea na kutoa mitazamo yao au kuandika.
 
Sasa utategemeaje wajue mambo ya Seychelles na Maldives?
Kuna soko kubwa la Wamarekani weusi na ndugu zetu waliohamia Marekani na Ulaya lakini hatuwaoni. Tunawakazania tu wazee wakizungu wakati vijana wengi sasa hivi ndio wanasafiri.

Amandla...
Royal Tour si inawafikia watu wa aina zote amaa?
 
Royal Tour si inawafikia watu wa aina zote amaa?
Mke mwenzake Meghan wewe! Watu wa aina gani wanaangalia PBS? Kule kila kundi na Channel zake. Watu wa Trump utawakuta Fox, wa Biden utawakuta MSNBC na CNN. PBS inayorusha Royal Tour nayo ina watu wake.

Amandla...
 
Achana nao wameshakua wanasiasa wa hovyo hovyo.

Haiwezekani mama anafanya Yale waliyoyapigania Kwa miaka mingi halafu wanapinga TU bila hata aibu.

Kuna mjinga Mwingine nimemsikia akisema eti Filam ya Royal tours haitainufaisha Tanzania Kwa sababu hati miliki ni ya Mtu binafsi.
WAKATI huo huo anasema huyo aliyitengeneza Kwa Nini aitengeneze Kwa gaharama zake atanufaikaje? Yaani mambo ya kipumbavu kabisa .

Yaani mtu anakutangazia nchi Kwa gaharama zake Kwa sababu TU yeye anataka anufaike na filam na wewe iwe ni matangazo halafu unalalamuka kwani angeacha tungenufaika nini? Mbona waafrika tupo hapa miaka mingi lakini hatukuwaza kutengeneza filam kama hiyo. Dunia ni Kijiji MTU yeyote akishirikiana nasi Kwa ajili ya maendeleo sio kuvuruga amani basi ni ndugu yetu kama Bongo zozo.

Lisu ameanza kuwa Mwanasiasa wa hovyohovyo.
Msigwa ameonyesha wazi kuwa anafaa kuwa Waziri wa utalii.

Mama Samia anapaswa kumteua Msigwa kuwa Mbunge na Kisha amteue kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Mama Samia Kwa kiasi Fulani ni Mpenda Demokrasia Kwa hiyo ni Wehu TU ,Machozi, Wanasiasa wa hovyohovyo , mafala , malofa na wapumbavu wasio na shukrani , wanasiasa wasio na dira watampinga na kumukana kama vile walivyokua wanapinga Marais waliomtangilia kutoka bara ambao Kwa hulka zao TU ni watu katili na wabinafsi na walafi.

Mama Samia ni Tofauti sana na Watawala waliolivuruga hili Taifa Kwa kujilimbikizia Mali na marafiki zao ambao wengi wao ni wale waliosoma pamoja kwenye baadhi ya vyuo ambavyo vingi vimekua chanzo Cha kuasisi Mafisadi na wanasiasa Wabinafsi wanaolitafuna Taifa hili bila huruma.

Kwenye club house wanapaswa kualika watalamu wawili wa jambo husika Lisu na Heche hawajui kiwanda cha utalii hata kwa asilimia 2
Wale wakialika wataalamu labda wawe upande wao
 
So u think everybody in the US ama Europe anaijua Tanzania?..especially raia wa kawaida?

Was in DC once ktk kusalimiana mtaani tu hv nkasema am from Tanzania hawapajui..kusema East Africa bado hawapati picha kusema Ethiopia,Eritrea na Kenya ndo they were ahhh okayyy that side...

Ni kama vile we saivi how much do you know about Papua New Guinea?ama Barbados...Maldives je?unapajua
Seychelles na Mauritius?!
Acha kujua jina la nchi..vivutio vya ndani unavijuaaa?
Mkuu,heshima kwako.
Kwenye suala LA watalii wanajua wenyewe msimu na muda wa kuja na wapi pa kuja. Istoshe watalii wengi hutokea ulaya so it is irrelevant kufanya uzinduzi marekani wakati target kubwa iko ulaya.
Pia usidhani hao tembo na faru wako huku tu....wako na kwingine kule. Kikubwa we don't need to make noise for them to come.....anyway tujipe muda.
 
Lissu aliulizwa swali huko clubhouse aeleze kwa nini Tanzania ni masikini na ifanye nini ili iweze kuendelea akajibu hivi:
Sikiliza hiyo audio
 

Attachments

  • AUD-20220502-WA0064.aac
    969.6 KB · Views: 5
Royal Tour was a bad idea.

Nguvu, muda na fedha zilizotumika haviendani na impact yake kwenye soko.

Pale ni hasara tupu.
 
Ukianza na Sarungi yule anajiita mwanaharakati lakini naona yupo kwenye kupinga kila kitu cha serikali kwake hakuna jema inafaa ajitambulishe tu ni mwana Chadema.
Ukija kwa viongozi wa Chadema nilitegemea wakati huu ambao kuna mfumuko wa vitu kupanda bei wao ndo wawe mstari wa mbele kufanya mikutano na kutoa analysis ya nini kifanyike kama kuna vipengele vyovyote vifanyiwe kazi watoe ushauri lakini wengi wao utawakuta Club house ,Kufanya mkutano kwenye redio na TV ni tofauti na kuwa Keyboard warrior wa Twitter .
Wana mkakati wa Chadema wanawaangusha sana namiss sana zile old days za kina Zitto,Mnyika akina Slaa walikua vichwa kweli sijui nini kimewapata?
 
Mkuu,heshima kwako.
Kwenye suala LA watalii wanajua wenyewe msimu na muda wa kuja na wapi pa kuja. Istoshe watalii wengi hutokea ulaya so it is irrelevant kufanya uzinduzi marekani wakati target kubwa iko ulaya.
Pia usidhani hao tembo na faru wako huku tu....wako na kwingine kule. Kikubwa we don't need to make noise for them to come.....anyway tujipe muda.
US has influence jmn
Ulaya tungeenda nchi gani?
 
Back
Top Bottom