Uthubutu na ushupavu wa Rais Samia umefufua sekta ya utalii nchini, wasaidizi na wadau tuendelee alipoishia

AFRIKAMOJA

Member
Aug 11, 2022
30
37
Royal Tour ni Brand ya Rais Samia Suluhu Hassan kazi kubwa ameifanya kutangaza utalii. Royal Tour imekuwa ya mafanikio makubwa. Changamoto kubwa inayoonekana wasaidizi wake hakuna juhudi za kimkakati wanazozifanya kuendelea pale alipoishia.

Bado kazi haijafanyika vya kutosha kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Samia badala yake wasaidizi wake na wadau wameishia kusifia tu Royal Tour badala ya kujipanga vyema kufikia lengo lake.

Kama vile juhudi za kuhamasisha na kuvutia wawekezaji na wafanyabishara wa ndani na nje kujenga mahoteli, kuboresha huduma za kitalii, kuhamashisha mageuzi ya kisekta ili kuongeza bidhaa za kitalii, kuyafikia mataifa yenye wananchi wanaopenda kusafiri duniani pamoja kuondoa urasimu katika kuhudumia watalii.

Aliamua kuruhusu chanjo dhidi ya Uviko-19 ili kuunga mkono juhudi za ulimwengu kukabiliana na maradhi hayo yaliyotikisa uchumi wa dunia. Uamuzi huo ulipelekea nchi yetu kuondolewa kwenye orodha ya mataifa yasiyo salama kutembelewa hali iliyoimarisha sekta ya utalii kwa kuwa wageni walianza kufurika.

Pamoja na upotoshaji mwingi wa athari hasi za chanjo hiyo ikiwemo Watanzania kuaminishwa kuwa chanjo ya Korona itawafanya mazezeta, mazombi au itawapa ugumba lakini bado Mheshimiwa Rais Samia alisimama Imara na kuongoza Kampeni ya kuchanja.

Binadamu tumeumbwa kusahau na kubeza lakini ni ukweli kuwa ushupavu wa Rais Samia ndio umefufua Utalii wetu uliokuwa umedorora kupitia chanjo na kuutangaza ulimwenguni kupitia filamu maalum ya Tanzania The Royal Tour. Hongera Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hapa uliupiga mwingi!

IMG-20220911-WA0038.jpg
 
Back
Top Bottom