Sharp Observer
Member
- Apr 11, 2011
- 59
- 41
Wadau, wiki liliyopita nilikuwa moro kwa mambo yangu binafsi. Mishale ya saa tano nikatinga baa moja kupata maji ya ilala. Mezani nilipokaa nilikuwa peke yangu, kupiga funda tatu tu, jimama akajipitisha. Baada ya kufika mezani kwangu, akauliza kama anaweza kukaa, nikamwambia kaa.
MWANAMKE KUMTONGOZA MWANAUME KAZI. Naye akajiagizia, akaanzisha mazungumzo fastafasta, lakini akiwa tayari kalewa, akajitambulisha yeye ni mwalimu, mc, ana undugu na mwanasheria mkuu wa serikali aliyestaafu (Mwanyika kama sijkosea), vile vile ni mjasiliamali, longolongo kibao. Wakati huo sijamaliza hata serengeti moja niliyojinunulia, akaniagizia. Nikashukuru ila nikamwambia mhudumu akae nayo kwanza maana ilikuwa ugenini na bado sijasoma ramani vizuri.
Awali nikahisi mwanamke yule ni chizi au ana frustration. Akanyanyua simu kumpigia mtu, huku sijui hili wala lile akaja mwanaume mmoja akamkwapua ile simu. Nikaanza kupata ramani ya vita. Jimama likaniomba angalau namba ya simu huku likidai hali ya hewa imechafuka, ikibidi nimpatie mhudumu ili ampatie, bado nazubaazubaa, yule mwanaume akarudi akamwaga pombe iliyokuwa kwenye grasi ya jimama na kufoka "kwani huku kwangu pombe zimeisha". Hapo nikahama meza.
Jimama hakuridhika, akamwachia maelekezo mhudumu amchukulie namba yangu, jimama akaondoka na bwana wake. Kufika mbele jimama akarudi bar, bwana wake akarudi kumchukua tena, ndio wakaondoka jumla.
NILICHOJIFUNZA

- Hata wanawake wanajimwagia sifa wakati wa kutongoza
- Wanahonga ili kutongoza
- Ukiwa ugenini kuwa makini na kila mtu aliyekaribu yako