Nimetokewa na mauza uza kazini kwangu, naomba ushauri

JITABOY

JF-Expert Member
Sep 2, 2013
254
35
Nilitokewa na mtu akiwa ni mwanamke aliye kuwa amejifunga kiremba che ----- dukani kwangu akihudumia watu pindi ninapo toka kwenda kupata chakula.

Nanimekuwa nikipoteza pesa tena nyingi tu hapo kazini bila kujua zinaelekea wapi na zinatokaje.

Hivi jamani huyo ni mtu wa kawaida au ni jini?

Nitawezaje kulidhibiti hilo tatizo?

Mimi binafsi sijawahi kumuona bali naambiwa na wateja wanaokuja pale wakati mimi sipo.
 
Nilitokewa na mtu akiwa ni mwanamke aliye kuwa amejifunga kiremba che ----- dukani kwangu akihudumia watu pindi ninapo toka kwenda kupata chakula.Nanimekuwa nikipoteza pesa tena nyingitu hapo kazni bila kujua zinaelekea wapi na znatokaje.Hiv jamani huyo ni mtu wa kawaida au ni jini? naje? ntawezaje kulzbiti hlo tatizo? mimibinafsi cjawahkumuona bali naambiwa na wateja wanao kuja pale wakati mimi sipo.

Fanya maombi mara moja huyo ni jini. omba sana pia shirikiana na wanamaombi.
 
duu mkuuu kuna mtu anataka cheo chako..kuna mfanyakazi mwenzako upo nae ofisi moja anataka kukutoa duniani .usipokuwa makini utaiaga dunia cha umuhimu wahi kwenye maombi ..fasta.....haya mambo yapo sana ofisi
za serikali ...tena hasa hasa
1.tra
2.bandarini
3.uhamiaji
4.ofisi za bunge...
5.wizara ya nishati na madini
6.udsm....
 
nenda kwenye maombi fasta, ukiweza tafuta annointed water ya tb joshua pale benjamin mkapa tower
 
duu mkuuu kuna mtu anataka cheo chako..kuna mfanyakazi mwenzako upo nae ofisi moja anataka kukutoa duniani .usipokuwa makini utaiaga dunia cha umuhimu wahi kwenye maombi ..fasta.....haya mambo yapo sana ofisi
za serikali ...tena hasa hasa
1.tra
2.bandarini
3.uhamiaji
4.ofisi za bunge...
5.wizara ya nishati na madini
6.udsm....

DU......!
 
Nilitokewa na mtu akiwa ni
mwanamke aliye kuwa amejifunga kiremba che ----- dukani kwangu
akihudumia watu pindi ninapo toka kwenda kupata chakula.

Nanimekuwa nikipoteza pesa tena nyingi tu hapo kazini bila kujua
zinaelekea wapi na zinatokaje.

Hivi jamani huyo ni mtu wa kawaida au ni jini?

Nitawezaje kulidhibiti hilo tatizo?

Mimi binafsi sijawahi kumuona bali naambiwa na wateja wanaokuja pale
wakati mimi sipo.
Tubu dhambi, mpokee Yesu, na shirikisha watumishi wa Mungu uombewe kwa Jina la Yesu na uendelee kumtegemea Mungu kwa Jina la Yesu.
 
Hilo duka ni la kwako au umeajiriwa tu? Kama sio lako. basi hayo ni mauzauza ya mwenye mali, na kama ni lako, jiulize mara mbili kama mali hiyo umeipata kihalali pasipo kutoa kafara ndugu yako. Kama umeajiriwa, acha kazi katafute kazi kwingine na kama duka ni lako, ujipime umepaje mali hiyo vinginevyo ujisalimishe kwa Mungu wako. DAIMA KWELI ITAKUWEKA HURU.
 
Huyo ni chuma ulete tena amekuwa sugu mpaka anaonekana live tafuta njia ya kumchomoa hapo la sivyo kazi unamfanyia yy
 
Porojo.

Wakati yeye hayupo anamuwacha nani? anawacha biashara yake bila kuwepo mtu?

Habari za kufikirika au mleta mada ni "schizophrenic".

Wakati mimi natoka huwa c mwachi mtu ispokuwa nawambia jirani zangu kwamba muniangalizie hapa akija mteja munibeep na mimi uwa naondoka na hela zangu na simu za kawz.
 
Fanya maombi mara moja huyo ni jini. omba sana pia shirikiana na wanamaombi.

Ahsante sana kaka ukweli nimeanza maombi na nilijaribu kumshirikisha mchungaji fulani hapa na tumeanza maombi.
 
Toa sadaka yawezekana hata maskini husaidii wewe

Nikweli kabisa kwamba sadaka huwa ctoi maana ukweli hata kanisani nina miaka mingi sana siend binafsi nina moyo wa kusaidia japo sina kipato kikubwa.
 
Hilo duka ni la kwako au umeajiriwa tu? Kama sio lako. basi hayo ni mauzauza ya mwenye mali, na kama ni lako, jiulize mara mbili kama mali hiyo umeipata kihalali pasipo kutoa kafara ndugu yako. Kama umeajiriwa, acha kazi katafute kazi kwingine na kama duka ni lako, ujipime umepaje mali hiyo vinginevyo ujisalimishe kwa Mungu wako. DAIMA KWELI ITAKUWEKA HURU.

Hiyo kaz niyakwangu mwenye na ktk kuipata nimepat kwa njia halali,kabisa na mali yenyewe siyokubwa sana,nadhanh ni mchezo wa watu ambao hawapendi maendeleo ya watu.
 
Nenda kwenye maombi na leta mtumishi wa maombi aje kuombea duka lako. Hiyo ni chuma ulete. Ni utafanikiwa kama unaamini Mungu anaweza. Ila sijui wewe ni muumini wa dhehebu gani. Hapa nimekushauri kikristo.
 
Hujakosea kaka mimi mwenyewe mkristo ukweli nilijisahau katk mambo ya maombi na tangu nizaliwe sijaknyaga kanisani zaid ya mara 10.Nashukuru sana kwa ushauri wenu ndg zangu amen!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom