Nimesikitishwa sana baada ya kuona kwenye CCTV vitendo alivyofanya shemeji yangu.

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,936
32,342
Wanabodi JF.

Mie sio mwenyeji sana huku nimeona nije nipate michango yenu kutoka kwenu wadau wa MMU.

Kuna rafiki yangu wa karibu mke wake anafanya kazi benki mmoja maeneo ya posta mpya, mara nyingi anafanya kazi mpaka mida ya saa mbili usiku (part time).

Shughuli zake za kibenki zipo ghorofa ya saba ndio kuna ofisi yake, wakati anatoka kazini mida ya saa mbili usiku huwa anapanda lifti na mmoja wa mfanyakazi mwenzake wa kiume, mida hiyo ofisi zote zimefungwa kwenye jengo hilo.

Kinachofanyika kwenye lifti ni kunyonyana ndimi na kufanya machafu, tuna rafiki yetu pale kwenye hilo jengo yupo kitengo cha CCTV Control room ambaye ndio kanionyesha shemeji yetu anavyofanya uchafu huo.

Bahati mbaya rafiki yetu ambae mwenye mke kaambiwa lakini hataki kuona hizo picha za video za mke wake akifanya uchafu kwenye lift.
 
Kalishwa limbwata utateseka bure, achana Naye au Kama unataka uwe na Amani muombe limbwata Shemeji yako pia.

Wanabodi JF.

Mie sio mwenyeji sana huku nimeona nije nipate michango yenu kutoka kwenu wadau wa MMU.

Kuna rafiki yangu wa karibu mke wake anafanya kazi benki mmoja maeneo ya posta mpya, mara nyingi anafanya kazi mpaka mida ya saa mbili usiku (part time).

Shughuli zake za kibenki zipo ghorofa ya saba ndio kuna ofisi yake, wakati anatoka kazini mida ya saa mbili usiku huwa anapanda lifti na mmoja wa mfanyakazi mwenzake wa kiume, mida hiyo ofisi zote zimefungwa kwenye jengo hilo.

Kinachofanyika kwenye lifti ni kunyonyana ndimi na kufanya machafu, tuna rafiki yetu pale kwenye hilo jengo yupo kitengo cha CCTV Control room ambaye ndio kanionyesha shemeji yetu anavyofanya uchafu huo.

Bahati mbaya rafiki yetu ambae mwenye mke kaambiwa lakini hataki kuona hizo picha za video za mke wake akifanya uchafu kwenye lift.
 
Ritz, wanadamu hatufanani. Keshaambiwa na ujumbe ameupata, wakati ukifika atafanya maamuzi na si lazima yafanane na unavyotaka wewe.
 
Wanabodi JF.

.......Bahati mbaya rafiki yetu ambae mwenye mke kaambiwa lakini hataki kuona hizo picha za video za mke wake akifanya uchafu kwenye lift.

Hataki kuziona au hataki kuchukua hatua.....
 
Mbaya sana hii! Kama jamaa kaambiwa mpaka na ushahidi upo na hataki kuchukua hatua basi hilo nalo ni tatizo

Swali kwa wadada wenye tabia kama hii hivi unakubalije kuolewa kama unaona huwezi kuheshimu misingi ya ndoa?

Swali kwa wanaume.. unajisikiaje kufanya mapenzi na mke wa mwenzio? imagine kibao kikigeuzwautajisikiaje?
 
ndo nini hapo kwenye red!
pampkin.jpg

pampkin.jpg

Kuna rafiki yangu wa karibu mke wake anafanya kazi benki mmoja maeneo ya posta mpya, mara nyingi anafanya kazi mpaka mida ya saa mbili usiku (part time).
 
ukikaa sana kwenye hayo macctv yao unakuwa kama unawala chabo watu,unaweza kuwa addictive charii.huyo charii yako anajipanga kutoa tamko.anataka aitishe kwanza CC yake ili imshauri...,we subiri tu utaona
 
Sasa wewe inakuhusu nini kama mwenye mke hataki we kinachokuuma nini,kama uliuomba akakunyima ndo maana umeamua umuanike humu JF,haitakusaidia hii we dili na mkeo,labda uwezi jua jamaa kashazoe na mama ndo anatoa matumizi we unataka umuaribie, MTU MZIMA KUWA MBEA HAIPENDEZI,UTAVALISHWA GAUNI WEWE
 
duu kumbe na kwenye lift kuna cctv?loh tutabambwa wengi.manejimenti huwa haipitii hizo records?itakua ppf tower crdb
 
Ni VIZURI SASA MWANAMKE NA HUYO MWANAUMME WAJULISHWE KUWA MAMBO YAO YAPO HADHARANI MAANA WOTE WAKOSAJI. NAMI NINGEMJUA MKE WA HUYO MWANAUMME NAYE APEWE CD
 
Huyo rafiki yako nae alie kuonyesha kwenye CCTV ulimuajiri kukupa udaku wa mambo ya watu au aliambiwa aangalie mengine? yani ji roho lake linamuuma kisa jamaa hachukue uamuzi loh, ebu muacheni hamjui wenyewe wanaelewana vp.
 
Huyo nae ni rafiki yetu kitendo hicho kilimkwaza ndio maana akaniambia.
 
Sasa kweli mlitaka akaangalie mkewe anavyokamuliwa???
Mko serious? Unajua EGO ya mwanamme? Mnataka kumuua?

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mke na kimada
Angekuwa kimada angeenda kuangalia.
 
Rizt mkuu kwenye lift ni muda mchache sana mtu anakaa, sasa hiyo shemeji yetu hana aibu kiasi hicho?!!!!!
 
Unataka ushauri gani sasa? Wa kuongeza cctv cameras kwenye lift ama na wewe unataka uombe kwa shemejio?
Wanabodi JF.

Mie sio mwenyeji sana huku nimeona nije nipate michango yenu kutoka kwenu wadau wa MMU.
 
Back
Top Bottom