Nimeshindwa Kuvumilia naombeni msaada wenu wa haraka nimuokoe huyu Mtoto kwa Mama wa Kambo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,177
Baba yake Mzazi ni Rafiki yangu mkubwa sana tu na tunaheshimiana halafu hata Kiumri ni kama Mdogo wangu ila tatizo ni kwamba Mwanamke wake wa sasa sijui keshamroga au hapana kwani ( Jamaa ) hapindui kwa huyo Mwanamke ( yaani Mkewe )

Sasa ni mwezi wa tatu unakatika tokea huyu Mtoto atoke kwa Mama yake na kuja kuishi na Baba yake ambaye ni Jirani yangu ila tokea aje / ahamie kwa Baba yake na kukutana na Mama yake wa Kambo ambaye pia ana Mtoto wake wa Kike sijawahi kuona siku yoyote ile huyu Mtoto akakosa ' Kupigwa ' na ' Kunyanyasika ' na huyu Mama yake wa Kambo anayeishi nae sasa.

GENTAMYCINE huwa nina huruma mno na uchungu na niliamua kuvumilia kunyamaza sasa naona yamenifika shingoni hivyo natafuta namna ya kumwambia Baba yake kuwa Mwanae anateswa na kupigwa mno na Mkewe tena kuna muda bila hata sababu za msingi.

Ila changamoto kubwa Kwangu ni jinsi tu ya kumuingia huyu Baba yake na aniamini kwani kwa huyu Mkewe Jamaa hapindui kabisa hivyo nimekimbilia Kwenu humu muweze kunisaidia kusudi nimuokoe huyu Mtoto kwani kwa dalili ambazo naziona kwa ' mateso ' anayoyapata huyu Mtoto kuna Siku Turubai la Msiba litawekwa pale Kwao na kwenda Kumzika huyu Mtoto wa Watu.

Je nifanyeje? Nimvae huyu Mama Yeye kama Yeye nimpe ' makavu ' yake au nimwambie Baba Mtoto ambaye kuna kila dalili ' Limbwata ' limeshamkolea au nijenge Urafiki wa Kimkakati na huyu Mtoto nimfundishe ' Ujeuri ' na ' Ubabe ' ili awe anamdindia Mama yake na ikibidi awe anampiga hata na Matofa / Mawe?

Dada zangu Wapendwa ( Wanawake ) mtanisamehe ila mna roho mbaya sana. Badilikeni tafadhali. Hivi mnawezaje kumchukia Mtoto wa Mwanamke mwenzako ambaye na Yeye pia aliutumikia ' Mkuyenge ' vilivyo kama ulivyoutumikia Wewe na akajifungua kama ulivyojifungua Wewe?

Najua wengi wenu humu mmeshazoea kuwa GENTAMYCINE ni Mtu wa Utani ila kwa hili nisiwaficheni limeniumiza na limenikera mno na hadi hasira kunipanda na natamani hata siku moja huyu Mama akosee tu anijibu hovyo ili nimpe ' Kipondo ' cha kulipizia Hasira zangu Kwake kwa jinsi anavyomtesa huyu Mtoto wa Watu. Imeniuma sana!

Nawasilisha.
 
No tafuta ushahidi wa kutosha kwanza angalau mue wawili kwani unaweza kukurupuka akakwambia unataka kuharibu ndoa yake.au hata akamwambia mkewe kuhusu hilo swala na aka kutaja hapo ni ugomvi.

Fanya uchunguzi kisha peleka mada ukiwa hata na mwenye kiti wako wa mtaa na sio peke yako.

Unaweza ukaenda mwenyewe Mara shilawadu!! Waka kunyapia that's all
 
Genta chukua ka video, hata ka sauti tu. Kama huwezi ajiri kijana akufanyie kazi ya ku-shilawadu ukishapata ushahidi huna haja ya kuongea unamwonyesha muhusika. Watoto wanapata shida sana na baadhi ya wamama wa kambo.

Tatizo Simu yangu yenyewe ni ya Tochi halafu pia huwa haikai na Chaji na katika Vipindi vya mvua kama hivi huwa inazima sana.
 
Kwanini haumtetei akiwa ananyanyasika.. as unaonyesha mnaishi kwa nyumba moja labda vyumba tofauti?

Tatizo siyo kumtetea kinachonipa wakati mgumu ni kwamba Baba yake hapindui kwa huyu Mama kwa lolote hivyo nahitaji umakini mkubwa katika kumsaidia huyu Mtoto. Jamani huyu Mtoto anapigwa hadi huruma na kuna Siku zingine akiwa anapigwa hadi maumivu yake na Mimi nayapata na naungana nae katika Kulia japo Mimi huwa nalilia tu Chumbani Kwangu dirishani ili nami ' nisichoreke ' hadharani kwa Kulia kama Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda. Ila huwa nalia nae!

Sijui nifanyeje ili niweze kumuokoa huyu ' Dogo ' hakyanani. Jamani naombeni msaada Wenu kwani linalomtokea huyu Mtoto linaweza pia kukutokea Wewe kwa Mwanao hivyo tusaidiane katika kupatikana kwa ufumbuzi wake ili likomeshwe Tanzania nzima.

Nilikuwa nasikia tu kuwa Mama wa Kambo wengi ni Baghdad ( wana roho mbaya na makatili ) nikawa nakataa na siamini ila kwa hiki ninachokiona sasa nimethibitisha rasmi. Hivi nyie Wanawake hizi roho mbaya mmerithi labda kwa ' Malaika ' gani kutoka kule Mbinguni kwa Mungu Baba?
 
Ila changamoto kubwa Kwangu ni jinsi tu ya kumuingia huyu Baba yake na aniamini kwani kwa huyu Mkewe Jamaa hapindui kabisa hivyo nimekimbilia Kwenu humu muweze kunisaidia kusudi nimuokoe huyu Mtoto kwani kwa dalili ambazo naziona kwa ' mateso ' anayoyapata huyu Mtoto kuna Siku Turubai la Msiba litawekwa pale Kwao na kwenda Kumzika huyu Mtoto wa Watu.

Hujui jinsi ya kumwambia rafiki yako juu ya mtoto wake anayeteswa, na unaogopa anaweza asikuamini? Unaonyesa dalili za kuwa na ukaribu sana na huyo mkewe na hivyo atahisi unataka kuanzisha visa ili watengane.

Ukishindwa kumwambia (kitu ambacho nakushangaa na kukuona una weakness fulani) basi nenda kawaambie Ustawi wa jamii.
 
Ukimwambia baba mtu utaonekana wewe mgombanishi na mzindiki.

Kama walivyosema wadau wengine jaribu kukusanya ushahid hata wa video ili uweze kujitetea baadae.

Mama wa kambo mmoja kati ya 10000 ndio anaweza kaa na mtoto wa mwanamke mwenzie vizuri.
 
Back
Top Bottom