Nimeshikwa pabaya - wakuu naomba msaada tutani!

Ni kweli ukisoma alichoandika kwenye utangulizi na mkasa wenyewe haviendani. Rafiki yako kabisaaaaaaaaaaa, mmesoma tangu primary hadi UDSM, umemsaidia mkewe kapata masters huko majuu tena kwa gharama zako. Halafu leo hii mkewe tu aseme umemtongoza tu na yeye aahidi kukuchinja? No! Hii ni stori ya kutunga.

Kwa upande mwingine ukiamini kuwa ni kweli, ndiyo maana wengine tunaona kuwa huyu jamaa ni hovyo kabisa, limbukeni wa mapenzi...ni kiazi kweli kweli!
 
Wandugu wote mliochangia, nawashukuru sana kwa ujumla wenu, naendelea kukaribisha ushauri huku nikifanyia kazi ambao nimeshapewa, offcourse as usual .........za kuambiwa....mix with yours! Nami nitachang'anya na zangu kupata ufumbuzi wa hili. Wana JF, nitawajuza kitakachoendelea.
kama unataka ushauri wangu kisha uumbayuwayu ni hivi,
tafuta kamera swaaafi kisha fanya mpango wa kuwanasa ktk mikao mibovu ya hasara kisha tandika foto kadhaa kwa siku tofauti tofauti then mtumie mbwiga mwenye mke ili afure zaidi. wewe usiongee neno just tuma picha maana huwa zinaongea kuliko maneno.
 
Huyo jamaa yako kama hataki kuelewa, na wewe mchimbe mkwara aache kukutishia maisha

...No no, no!
Hiyo itamaanisha kuna kaukweli amemind 'kupigwa kibuti!.'
Asubirie tu 'siku ya kilio,' kumkumbushia rafiki yake; "nilikwambia hukuniamini!"
 
kama unataka ushauri wangu kisha uumbayuwayu ni hivi,
tafuta kamera swaaafi kisha fanya mpango wa kuwanasa ktk mikao mibovu ya hasara kisha tandika foto kadhaa kwa siku tofauti tofauti then mtumie mbwiga mwenye mke ili afure zaidi. wewe usiongee neno just tuma picha maana huwa zinaongea kuliko maneno.

...ebana wee,..yanini unamshawishi huyu jamaa 'hobby' ya ukozimeni bana?

Yaliyompata yeshamtosha. Keshasema yupo ughaibuni, na winter ndio ishaanza sasa,
Unataka apate pneumonia bure kwa kunyatia na kuchungulia vidirishani mwa watu?

Atakuja sutwa bure mwenzenu. Jamaa mshamsikia, anaweza pata picha na still akasema
ni photoshop sijui nini!...
 
Ni kitu rahisi sana kwani ukigusana na mwenzio sehemu yoyote ya mwili basi wewe huacha DNA zako sehemu hiyo na hazipotei asilani,

Uses of DNA in Criminal Investigations:

1. Identifying remains
2. Provides a Record of a particular person
being in a particular place
3. Ownership of personal items such as clothing
4. Determining Kinship
Thanks for the knowledge!:smow:
 
Na hili ndilo mshikaji (rafiki yangu) analong'ang'ania kuwa kama nilijua kwanini sikutangulia kumwambia. Ukweli ni kwamba sikutaka kukurupuka katika kumtaarifu jamaa hasa ukizingatia najua kuwa anamppenda sana mkewe.
Ulikuwa sawa pia kwani wakati mwingine si vizuri kukurupuka,never regret
 
Ni kweli ukisoma alichoandika kwenye utangulizi na mkasa wenyewe haviendani. Rafiki yako kabisaaaaaaaaaaa, mmesoma tangu primary hadi UDSM, umemsaidia mkewe kapata masters huko majuu tena kwa gharama zako. Halafu leo hii mkewe tu aseme umemtongoza tu na yeye aahidi kukuchinja? No! Hii ni stori ya kutunga.

Duuh, samahani sana kaka kama hukunipata vizuri pengine sikuwa clear. Lakini kilichopo ni kwamba huyu shemeji yangu ametumia "defensive mechanism", yaani kutangulia kuripoti kuwa nimemtongoza ili in case mimi nikimripoti yeye kuwa ana-cheat, nionekane muongo, na kwa hilo amefanikiwa. Nashukuru wachangiaji wengi walinielewa hivyo. Hata hivyo nashukuru kwa mchango wako.

Halafu siyo kwamba niligharamia safari yake yote ya kuja hapa isipokuwa katika pilikapilika za kumsaidia niliingia gharama fulani, naona mkuu hiyo umeikolezea sana.
 
hapo kazi ipo, kama jamaa anaweza pata vekeshen ya kuja huko, japo ya muda mfupi tu! aje na afikie kwako na bila kumtaarifu mkewe angalau ajionee mwenyewe kinachoendelea, indekusaidia zaidi, pole sana mkuu.
 
Bora uyo mama ana megwa a uyo jamaa ,kuliko angekaa Bongo angemegwa na mapredejee na kukamata ngoma ingawa ngoma iko kote.
Hivi kwa nini unapoteza muda na kujistress na huyo mlupo? kama amemegwa huko ulaya inawezekana alisha kua ana megwa hata huko TZ nadhani ni vizuri wamesha tengana bila kujijua ,sababu wanaishi nchi tofauti ni vizuri utumie njia za busara kumfahamisha huyo rafiki yako ( haswa ukiwa na ushahidi wa uhakika ) kama mkewe amewekwa kinyumba na jamaa huko mamtoni. Hapo huyo rafiki yako ataamua kubeba mlupo au kuachana naye.
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokukuta.
Nakushauri kama kama inawezekana jaribu kuongea na rafiki yako tena kwa upya kuhusu ishu hiyo.Usimchukie coz hata ungekuwa wewe lazima ungepata mshtuko fulani though sio lazima kwamba unge-react kama yeye,ila lazima hiyo kitu ingekustua!Jaribu kadri uwezavyo kumueleza kuwa kama anaweza aje huko ulipo pasipo mke wake kujua ili aje ajionee mwenyewe yanayoendelea na kwamba wife kashahama hostel kabisa.
Na alifanya hivyo kama njia ya kujilinda tu ili pindi ukimweleza asikuamini kwa lolote.Stick on that uone rafiki yako atachukua hatua gani.All in all just try to ease yourself ili hii ishu isije kukuletea BP bure ndugu yangu....asipokuelewa achana naye.
 
Dem kakuwahi huyo.inabidi upate hard evidence za kujikinga au vipi ukirudi bongo jamaa akupige kisu cha KANYUNGU !!!!
 
hapo kazi ipo, kama jamaa anaweza pata vekeshen ya kuja huko, japo ya muda mfupi tu! aje na afikie kwako na bila kumtaarifu mkewe angalau ajionee mwenyewe kinachoendelea, indekusaidia zaidi, pole sana mkuu.

...enyi watu hamkubali ukweli 'sikio la kufa halisikii dawa!' ???
keshasema hataki kuambiwa upuuzi huo kuhusu mkewe!
Mpaka amuue Deodat ndio mtaamini huyu bwana 'kazidiwa?'
 
Mimi niko hapa ughaibuni (nchi kapuni - for security reasons), kama wengi mnavyojua mara nyingi ukiwa huku nje ndugu, jamaa na marafiki kule nyumbani bongo huwa wanaomba kila siku ‘uwavute’ nao waje huku (bila kujali si rahisi kihivyo). Mwaka jana rafiki yangu kipenzi (tumesoma pamoja tangu shule ya msingi mpaka chuo kikuu pale mlimani) aliniomba nimsaidie kumfanyia mpango mkewe aje hapa kufanya masters degree, nilijitahidi kwa nguvu zangu zote hata kuingia gharama nyingi na hatimaye shemeji yangu kipenzi akafika hapa.

Hapa tulipo sio mji mkubwa sana, una watu elfu 25 tu na watanzania tuko wachache sana na tunafahamiana kwa kiasi kikubwa. Mara nyingi huwa tunakutana na kupiga soga, kunywa na kula pamoja huku tukikumbushana haya na yale hasa kuhusu nyumbani. Hatuna chama rasmi cha watanzania lakini tunashirikiana vizuri sana na tumekubaliana hatutaanzisha chama kwakuwa mara nyingi mkishakuwa na vyama ndio majungu na ufisadi vinaanza na pia tumekubaliana hatutafungua tawi la nje la chama cha siasa (hasa CCM) labda Chadema tutafikiria.

Stori iko hivi: Katika sisi watanzania tulio hapa kuna jamaa mmoja yeye ni mkongwe hapa, ameeishi kwa miaka saba sasa, ameajiriwa na kitengo kimoja cha serikali kama Strategic Analyst (ana pesa nzuri tu) na ni mtu mkarimu sana kiasi kila mtanzania anayefika hapa huwa anamu-appreciate sana jamaa. Huyu jamaa hana mke, sasa shemeji yangu alipofika nilimtambulisha kwa watanzania wengine akiwepo huyu jamaa, wakazoeana sana, siku za mwanzo nilijua ni kawaida tu lakini baadae niligundua wameanza mahusiano, na kwa hivi sasa napoongea shemeji keshahama hostel anaishi kwa jamaa, wanapika na kupakua.

Hicho kitu kimeniumiza sana hasa ukifikiria ni mke wa rafiki yangu. Kwasababu alijua anachokifanya, shemeji sasa ananionea aibu sana kiasi kwamba hata nikimpigia simu hapokei. Wakati naendelea kutafakari nini cha kufanya, nikapokea simu kutoka kwa huyo rafiki yangu (mwenye mke) akinituhumu kuwa mkewe kampigia simu kuwa mimi nimemtongoza na nataka niwe na mahusiano naye kimapenzi, kwakuwa jamaa anamuamini sana mkewe na anampenda mno, amefedheheshwa sana na taarifa hizo hasa ukizingatia sisi ni marafiki wa siku nyingi, jamaa ameapa ‘kunichinja’ siku tukionana. Nimejaribu kumuelewesha jamaa haelewi.

Wandugu nifanyeje?

(Samahani sana kwa kuweka stori ndeeeefu lakini ilibidi nifanye hivi ili issue iwe clear kidogo)

Usirudi Bongo.

Kwanza huku njaa tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom