Nimeshikwa pabaya - wakuu naomba msaada tutani!

huo mji hakuna mswahili anaejuana na huyu rafiki yako huku akakusaidia kuelezea hii ishu vizuri, najua frnd wako kwa sasa ana hacra sana na wewe lakini angepata mtu tofauti na wewe kumwelezea haya mambo na kumpa ukweli wenyewe nadhani akili yake ingefikiri mara mbili.

Asante sana, naona hii ina-click!
 
Hili nalifanyia kazi, nataka ni-establish evidence beyond doubt! Thanks!
If I were u i would cut them loose. Elekeza nguvu zako kwenye mambo ya maana yaliyokuleta huko. Wabongo mi nawajua, so much drama na wanaeza kukuharibia huko nchi za watu ukakosa mwana na maji ya moto ukakandwa.
 
Wandugu wote mliochangia, nawashukuru sana kwa ujumla wenu, naendelea kukaribisha ushauri huku nikifanyia kazi ambao nimeshapewa, offcourse as usual .........za kuambiwa....mix with yours! Nami nitachang'anya na zangu kupata ufumbuzi wa hili. Wana JF, nitawajuza kitakachoendelea.
 
Wandugu wote mliochangia, nawashukuru sana kwa ujumla wenu, naendelea kukaribisha ushauri huku nikifanyia kazi ambao nimeshapewa, offcourse as usual .........za kuambiwa....mix with yours! Nami nitachang'anya na zangu kupata ufumbuzi wa hili. Wana JF, nitawajuza kitakachoendelea.


haya Deodat
 
...hivi sasa napoongea shemeji keshahama hostel anaishi kwa jamaa, wanapika na kupakua.

Hicho kitu kimeniumiza sana hasa ukifikiria ni mke wa rafiki yangu. Kwasababu alijua anachokifanya, shemeji sasa ananionea aibu sana kiasi kwamba hata nikimpigia simu hapokei. Wakati naendelea kutafakari nini cha kufanya, nikapokea simu kutoka kwa huyo rafiki yangu (mwenye mke) akinituhumu kuwa mkewe kampigia simu kuwa mimi nimemtongoza na nataka niwe na mahusiano naye kimapenzi, kwakuwa jamaa anamuamini sana mkewe na anampenda mno, amefedheheshwa sana na taarifa hizo hasa ukizingatia sisi ni marafiki wa siku nyingi, jamaa ameapa ‘kunichinja’ siku tukionana. Nimejaribu kumuelewesha jamaa haelewi.

Wandugu nifanyeje?

(Samahani sana kwa kuweka stori ndeeeefu lakini ilibidi nifanye hivi ili issue iwe clear kidogo)

...wote wawili hawana maana. Achana nao na huo mtindo wa maisha yao.
Mind your own business!
 
kesi yako complicated kweli.. pole sana.. chakufanya mwambie ukweli tu huyo rafiki yako akikataa tafuta camera piga picha ya huyo shem wako wakiwa na huyo jamaa.. mtumie rafiki yako kazi iwe kwake.. alale ama aoshe vyombo alale
 
Ni kitu rahisi sana kwani ukigusana na mwenzio sehemu yoyote ya mwili basi wewe huacha DNA zako sehemu hiyo na hazipotei asilani,

Uses of DNA in Criminal Investigations:

1. Identifying remains
2. Provides a Record of a particular person
being in a particular place
3. Ownership of personal items such as clothing
4. Determining Kinship

...asilani? si kweli.
 
Ni kitu rahisi sana kwani ukigusana na mwenzio sehemu yoyote ya mwili basi wewe huacha DNA zako sehemu hiyo na hazipotei asilani,

Uses of DNA in Criminal Investigations:

1. Identifying remains
2. Provides a Record of a particular person
being in a particular place
3. Ownership of personal items such as clothing
4. Determining Kinship


Ni kweli DNA inatumika kwenye uchunguzi wa mambo ya uhalifu (criminal and forensics) ila tatizo langu ni nyweie za mtu kubaki kwa mwenzake kama vile zimepandwa. Hii haina ukweli wowote, labda kama kitendo kimefanyika muda si mrefu. Hata hivyo kiwango cha DNA kwenye nywele siyo kingi zaidi kama kama kile kinachoweza kupatika katika maji maji yanayokutwa sehemu za siri. Hilo suala la nywele kugandamana kwenye mwili halipo kabisa. Kama una ushahidi wa kisayansi, basi tupatie.
 
kesi yako complicated kweli.. pole sana.. chakufanya mwambie ukweli tu huyo rafiki yako akikataa tafuta camera piga picha ya huyo shem wako wakiwa na huyo jamaa.. mtumie rafiki yako kazi iwe kwake.. alale ama aoshe vyombo alale

Huyo mshikaji wake inaonekana ni mpuuzi. Hata akitumiwa picha nadhani hataamini. Dawa ni kumwacha ili aje ayajue mwenyewe. Kitendo cha kuamibiwa na mke kwamba rafiki yake anamtogoza kilitakiwa tu kimpe hints. He is a loser!
 
ebanaeeee!!!! pole sana kwa yanayokusibu ndugu, ushauri wangu kwako ni kwamba usicomplicate maisha we kama ushamwambia akaona unamzingua, mpotezee we kula buyu tu haina haja ya kumbembeleza akuamini, wacha mazoea na huyo shemejiyo aso na haya wala soni.
ilimradi ushamfikishia ujumbe, u move on with your life.
 
Kwani mkuu huwezi fanya upaparazi ukawapiga hata picha kadhaa wakiwa maeneo yao tofauti ya kujidai halafu ukamtumia huyo jamaa yake ajithibitishie mwenyewe!!
 
Kwani mkuu huwezi fanya upaparazi ukawapiga hata picha kadhaa wakiwa maeneo yao tofauti ya kujidai halafu ukamtumia huyo jamaa yake ajithibitishie mwenyewe!!

...hapana bana, hiyo ni tabia mbaya sana.
Nadhani ndio inaitwa umbea hiyo.
 
Huyo mshikaji wake inaonekana ni mpuuzi

Uko sahihi kwa hilo, manake asivyotaka kuelewa ukweli, yaani mpaka ananishangaza kama ile degree aliyopata pale mlimani ilikuwa ni chetu au la.
 
pole kaka,just hire a private investigator.then mtumie rafiki yako hizo picha na ripoti ya upelelzi
 
Uko sahihi kwa hilo, manake asivyotaka kuelewa ukweli, yaani mpaka ananishangaza kama ile degree aliyopata pale mlimani ilikuwa ni chetu au la.[/QUOTE]

Taratibu ndugu yangu. Kwenye mambo ya unyumba hakuna degreee, diploma au form 7. Wote sawa, ni uchizi kwa kwenda mbele.

Hata hivyo busara inatakiwa kuwepo kila mahali bila kujali elimu ya darasani. Ndio maana naamini huyu mshikaji wako ni kiazi fulani katika haya mambo ya unyumba. Kwani angemwambia Mama yake anamtongoza (assume ni lesbian) angekubali? We nyamaza tu, kuna siku atakuja kwako analia machozi kama toto lilivimbia!
 
Deodat;
Unless story ni ya kutunga, it is very touching!
Ningekushauri pia kisirisiri umpe rafiki yako contacts za simu za watanzania wawili au watatu ; najua sababu shemeji yako, mume wake hayupo kule, watakuwa wameshaji-expose ki-aina to the extent ambayo nina shaka kama kuna mtanzania yeyote asiyejua nini kinaendelea kati ya wawili hao. Awapigie simu na watamweleza aelewe. Hasa ungejaribu kutumia wale wa kike, hasa wale walioko kwenye maisha ya ndoa na wanaishi na waume zao huko

Ni kweli ukisoma alichoandika kwenye utangulizi na mkasa wenyewe haviendani. Rafiki yako kabisaaaaaaaaaaa, mmesoma tangu primary hadi UDSM, umemsaidia mkewe kapata masters huko majuu tena kwa gharama zako. Halafu leo hii mkewe tu aseme umemtongoza tu na yeye aahidi kukuchinja? No! Hii ni stori ya kutunga.
 
Back
Top Bottom