Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,282
- 105,490
Mkuu Kiranga taratibu mkuu nilikuwa natoa mfano si kwamba nilikuwa na hakiki hoja samahani kama nimekukwaza. Inawezekana kuna mambo mengi tu yamemfanya arudi mjini lakini kwa ufupi maisha lazima yaendelee.
Maisha lazima yaendelee, lakini si lazima yaendelee mjini tu, hususan kwa watu waliotoka kujinadi kama wadau wakubwa wa maendeleo ya watu wa majimbo ya vijijini.
Wabunge wote pamoja na wadau wengine wanaojinadi kuwa au kutaka kuwawakilisha wananchi wa majimbo ya vijijini inawabidi wawe wakazi wa huko huko vijijini, sio mnawapelekea wananchi wagombea ubunge watalii ambao hata wananchi hawawajui. Na wakishindwa uchaguzi wiki moja tu wanakitoa "kurudi" mjini kwenye viyoyozi wakisubiria uchaguzi ujao.