Nimerudi salama-Niliwamiss sana

Status
Not open for further replies.
hivi inakuwaje kura zinashindwa kuibiwa Ubungo na Kawe lakini zinaibiwa kwenye majimbo mengine?

(Asprin, kama masuala ya aina hii pia hayatakiwi kwenye hii thread naomba kufahamishwa)
 
Kiranga nakubaliana na hoja zako ila nina wasiwasi unapost mfululizo kumyima Regia aituhabarishe kilichojiri huko jimboni Kilombero au umetumwa na mafisadi nini?

No you didn't.

You see this is the very same narowmindedness hoodwinked and railroaded on that one trackmindedness of "if you don't sing praises for Regia then you must be with the fisadis".

Ukweli ni kwamba, huhitaji kutumwa na mafisadi kuona kwamba Regia ana upeo mdogo. Na ukweli kwamba tuna kiu ya mabadiliko usitufanye tuwe desperate kiasi cha kutokubali ukweli kwamba wapinzani wetu hawakujiandaa vilivyo na waliweka wagombea dhaifu kama kina Regia. Mgombea hajui hata katiba inasemaje kuhusu some basic constitutional parts on the presidency ?

Halafu kiu yako ya kutaka kujua nini kilitokea Kilombero isikutake kuamini kila kitu atakachosema Regia hapa, hata kama atakuja kukujibu.
 
hivi inakuwaje kura zinashindwa kuibiwa Ubungo na Kawe lakini zinaibiwa kwenye majimbo mengine?

(Asprin, kama masuala ya aina hii pia hayatakiwi kwenye hii thread naomba kufahamishwa)

inawezekana kabisa hususan ktk jitihada za kutengeneza perception za kujengea hoja kama hiyo ya msingi wa swali lako maana kila mara wapenda haki tutakapolalama mtanyoosha vidole na kusema mbona mnyika na sugu wameshinda as if ushindi wao unamaanisha hakukuwa na vote rigging
 
karibu sana dada regia na pole kwa yote ,vuta subra iko siku mambo yatanyooka na shanira yako ya kuwatumikia wana kilombero na taifa kwa jumla itatimia.hata my wife alianguka lakini nafikiri ni muda wa kukaa chini na kutafakari upya.
 
inawezekana kabisa hususan ktk jitihada za kutengeneza perception za kujengea hoja kama hiyo ya msingi wa swali lako maana kila mara wapenda haki tutakapolalama mtanyoosha vidole na kusema mbona mnyika na sugu wameshinda

badala ya kutafuta kiini cha tatizo na kujua kwa nini mkakati wa kuzuwia kura zisiibiwe ulifanikiwa ubungo na na kushindwa katika majimbo mengine imekuwa muuliza suali miongoni mwa watakaonyoosha vidole kupinga wapenda haki.

kazi kweli kweli.
 
Regia welkum back pole na masahibu yote uliyokutana nayo huko najua, Mungu na bado ataendelea kukuzidisha na kukubariki all the best na karibu tena kwenye jukwaa letu la MM
 
hivi inakuwaje kura zinashindwa kuibiwa Ubungo na Kawe lakini zinaibiwa kwenye majimbo mengine?

(Asprin, kama masuala ya aina hii pia hayatakiwi kwenye hii thread naomba kufahamishwa)

Ubungo na Kawe jua limeshachwea wakati Kilombero na kwingineko ndio kunapambazuka.
 
Niseme haya machache. Mpaka sasa regia hajasema mipango yake ya baadaye ni ipi - kama atagombea tena au la. Na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja ambaye kamuuliza kuhusiana na mustakabali wa mipango yake ya baadaye. Katamka "karudi" ndiyo imekuwa nongwa hadi kupelekea kuitwa "mamluki". Ni kama vile regia hana haki ya kupumzika baada ya mikikimikiki ya kampeni. Kibaya zaidi hakuna ambaye kamuuliza kuhusu mipango yake ya baadaye (ya kisiasa). Vipi kama keshaamua kuwa siasa yeye basi? Aendelee kukaa tu kilombero? Wakati mwingine ni vizuri kuuliza kwanza kuliko kusadiki na/au kutoa hukumu haraka haraka
 
Mkuu Kiranga, unaonekana una kitu personal na dada Regia. Ushauri wangu kwa dada regia ni kuhakikisha kuwa anakuwa na ukaribu zaidi na wananchi wa Kilombero katika shughuli za maendeleo kwa kubuni miradi mbalimbali itakayosaidia kuondoa kero zao mbalimbali hasa maji na pengine kusaidia wasiojiweza kulipia karo/ada za shule watoto wao ili watoto wao watumie nafasi wanazopata katika kujiendeleza kielimu. Ukifanya hayo mawili nje ya ubunge na uhakika utaweka ukaribu zaidi na wananchi na mwaka 2015 god willing utarudi kwa kishindo kikuu. Mungu akubariki na akutie nguvu. Amen
 
Mkuu Kiranga, unaonekana una kitu personal na dada Regia.

Sishangai, ni kawaida yetu wabongo wengi kuchukulia kila kitu personal.

Ushauri wangu kwa dada regia ni kuhakikisha kuwa anakuwa na ukaribu zaidi na wananchi wa Kilombero katika shughuli za maendeleo kwa kubuni miradi mbalimbali itakayosaidia kuondoa kero zao mbalimbali hasa maji na pengine kusaidia wasiojiweza kulipia karo/ada za shule watoto wao ili watoto wao watumie nafasi wanazopata katika kujiendeleza kielimu. Ukifanya hayo mawili nje ya ubunge na uhakika utaweka ukaribu zaidi na wananchi na mwaka 2015 god willing utarudi kwa kishindo kikuu. Mungu akubariki na akutie nguvu. Amen

Sasa atakuwaje karibu na wananchi wa Kilombero kwa speed hii ya kuwakimbia wiki moja tu baada ya uchaguzi? I mean hata hakuwa na decency ya kukaa nao kidogo baada ya uchaguzi kuangalia maisha yao wajue alikuwa na interest beyond campaign za uchaguzi ?
 
kwa mujibu wa orodha ya Chadema ya viti maalum kwa wanawake iliyochapishwa magazetini, Regia yupo kwenye orodha kwenye nafasi za mwanzo mwanzo

labda ndio maana wengi hawajamuuliza kwa kuwa iko wazi kuwa ni mbunge wa viti maalum vya chadema.
 
badala ya kutafuta kiini cha tatizo na kujua kwa nini mkakati wa kuzuwia kura zisiibiwe ulifanikiwa ubungo na na kushindwa katika majimbo mengine imekuwa muuliza suali miongoni mwa watakaonyoosha vidole kupinga wapenda haki.

kazi kweli kweli.

basi jifunze namna ya kuunda na kuuliza maswali ili pindi unapouliza usionekane kama unatia shaka au usionekane upo upande fulani wa hoja. Msikiko wa sauti (tone) ni suala muhimu sana ktk mawasiliano. Kumbuka 'its not what you say but how you say it'
 
Niseme haya machache. Mpaka sasa regia hajasema mipango yake ya baadaye ni ipi - kama atagombea tena au la. Na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja ambaye kamuuliza kuhusiana na mustakabali wa mipango yake ya baadaye. Katamka "karudi" ndiyo imekuwa nongwa hadi kupelekea kuitwa "mamluki". Ni kama vile regia hana haki ya kupumzika baada ya mikikimikiki ya kampeni. Kibaya zaidi hakuna ambaye kamuuliza kuhusu mipango yake ya baadaye (ya kisiasa). Vipi kama keshaamua kuwa siasa yeye basi? Aendelee kukaa tu kilombero? Wakati mwingine ni vizuri kuuliza kwanza kuliko kusadiki na/au kutoa hukumu haraka haraka

Kupumzika baada ya kampeni ni lazima kuondoka Kilombero ? Kama mtu una haja ya ku represent kweli watu wa Kilombero unapumzika wanavyopumzika wao huko, unawajua vizuri.

Sio mtu unataka kuwawakilisha watu wa Kilombero mapumziko yako dunia tofauti na yao. Huu si umamluki ninaousema hapa?

Ukisema Regia kaamua kuja mjini kwa sababu kaamua siasa tena yeye basi utakuwa unakubali kwamba Regia alikuwa hana interest ya moyoni kusaidia maendeleo Kilombero, alikuwa anatafuta ajira tu na ukubwa sasa imeshindikana hana muda wa kupoteza huko bush.

Mtu mwenye nia ya kuleta maendeleo Kilombero hata akishindwa ubunge atatafuta namna nyingine ya kufanya kazi na watu wa huko, sio kuwakimbia wiki moja baada ya uchaguzi.
 
kwa mujibu wa orodha ya Chadema ya viti maalum kwa wanawake iliyochapishwa magazetini, Regia yupo kwenye orodha kwenye nafasi za mwanzo mwanzo

labda ndio maana wengi hawajamuuliza kwa kuwa iko wazi kuwa ni mbunge wa viti maalum vya chadema.

Haya yote nilishayatabiri kitambo, yanatimia sasa.
 
Niseme haya machache. Mpaka sasa regia hajasema mipango yake ya baadaye ni ipi - kama atagombea tena au la. Na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja ambaye kamuuliza kuhusiana na mustakabali wa mipango yake ya baadaye. Katamka "karudi" ndiyo imekuwa nongwa hadi kupelekea kuitwa "mamluki". Ni kama vile regia hana haki ya kupumzika baada ya mikikimikiki ya kampeni. Kibaya zaidi hakuna ambaye kamuuliza kuhusu mipango yake ya baadaye (ya kisiasa). Vipi kama keshaamua kuwa siasa yeye basi? Aendelee kukaa tu kilombero? Wakati mwingine ni vizuri kuuliza kwanza kuliko kusadiki na/au kutoa hukumu haraka haraka

Dude, leo umeamkia upande upi? Mpaka sasa umeshakamata tuzo kadhaa za wema na utu toka kwangu!
 
Wapwaz na Binamuz wote.

Ni matumaini yangu kuwa wote mko salama.Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wale wote kwa namna moja ama nyingine mmeshiriki kufanikisha uchaguzi wa mwaka hu popote pale mlipo kwa ngazi yoyote ile iwe udiwani,ubunge na hata urais,pongezi sana!!!.

Napenda kuwaambia kuwa nimerudi salama toka Kilombero,nimepambana kadiri ya uwezo wangu na kufika hapa nilipofika.namshukuru MUNGU niko salama kabisa na nitaendelea kuvinjari kwenye jukwaa letu pendwa la urafiki na mapenzi.

Nimewamiss si kidogo!!!Natafuta muda nionane na baadhi yenu.

With love
Regia

Pole lakini kabla ya yote mi sijaelewa mambo yaliyotokea
 
Sasa atakuwaje karibu na wananchi wa Kilombero kwa speed hii ya kuwakimbia wiki moja tu baada ya uchaguzi? I mean hata hakuwa na decency ya kukaa nao kidogo baada ya uchaguzi kuangalia maisha yao wajue alikuwa na interest beyond campaign za uchaguzi ?

mazee kwani unaijua ratiba ya regia? Kwani regia ndo alienda kilombero wakati wa uchaguzi tu na huko siku za nyuma na miaka ya nyuma alikuwa hajawahi kwenda? Au kakwambia ndo keshaondoka for good?
 
basi jifunze namna ya kuunda na kuuliza maswali ili pindi unapouliza usionekane kama unatia shaka au usionekane upo upande fulani wa hoja. Msikiko wa sauti (tone) ni suala muhimu sana ktk mawasiliano. Kumbuka 'its not what you say but how you say it'

bila ya shaka natia shaka ndo maana nikauliza suali. Natia shaka ya kwanini chadema ikaruhusu hali hiyo itokee.

msikiko wa sauti ni kwa mujibu wa akili yako ulivyoiweka, Asprin kasikia uzuri na akatoa jibu muafaka mbona.
 
karibu sana dear tulikumiss pia....pole na majukumu yaliyokuwa magumu lakini tunamshukuru Mungu umerudi salama
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom