Nimeponea chupuchupu kulipia kundi kwenye mtoko

Pole mkuu ila wanawake bwana wakitoka out wao kwa wao kila mmoja analipia matumizi yake nina amini kabisa ulivyoondoka kama waliendelea kuagiza wala msalaba haukuwa wa gf wako bali kila mmoja alilipa.

sent from kuzimu
 
Kwastaili hili kweli kupiga hatua nishida ,, MTU ushapoteza almost laki nzima na ushereee alafu bado unaona umejisaidia ???

Akili za mwanamme kweli anazijua mwenyewe.
 
Hayo yalinikuta majuzi safarini Karatu nilikapata kamchepuko tukapanga tuonane jioni kakaja na rafiki yake nikaona poa tu ila baadae wakaanza kupigiana cm anakuja mmoja baada ya mwingine... hamadi!! Wakafika watano huku wanakonyezana tu hapo nikacheka kimoyomoyo! hawanijui hawa mimi mtoto wa mjini hawanipati ng'o. Yakaliwa makuku hapo na mibia ya kila namna. Mimi nikaamka kama naongea na cm ndo imetoka hiyo hadi leo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo mbinu huwa naitumia sana.
 
65000 Kwel Kuna Watu Wanahela Na Hazina Kazi Ukienda U.s.a Mtu Akikualika Lunch Ujue Unajilipia Ok Ni Pesa Yako Una Amua Upendacho
 
Siku ya jana Jumapili nikiwa nimechill home ilikuwa ni mbaya na nzuri kwangu, Ilikuwa nzuri pale nilipopigiwa na "Mdaiwa Sugu" kwamba anataka kurusdisha pesa niliyomkopa january 400,000 taslimu na hivyo akatuma pamoja na ya kumvumilia akatuma 430,000, Nlifurahi sana na hapo ndipo nilipofanya uamuzi uliofanya siku yangu ya jana iwe mbaya, Nikapata wazo la kumtoa out g.f wangu hoteli moja ya matawi ya juu hapa Mbeya, Kwenye mahusiano yetu tumewekeana kwamba wiki hii akilipia outing mimi outing inayofata nalipia, So kwa vile wiki iliopita alilipia outing basi outing ya jana ilibidi nilipie.

Kitu cha kwanza nlimtumia 50,000 ili atoke mwake, then nikaweka bajeti ya 150,000 kwa ajili ya ,chakula vinywaji,chumba na mafuta ya gari. Imefika mida ya jioni saa kumi hivi nikaenda kutafuta hoteli iliotulia then nikamwambia aje, Nikiwa nasubiri nikaona sio mbaya nipooze koo kwa juisi baridi na baada ya dakika 10 akaniambia kafika so nikamuelekeza eneo nilipo.

Kufumba na kufumbua nikashudia kitu ambacho sikudhania kabisa, My girlfriend kaja na wezake watano, Nimemtoa g.f wangu mitoko kibao lakini ni mara moja tu aliwahi kumleta rafiki moja tu, Kimya kimya nikajisemea moyoni,"Mama yangu!!!, Nimekwisha", Sikuonesha usoni kwamba nimekasirika so nika smile kibish kibishi, Viti kwenye meza niliyopo vilikuwa viwili so ikabidi waiter atupeke sehem tuliyotosha watu 7, Treni likaanza kuchochea waiter akaanza kuleta menu list, Kimbembe kikaanza wote wakahitaji redbull mbilimbili, Hapo nikawazaga ule msemo "ukimpa panya glasi ya maziwa atataka na siagi", So nilichofanya nikamtumia rafiki yangu meseji anipigie simu ajifanye ni boss wangu kwamba ananihitaji, Nikamsave jina "Boss" NA alivyopigia simu nikajifabya nimekereka nikamwambia g.f. wangu aipokee yeye, so rafiki yangu akafanya kama nilivyomwambia so hapo ndipo nilipoponea chupu chupu nikawaaga nikalipia hela ya red bull tu na juisi yangu kwa 65,000 tu nikamwachia msimba g.f wangu nikasepa.

Kiukweli hii tabia ya kualika kundi kwa huu usawa ni mbaya sana na nikaona sina haja ya kulipiza kisasi kwa kuwaleta marafiki zangu outing ya wiki ijayo ambayo girl friend wangu atalipia bali nikamchana live kwamba kitu alichotaka kunifanya ni kibaya sana ambacho kingenitoboa wallet na asije kurudia tena kukifanya pindi nimtoapo out,
Huwa nawashangaa sana wadada wanaopenda kudandia outing za watu .

Hivi hawajui kwamba wanawavurugia mazungumzo ya faragha baina ya shost yao na BF wake.

Ifike pahala wabadilike kwa kweli maana wanapeperushiana bahati hivihivi ,kwa maana mtu mwingine anakuwa amepanga amfanyie kitu kikubwa sana mpenzi wake ila kwa kuwa huyo mwanamke kafanya uswahili kwa kitendo cha kuja na lundo la marafiki basi hapo jamaa ile hamu ya kumfanyia mpenzi wake hiyo ishu aliyoipanga inamtoka na mwingine anaghairi mazima na pia kuna uwezekano hata uhusiano ukaisha siku hiyo hiyo.
 
Siku ya jana Jumapili nikiwa nimechill home ilikuwa ni mbaya na nzuri kwangu, Ilikuwa nzuri pale nilipopigiwa na "Mdaiwa Sugu" kwamba anataka kurusdisha pesa niliyomkopa january 400,000 taslimu na hivyo akatuma pamoja na ya kumvumilia akatuma 430,000, Nlifurahi sana na hapo ndipo nilipofanya uamuzi uliofanya siku yangu ya jana iwe mbaya, Nikapata wazo la kumtoa out g.f wangu hoteli moja ya matawi ya juu hapa Mbeya, Kwenye mahusiano yetu tumewekeana kwamba wiki hii akilipia outing mimi outing inayofata nalipia, So kwa vile wiki iliopita alilipia outing basi outing ya jana ilibidi nilipie.

Kitu cha kwanza nlimtumia 50,000 ili atoke mwake, then nikaweka bajeti ya 150,000 kwa ajili ya ,chakula vinywaji,chumba na mafuta ya gari. Imefika mida ya jioni saa kumi hivi nikaenda kutafuta hoteli iliotulia then nikamwambia aje, Nikiwa nasubiri nikaona sio mbaya nipooze koo kwa juisi baridi na baada ya dakika 10 akaniambia kafika so nikamuelekeza eneo nilipo.

Kufumba na kufumbua nikashudia kitu ambacho sikudhania kabisa, My girlfriend kaja na wezake watano, Nimemtoa g.f wangu mitoko kibao lakini ni mara moja tu aliwahi kumleta rafiki moja tu, Kimya kimya nikajisemea moyoni,"Mama yangu!!!, Nimekwisha", Sikuonesha usoni kwamba nimekasirika so nika smile kibish kibishi, Viti kwenye meza niliyopo vilikuwa viwili so ikabidi waiter atupeke sehem tuliyotosha watu 7, Treni likaanza kuchochea waiter akaanza kuleta menu list, Kimbembe kikaanza wote wakahitaji redbull mbilimbili, Hapo nikawazaga ule msemo "ukimpa panya glasi ya maziwa atataka na siagi", So nilichofanya nikamtumia rafiki yangu meseji anipigie simu ajifanye ni boss wangu kwamba ananihitaji, Nikamsave jina "Boss" NA alivyopigia simu nikajifabya nimekereka nikamwambia g.f. wangu aipokee yeye, so rafiki yangu akafanya kama nilivyomwambia so hapo ndipo nilipoponea chupu chupu nikawaaga nikalipia hela ya red bull tu na juisi yangu kwa 65,000 tu nikamwachia msimba g.f wangu nikasepa.

Kiukweli hii tabia ya kualika kundi kwa huu usawa ni mbaya sana na nikaona sina haja ya kulipiza kisasi kwa kuwaleta marafiki zangu outing ya wiki ijayo ambayo girl friend wangu atalipia bali nikamchana live kwamba kitu alichotaka kunifanya ni kibaya sana ambacho kingenitoboa wallet na asije kurudia tena kukifanya pindi nimtoapo out,

NO; 1: HAKUNA MTU MWENYE AKILI TIMAMU ANAYEWEZA KUAGIZA REDBUL 2.
 
Mm ukiniletea timu, ndio hapo utakapojua kuwa kujibebisha nilikuwa kwenye bongo movie huta amini nitakacho fanya, huu ujinga nilisha sema sita kaa niuendekeze, yaani nikualike ww then unaleta timu.

Embu wadada semeni huwa mnawazaga nini kufanya huu utumbo.

driller⛏⚒
 
Brother huyo sio girlfriend bali huyo ni mpigaji. Let me guess, anasoma kile chuo kipo pale juu sio karibu na ile club maarufu sio? Mimi hiyo ilinitokea Dodoma mwaka jana nimeenda kubeba babes Udom wakashuka 6. Nikasema poa. Nikawapeleka kwenye pizza kwa muitaliano kule Area D. Wakala wakanywa nikawarudisha. Ila watatu walilipa fadhila kwa namna yao. Yule aliyekuwa ni "wangu" alipogundua akamind. Nikamwambia uliniona buzi, imekula kwako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom