Nimepata kazi ya mkataba ila nilikuwa na uhitaji wa kazi ya kudumu

Ukiacha hiyo ta mkataba hata hizo unataka utakosa utasugua benchi mpaka pumbu zichakae😁
Shida pia ni umri! Hapo Mungu alishachungulia kwenye mkeka wa Mama akaona kijana atoboe ngoja ambless kwenye mikataba ndio atajipata sasa yeye analeta ujuaji na utoto mwingi as if ni mtoto wa dada yake Mama Kizimkazi so sad na inatia hasira 😭😭😭😭😭😭
 
Una akili kweli wewe??aliyekuhakikishia zinatangazwa mwezi ujao ni nani? huko Vyuoni maendaga kusomea nini?
Halafu muulize kwenye hizo ajira za kudumu ni lini walipata wote au yeye ni mtoto wa Mama Samia au Waziri wa Tamisemi?
 
Shida pia ni umri! Hapo Mungu alishachungulia kwenye mkeka wa Mama akaona kijana atoboe ngoja ambless kwenye mikataba ndio atajipata sasa yeye analeta ujuaji na utoto mwingi as if ni mtoto wa dada yake Mama Kizimkazi so sad na inatia hasira
Hata miaka 30 sijafika.
 
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba humu jamvini kunawatu wako kwenye mifumo ya ajira za serikali wanajua wanachokushauri nenda karipoti ,Fanya kazi Kwa uadilifu mkubwa kajitume utaonekana tu na utapata kazi ya kudumu inshallah.lakin chamsingi mshahara wako jibane sana achana na starehe.ndani ya miaka miwili utakuwa umejipatia mtaji Ili upate kiofisi chakujishikiza Huku mapambano yakiendelea yakutafuta kazi.
Ahsante japo Halmashauri
 
Habari wana jf.

Mimi ni kijana niliyekuwa nahangaika kutafuta ajira serikalini kwa muda mrefu kidogo.

Juzi ijumaa Tamisemi wametoa majina ya ajira ila kwa muundo wa mkataba na jina langu likiwemo.
Ila imeniletea ukakasi hii hali naombeni ushauri wenu wakuu.

Ajira wanasema ni ya mkataba wa miaka miwili na utapata shtahiki zote za mtumishi wa umma na majina yametolewa na Tamisemi wenyewe.

Mimi nataka niipotezee maana kuna kibali cha ajira Mama Samia alishakitoa mwaka jana Nadhani mwaka huu wanatangaza watumishi elfu 23.

Hofu yangu

Kama nikienda kuripoti nadhani sitapata tena ajira za tamisemi zinazotoka mwezi ujao maana Database yao itaonesha nimepata kazi.
View attachment 2886023
Acha mambo yako, chukua kidogo hicho wakati unasubiria kikubwa,kilicho mkononi ndio chako ,kisicho mkononi sii chako hadi kiwepo mkononi mwako🤔.Eboo
 
Wazo zuri yeye anawaza la kesho badala achangamkie fulsa .anauhakika Gani kama hao elf 23 na yeye ataapia Malaki Hawana ajira yeye kapata ya mkataba anaanza maringo tena sasa asiripoti asubir kibali Cha mama
Ajira ya kudumu ina utamu wake unafanya Longterm plan.
 
Tusio na ajira na hatujui Ni lini tutapata ajira, tunakuangalia kwa jicho Kali Sana...tunatamani tukutukane Ila Sheria za jukwaa hazirihusu.
Acha basi mi nikushauri kwa kuzingatia Sheria za jamiiforum.

Nakushauri nenda kafanye kazi.. miaka miwili Ni mingi Sana endapo utafanya kazi kwa umakini na kujituma na kua na nidhamu na pesa, kupitia ajira hio ya Muda utapata connection nyingi tu.

NB: Usipoenda usirudi hapa kulalamika mtaani kugumu.
Haah. .nilihitaji mawazo na ushauri
 
Nakushahuri uende ukafanye hio kazi, kama sikosei ni kazi ya mradi wa wizara ya afya upate uzoefu na connection. Zikitoka za kudumu omba pia, Hizo database za wafanyakazi wa kudumu na wa mradi ni mbili tofauti wala Haito leta shida ukija kuomba kazi ya kudumu.
Umepatia Mradi unaitwa TMCHIS (Tanzania maternal child health initiative project ) imefadhiliwa na World bank iko chini ya Tamisemi na Wizara ya afya.
 
Binafsi huwa sipendi kuajiriwa ila mkuu umezingua

Nenda kapige hiyo miaka miwili

Kuwa na nidhamu ya Pesa

Jiwekee akiba ukiweza fungua fixed account kabisa ili endapo mkataba wako utaisha na usipopewa mwingine unakuwa tayari una mtaji

Unaangalia biashara ambayo una uzoefu nayo unafanya

Biashara ikichanganya unaweka mtu kisha unatafuta ajira nyingine(kama unapenda kuajiriwa)

Mtaani sio kuzuri mkuu

Unaweza ngoja hizo nyingine kisha ukazikosa, utafanyaje?
Ahsante shida .

Mjini nina kibarua cha private chenye mshahara kama huu
 
tamisemi kutoa ajira kuanzia application adi uje kuwa allocated kwenye kituo ni mchakato wa zaidi ya miezi sita . wewe kaa home wengine wakaanze one step ahead na zikija ukikosa uje kulia jukwaani.. nani kakuambia ukienda utashindwa kuomba kazi nyingine wakati ndio utakua na high chance. watu wako serikalini na wanaomba interview za serikali from scratch kabisa
 
Back
Top Bottom