Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,323
- 6,810
Juzi nilikuta ugumvi wa majirani wangu, kaka mkubwa na mdogo wake, kaka ni mkubwa kwa miaka 15 hivi. Kaka mtu anasema mdogo wake hamjali kabisa ingawa yeye ndiye aliemsomesha hadi darasa la saba alipofaulu na kuendelea na masomo hadi sasa kamaliza mavyuo na maisha yameanza kukaa vizuri.
Kaka mtu akasema "nilikuwa nakulaza njaa wewe siku tatu, hamna kula kitu chochote, na kukupiga nilikupuga! si unaona ulivyo na akili? tofauti na wenzio waliokulia raha." "mimi najua kulea bwana, angalia kina.........(akawataja ndugu zake) watoto wote waliokulia kwao hakuna aliyefanikiwa kama wewe!"
Sasa baadae mimi nikajiuliza hivi kumyima mtoto wa shule chakula siku tatu ni kujua kulea??
Kama ni kujua kulea yule bwana mkubwa itatakiwa awe anawanyima watoto wake wakuwazaa chakula kwa siku 6 hivi ili wawe na mafanikio maradufu, kwani hawezi kumlea vizuri mdogo wake kuliko watoto wake.
Mwisho, hivi jamani ni kweli ukimpa mtoto shuruba kama hizo za kumyima msosi atakuja kuwa na akili??
!
Yule mdogo mtu baadae akanifuata akaniambia kaka yake huwa anamkera sana kwa tabia yake hiyo...ya kumdhalilisha hata mbele ya mkewe na watoto akaniomba ushauri nikamwambia ntapa jibu, asubiri kwanza.. Jamani naomba ushauri wenu kwa niaba yake, please!