Je, Mahusiano gani mtu anatakiwa kuwa na familia yake?

Ricky Blair

JF-Expert Member
Mar 13, 2023
391
872
Je, Mahusiano gani mtu anatakiwa kuwa na familia yake?

Kwa kutumia akili timamu mahusiano yote yanatakiwa kuwa kama ya mfanyabiashara na kanuni za biashara kwa maana yatushirikiane na watu kwa kubadilishanamaadili tofauti yanayofanana natunayoyapenda kama ubunifu, michezo au muziki na falsafa zinazaofanana, siasa naMaisha kwa ujumla. Kwa muonekano huu, hu undo upeo mkubwa wa mahusiano yoyoteikiwemo uhusiano wa watu wa familia yako.

Watu wengi wanadanganywa na Imani hiikwamba lazima tuwapende watu wote katikafamilia yako kwa sababu ni damu yako na siokwa tabia zenu zikiwa zinaendana au hataakiwa ni mtu mwema bali ni familia yako tun a tunasikia kwenye misemo mingi ikiwemoDamu ni Nzito kuliko Maji.

Imani hiihaiendani na taswira ya mfanyabiashara ambayo inasemna inabidi uingie kwenyemahusiano yoyote ukiwa unapata kitu sio kwakujitolea tu hata kama hupati kitu, hivyo kunawana familia unaweza usipate kitu chochotecha muhimu iwe mawazo, mitazamo, msaadaunapohitaji au maadili yoyote ivyo unawezausiwapende hata kutaka kuwa nao mara kwamara.

Kuna tofauti kubwa kati ya Familia tuliyozaliwa nayo ambayo hatukuwa na uwezowa kuchagua mfano wazazi, dada, kaka nafamilia ambayo tunaweza kuchagua kama mkeau mume. Ikiwa mahusiano ya kwanza hatukuyachagua, itakuwa nadra sana kamatunaweza kuwapenda kila ndugu yetu kamaalivyo.

Uwezekano wa kuzaliwa nakuzungukwa na watu ambao mna mtazamosaw awa kifalsafa na mengine sio mkubwatena ni mdogo sana. Kuwapenda ndugu nawazazi wetu kiukweli kabisa italeta maanakama tungeendelea kuwapenda hata kamawasingekuwa ndugu au wazazi wetu.

Mahusiano pekee ambayo mapenzi yanawezakutawala na ambayo tunaweza kuyachagua nimapenzi ya mke/mume au hata marafikiambao unaweza kuwachagua na kuwaachakama hamtoendana au hata mkigombana, kituambachon huwezi kubadili Mama, Baba, Dada au Kaka zako. Chaguo la mke au mume au marafiki inameremeta maadili yetuyanayoendana.

Lakini mahusiano na familia ambayohatujaichagua sio muda wote yanatafakarimaadili yetu wote. Ingawa mahusiano yetu nahisia zinaweza kuwa za muhimu, uhusianohuu si wa lazima na pia kutokana namahusiano haya majukumu yetu pia nimadogo kuliko watu wanavyodhani.

Jukumu la kubwa la muhimu ni lile la wazazikwa Watoto wao wadogo ambao wanahitajiulinzi na kulelewa mpaka wakuwe na wawezekujitegemea na kufikiri binafsi. Kwa kuamuakuzaa kwa matakwa yao wenyewe na sio kwakulazimishwa, wazazi hao wanalivaa jukumuhili.

Sababu zao za kuzaa zinaweza kuwatofauti kama sababu ya maana kama kupataFaraja kushuhudia na kushiriki kwenye kuonaMaisha mapya yam toto mdogo akiwa anakuana sababu zingine za kipuuzi kama kubeba au kuendeleza jina la Familia na kadhalika. Lakini ukiachilia mbali sababu zao zozote ilikuwa wazazi wazuri ni lazima wajiwekezekihisia na kimali wakati Watoto zao wakiwawadogo na kutokuwa na uwezo wa kujitunzawenyewe.

Uwekezaji huu lakini hauwapi wazazi hao madai ya milele kwenye Maisha ya Watoto wao. Watoto hao wakiwa watu wazima, Watoto hao wanaweza wasiwaheshimu au kuwapenda wazazi wao kulingana na wazaziwalivyowalea na mahusiano waliyokuwa nayowakiwa wadogo.

Watoto hao ni lazimawawatambue wazazi wao kama mzizi waMaisha yao na kuwepo duniani lakini pia watambue sio lazima wawapende tu hata kamawamewafanyia mambo ya ovyo mfanokuonewa, kubakwa au maovu mengi ambayoWatoto wanaweza kupitia kwenye mikono yawalezi wao. Ivyo pia hakuna jukumu la mojakwa moja ya Watoto kuja kuwalea wazazi waowakija kuwa wazee. Amri hii sio ya mantikikwa sababu Watoto hao wasingewezakuulizwa kuhusu mkataba huu kablahawajazaliwa.

Jukumu hilo hutokea kwa Watoto kamawataendelea kuwa na mahusiano mazuri yakihisia na kimali na wazazi wao mpakawakiwa wamekua. Wazazi pia wanakazanakuendelea kutoa msaada hata ambapo siolazima tena Watoto wakishakua na hivyowanaendelea kufanya ivyo kwa raha yaowenyewe na kutaka Watoto zao wafanikiwe naivyo Watoto wanaweza kuchagua pia kuwaleawazazi wao mpaka watakavyokufa. Ila pia kama Watoto wamekua na wamekuwa watuwa ovyo sio lazima wazazi wawajibikekuwasaidia kwa lolote kwani kazi yaoimeshaisha. Ivyo muenendo huo unaendana nabiashara ya kutoa na kupokea.

Muda mwingine malumbano hutokea kwasababu ya tofauti na matarajio kutoka kwenyemahusiano haya. Kosa moja la matarajio ni hiiya kupendwa au kuheshamiwa moja kwa mojabila sababu. Lingine ni kwamba hii tabia yawazazi kutegemea au hata kulazimisha Watoto wao watafuata au kutaka kufuata misimamoyao ya falsafa, siasa au dini.

Lakini mawazoau mitazamo haiwezi kulazimishwa kwa watuna kila mtu lazima afanye uamuzi wake mwenyewe akiwa na akili timamu; ivyo siasaau dini Watoto wengi hurithi tu kutoka kwawazazi wao kama jina la mwisho la upande wababa zao. Kwaiyo wazazi hawana njia yakujua Watoto zao watakuwaje uko mbele, wanaweza kuwa na tumaini dogo tu. Lakinimalezi mazuri yanaweza kumfanya mtotoakue kuwa mtu mzuri na busara lakini pia haiwezi kufanya machaguo kwa hao Watoto uko mbeleni.

Mwishowe, ni muhimu tugundue kwambahata tukae kwa muda gani na familia zetutukiwa tunakua, familia yenyewe sio muhimusana kwenye kushepu mienendo yetu na utu wetu. Inaweza kusababisha vitu tofauti kamajinni tulizozirithi na malezi tuliyoyapokea, lakini kwenye mbio ndefu uko mbele inawezaisijenge sana utu wetu na mienendo yetuwenyewe ikawa chaguo letu natutakavyoamua kuishi Maisha yetu.

Ukiachanana kesi chache za uonevu, unyanyasaji ubakajiambao unaweza ukawa na madhara yakudumu uko ukubwani, lakini sote na utu wetuni maamuzi yetu na tunayochagua kuyafanya. Wazazi wa busara wanaweza wakawa msaadamkubwa tukiwa tunakua lakini kukosa wazazihao wenye busara sio sababu ya kufanya uovuau ujinga mwingi na kufeli kwa mambo mengiukubwani.

Hivyo basi uhusiano wa busara wa familialazima uwe kwenye maadili yanayofanana. Mahusiano mazuri katika familia sio lazima au muhimu sana kwenye furaha ya mtu lakiniyanaweza kuwa ya muhimu sana kuwa mziziwa furaha kwa wengi na kuacha urafiki mzurina wa kudumu, lakini sio kila mtu ana bahati hiyo ya kupatana na kila ndugu yake au wazazina ambapo wote mshakuwa na hampatani siolazima muendelee kuwa na mahusiano kamamtaishia kugombana tu au kila mtu kumtakamwingine abadilike kama mwingineanavyotaka, iwe mitazamo ya kisiasa, falsafa, dini au mienendo mingine ya Maisha.
 
Back
Top Bottom