Nimekoma kutumia Airtel Money.

Jana jioni nikiwa mitaa ya Sinza nilikuwa natafuta sehemu ambapo ningeweza kuweka Airtel Money kwenye simu yangu ili nimtumie mtu, nilikuwa nataka kiasi kama cha laki 2 mbili. Nikaanza kuulizia kwenye maduka amabyo yalikuwa na vibao vinavyoonyesha kuwa ni wakala wa Airtel Money lakini cha ajabu kila duka/kibanda nilicho ulizia hawakuwa na Airtel Money, zaidi tu ya kunijibu kuwa Airtel Money haipatikani, wanatusumbua sana, hawatuletei, hatupati virtual money, nina virtual kidogo siwezi kukupa yote… na blah blah za hivyo. Nilizunguka zaidi ya maduka/vibanda 10 na sikuweza kufanikiwa ila duka la Mwisho nililofika pale Survey ndiyo walionikatisha tama kabisa, nakumbuka dada muuzaji alinijibu kuwa mimi ninayo laki 2 lakini siwezi kukupa yote kwa sababu wateja wegine watakaosa, labda nikuuzie elfu 50 tu! Nuilichoka na hiyo 50 sikuchukua, mimi nilifikiri raha ya mfanya biashara ni kuuza kumbe kuna wengine wana reserve huduma kwa wateja ambao hata hawajulikani watakuja saa ngapi?

Airtel kwa kweli mnakatisha tamaa na huduma yenu hii mbovu kabisa, kumbe mnajua haipatikani ndiyo maana mnatuchosha na matangazo yenu kuwa inapatikana bure, mmekimbilia kututangazia matangazo yasiyokuwa na maana badala ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwanza. Halafu na nyie wauzaji/wakala kwanini mnakubali kuweka matangazo ya huduma hiyo wakati mnajua haipatikani?

pole sana mkuu ndio uwezo wao huo tatizo ni kwamba bado haijakubalika kivile mujini..
 
Kwa kweli hilo tatizo limekithiri sana.Lakini mimi nadhani kampuni haina tatizo ila ni wale mawakala katika ufanyaji shughuli.Unajua wakati mwingine sisi watanzania ni wazembe sana katika biashara tunataka kujionyesha kwamba tunajua biashara wakati hakuna kitu.Mtu anaomba uwakala kwa umakini kabisa na kampuni inamuona huyu atafanya vyema hatimaye ankuwa mzembe.Sasa sijui ni mtaji unamuishia au nini.Kwa hili hatuko makini.Hata vocha za Vodacom ya shs 450 wanatuuzia 500.Ukimuukliza kwa nini unauza hiyo bei anasema hailipi tukiuza 450.Swali:Sasa si uache kuuza uuze vyenye faida na sisi kukandamiza wengine?
 
Usimshangae hy dada, ana royal customers wake hataki kuwapoteza kwa ww mpita njia, hujawai kuona ht maduka makubwa wanaacha kukuhudumia ww na kumhudumia aliyekuja baada ya ww, we ni mpitaji tu.
 
Watu mnadanganywa na vya bure. Hakuna kitu cha bure hapo. Kama ni bure wanapataje faida? Jiulize hilo swali kabla hujaliwa. So far, M-PESA ndio superior mobile money transfer service in Bongo. Nimeitumia mara nyingi sana na sina regrets kubwa sana ila inconvenience fulani pindi service inapokuwa down lakini ikirudi ni bien.
 
Ni bora kuachana na hiyo 'eatel mane,' inakatisha tamaa, kero nyingi. Nimemtumia mai waifu wangu elf 40, wakala kakata elf 2,kampa elf 38, kisa? anadai mtandao haumpi chochote? ndo aibe pesa za wateja? si aache kufanya nao kazi? pata picha kila atoaye chini ya laki 1 anakatwa elf 2, ni wizi ulioje?
 
Tar 8 walitutumia sms za kubadili password,nikabadili juzi nikanunua mpesa kama 250,000 kwa mara ya kwanza kutuma airtel money,nikawa namtumia jamaa yangu kama laki 2 hivi,cha kushangaza password ikawa tatizo attempts zote 6 zikafail wakalock simu nikaenda ofisini kwao wakasema utapigiwa simu mpaka sasa siku ya pili sijui hatima ya pesa yangu,

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Kumbe ndio ilivyo! Mimi nilifikiri nimesahau password ati, najuta sana kupadili password coz siwezi hata kumtumia mtu salio.

Ulifanikiwa kuifungua?
 
nzagamba yapi ndugu yangu eti wakiblock inachukua wiki mbili kufungua account yako tena. Mimi sijawahi pata logic ya hii kitu.
Mimi pia natumia airtel wiki mbili zilizopita nilikuwa nashughulikia airtel money account yangu jamani walinizungushaaa...mara ooh baada ya masaa 48 utatumiwa ujumbe..ooh baada ya masaa 48 password itarudi 1234 then utabadili..mara ohh account yako haina hela ndo maana tunashindwa kuaccelerate tatizo lako kwa it..mara ohh nenda kasajili namba yako...kumbe namba ishasajiliwa maana nlikuwa naweza access ile menu after 150*60#.mara ohh umepiga maranyingi so usipige tena subiri 48 hrs itakuwa sawa..nikangoja three days nkajaribu holla...nikapiga ndo nikaambiwa two weeks ndo account yako itakuwa ok watanitumia message. Tarehe 14 ndo wiki mbili ziliisha leo 17 sioni msg sioni simu..na wala siwatafuti.
Nmenunua line yangu ya tigo napata sms za bure..net bure...dk 15, na tigo pesa....ol kwa sh. 450.

nilishalitupa li line lao
 
Back
Top Bottom