Nimekatwa Tsh 5,300 kuhamisha Tsh 50,000 kutoka NMB mobile kwenda M-PESA

Kwa hali ilivyo kama huna umuhimu wa kumiliki akaunti ya benki nakushauri chimbia pesa zako ardhini tu njia salama na ya uhakika isiyo na makato ya kingese.
 
Nilikuwa sijawahi kutumia hii huduma lakini sasa nilijaribu wiki mbili zilizopita na sikuangalia salio. Muda huu nimepata bank statement kwenye email ndio naona hayo makato.

5300 (NMB 4491.53 na Vat 808.47) imenishangaza kukatwa zaidi ya asilimia 10 ya fedha niliyohamisha.

Hongereni sana NMB Tanzania
 
Attachments

  • 20220723_104036.jpg
    20220723_104036.jpg
    182.6 KB · Views: 17
Hizi bank zinatupelekesha zinavyotaka yani hawajali chochote. Wakiamua kupandisha transaction fee wapandisha tu wanavyojua. BOT kama regulatory body nao wamechill tu wavuja jasho tunaumia.

Hii nchi ni Shenzistan.
Mwigulu ndio tatizo...akipigwa chini watu tutapumua
 
Nilikuwa sijawahi kutumia hii huduma lakini sasa nilijaribu wiki mbili zilizopita na sikuangalia salio. Muda huu nimepata bank statement kwenye email ndio naona hayo makato.

5300 (NMB 4491.53 na Vat 808.47) imenishangaza kukatwa zaidi ya asilimia 10 ya fedha niliyohamisha.

Hongereni sana NMB Tanzania
Hizo huduma zina makato makubwa balaa,pole sana 😁😁
 
Hivi nilivyoeleza kuhusu tozo hamkuelewa vizuri
Wapi statement iliposema tozo ndio 5,000? Tozo ni 800 tuu..

Ni ajabu watu kulalamika tozo ndogo wakati makato ya makampuni ni makubwa mno..

Hata miamala ya simu makato ya kampuni za simu ni kubwa karibu mara 2 ya tozo za serikali sasa sijawahi elewa Kwa nini Serikali inalalamikiwa.
 
Kama hujaelewa ni kwamba kufanya muamala la kwenda nje ya taasisi husika..

Kama unabisha tuma pesa hapa kutoka mtandao wako wa simu kwenda mtandao tofauti uone moto.
Ni kweli mtandao mmoja kwenda mwingine inaongezeka kiasi lakini sio kama hayo ya elfu 5+ kwa kuhamisha elfu 50.
 
Wapi statement iliposema tozo ndio 5,000? Tozo ni 800 tuu..

Ni ajabu watu kulalamika tozo ndogo wakati makato ya makampuni ni makubwa mno..

Hata miamala ya simu makato ya kampuni za simu ni kubwa karibu mara 2 ya tozo za serikali sasa sijawahi elewa Kwa nini Serikali inalalamikiwa.
Acha kuwa mbishi ndio wame introduce juzi chunguza utajua,zamani tozo ilikuwa kwenye simu tu bank hazikuwepo na wengi tulikimbilia huko.
 
Back
Top Bottom