Nimekatwa Tsh 5,300 kuhamisha Tsh 50,000 kutoka NMB mobile kwenda M-PESA

Nilikuwa sijawahi kutumia hii huduma lakini sasa nilijaribu wiki mbili zilizopita na sikuangalia salio. Muda huu nimepata bank statement kwenye email ndio naona hayo makato.

5300 (NMB 4491.53 na Vat 808.47) imenishangaza kukatwa zaidi ya asilimia 10 ya fedha niliyohamisha.

Hongereni sana NMB Tanzania

Sasa hivi kila kona utakayotaka kupitia makato yapo yanacheka tu, yaani hakuna ujanja aisee! Weka sasa hivi milioni moja benki halafu nenda kesho kaitoe kwa njia ya foleni! Mbona utachekea Madaba!
 
Nilikuwa sijawahi kutumia hii huduma lakini sasa nilijaribu wiki mbili zilizopita na sikuangalia salio. Muda huu nimepata bank statement kwenye email ndio naona hayo makato.

5300 (NMB 4491.53 na Vat 808.47) imenishangaza kukatwa zaidi ya asilimia 10 ya fedha niliyohamisha.

Hongereni sana NMB Tanzania

Kwa kifupi kwenye makato hawa jamaa wamekaba kila kona hadi kivuli chao!
 
Nilikuwa sijawahi kutumia hii huduma lakini sasa nilijaribu wiki mbili zilizopita na sikuangalia salio. Muda huu nimepata bank statement kwenye email ndio naona hayo makato.

5300 (NMB 4491.53 na Vat 808.47) imenishangaza kukatwa zaidi ya asilimia 10 ya fedha niliyohamisha.

Hongereni sana NMB Tanzania
Binadamu wote siyo sawa. Yani iyo shilingi 5,300 unaona nyingiiiii. Mara ya kwanza niliposoma nilidhani umeandika umekatwa 5.3 millions kuhamisha Billion 5.
 
Tulio wengi tupo hivi, heri yako wewe Bilionea! Ila jamani makato yamekuwa mengi mno, kila mahari ni makato tu!!
Asante mkuu. Shukran za dhati kuwa billionaire siyo mchezo.

Ila haya makato ni mzigo kwa mtanzania. Halafu serikali haijali. Bora angalau kungekuwa na tija katika haya makato. Sijui lini tutaendelea kama taifa. Yani hata sisi wabeba boksi ukituma hela homie reciever akipokea tu ya ni makato ya hatariiii.

Wakulaumiwa hapa ni Putin na Magufuli.
 
Hoja hapa sio hiyo shs 5300, ishu ni kwamba hiyo ni zaidi ya asilimia 10 ya fedha iliyohamishwa.

Ni sawa na ukatwe zaidi ya 5m kwa kuhamisha 50m
Nimekupata mkuu 10% nyingi Sana angalau ingekuwa 2% kulingana na kipato Cha watanzania wengi. Yani wanashindana na Mungu kwenye makato kwasababu zaka lazima ukatwe 10% sasa nao eti wanaiga
 
Back
Top Bottom