Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Mada hii inaonesha hakuna ushirikiano kati ya akili, moyo na sehemu nyingine ya mwili. Akili inasema humfahamu Gambo lakini mdomo unaimba sifa za Gambo.
Hahahaha,hapendi tuu naturally, huwa inatokea tuu anawapenda wakaka!kila mtu analijua hiliHivi mbona sijawahi kukuona ukiwasifia wanawake?
UKUTA unawapa shida sana....nazidi kuamini kuwa Chadema imekua kimkakati tofauti na zamani.“TUNATAKA kuona taifa hili likiwa na vijana jeuri na wenye kujiamini, wasiwe vijana waoga aina ya ‘ndiyo’ bwana, mkubwa; vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya Kitanzania. Tunataka vijana wenye misimamo thabiti dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika taifa,”
Haya ni maneno aliyopata kuyanena, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Siku moja wakati nasoma Biblia nilikutana na ujumbe wa Mwanzo 45:5, ulisema “Yusufu akawaambia kaka zake, ingawa ninyi mliniuza ila Mungu alikusudia kunitanguliza ili niwasaidie”
Maendeleo ama mabadiliko katika nchi yoyote yanaletwa pale kunapokuwapo na watu walio tayari kuishi maisha ya kujitoa, watu ambao wanaamini kuwa wanao wajibu mkubwa kwa jamii yao.
Kimsingi mimi simfahamu sana na sina maelezo mengi kuhusu mtu niliyeamua kumzungumza leo mwenye jina la MRISHO MASHAKA GAMBO, maana yeye akiwa kwenye Umoja wa Vijana wa CCM kama mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM 2008 – 2012 kutoka Mkoa wa Arusha, mimi nilikuwa BAVICHA, wakati mimi nikijiunga na UVCCM na CCM mwaka 2013 mwanzoni yeye alikuwa ameshateuliwa kuwa DC wa Korogwe (akiwa DC wa Kwanza kwa wakati huo kubeba matofali na kushiriki kujenga shule na zahanati na Wananchi). Hivyo ni mtu ambaye nimekuta maneno yaliyovumisha sifa yake lakini sikupata bahati ya kumfahamu vizuri.
Lakini maneno niliyoyakuta ambayo yanamuelezea GAMBO yalishabihiana sana na maneno ya Mwalimu niliyoyanukuu, kuwa GAMBO ni Kijana JEURI, JASIRI na ANAYEJIAMINI.
Nimeambiwa katika historia ya maisha yake, halijawahi kutumika neno la MUOGA, kumuelezea juu ya wajihi wake na sifa yake…wala yeye mwenyewe hajawahi kusikika katika maisha yake akitamka neno NAOGOPA, ni Kijana anayehoji kwa HOJA.
Lakini hayo ni tisa, Kumi Mrisho Gambo ni Icon kamili ya Mwanamapinduzi anayechukia mifumo kandamizi, mifumo ya Ubwana na UFISADI. Historia yake inatueleza hivyo, alimkataa Mhe Lowassa ingawa alikuwa anatoka nae Mkoa mmoja tangu akiwa UVCCM kwa sababu moja kuu UFISADI.
Kwenye title ya andiko langu nimesema nimekataa kumpongeza Gambo, ni kweli nimekataa..!! Maana sio kwa juhudi za Mrisho pekee ndizo zilizomfikisha hapo bali malezi mazuri yanayotolewa na CCM na UVCCM kwa vijana wake ndio yaliyofanikisha kuwapata Mawaziri kama akina Makamba, Mavunde, Masauni na wengineo, ni mazao ya UVCCM yaliyotuletea wakuu wa Mikoa mahiri kama akina Makonda, Gambo, Mtaka na wengineo pamoja nao Ma-DC katika maeneo mbalimbali ya Nchi yetu. Kwa malezi haya nimeamua kuipongeza UVCCM na CCM na kukataa kumpongeza GAMBO.
Ni CCM pekee inayojenga Vijana majasiri wanaoweza kuwahoji Viongozi wao hadharani, katika historia yake GAMBO alipishana mawazo na kuhoji hadharani juu ya Lowassa, alihojiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na wakubwa wengine pale alipoona wanaenda kinyume na matakwa na matarajio ya jamii yetu, Jamii yetu ina kiu ya Maendeleo, Kiongozi yeyote anayekwamisha maendeleo katika eneo ambalo GAMBO yupo basi huyo amejitangazia Vita na Uadui mkubwa na Kijana huyu. Daima alitaka kuona haki ikitendeka na wananchi wanahudumiwa. Hata hivi karibuni Yule jamaa wa M4C wa Arusha Mjini alipotaka kupima ubavu, alijikuta kadondokewa na kitu kizito chenye ncha kali (maana sasa hivi Serikali imepiga marufuku zile posho zao za kifisadi) Ni CCM na UVCCM sio CHADEMA, sio BAVICHA wenye uwezo wa kutoa Vijana makini na wasio waoga na mabwana ndio Mzee. Wao ni Vijana wa kusubiri maelekezo na kutumwa kubweka.
Mungu amemchagua na kumuinua GAMBO, akamtenga mbali na dhulma na wafitini. Ni kama ilivyo kwa Yusuph, MUNGU ameamua kumtanguliza Gambo ili awasaidie. Mkoa wa Arusha unakufa, biashara zimesimama, utalii unadorora, mahoteli yanafungwa kwa sababu za kipuuzu na upuuzi wa mtu mmoja na kijikikundi chake, MUNGU amemuinua GAMBO ili awasaidie kuirudisha heshima ya ARUSHA.
Nimekataa kumpongeza GAMBO lakini nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru na kumpongeza Mhe John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuwaamini vijana na kuwapa nafasi, hakika mimi nachukua ahadi kwako kwa niaba yao kuwa HATUTOKUANGUSHA.
Hahahahahahaha umenichekesha Sana Mkuu,eti anampongeza Mungu!!!Hueleweki,Mara unaipongeza CCM na UVCCM ,Mara unampongeza Mungu!
Hujui kwamba Mungu Mwenyezi hajangamishwi na siasa ? Mungu aapenda wema,Upendo na haki.
CCM mnapenda siasa,ghasia na dhulma ambazo ni chukizo kwa Mungu
Kukiwasilisha?Sijaelewa hata nini huyu dada anataka kukiwakilisha kwenye bandiko lake
"Fasihi""humfahamu" lakini hatokuangusha na unampongeza sana?! Juliana tulia tu maana kila ukisema unaharibu na kuonesha jinsi ulivyo
Labda una mahaba nae lakini Hugo Gambo hamfikii hata kidogo Mdee,Mnyika, Katani s.Katani, Heche, n.k. Acha sifa za kitoto.Yaani mwenye sifa zote ulizomwaga hapo ni mtu unayekiri kuwa haumfahamu! Naomba basi unielekeze kitabu kinachomuhusu kinaitwaje ili na mimi nimfahamu kupitia historia yake!
CCM bwaaaaaana LOWASA tu ndio fisadi kwao hapa tu ndio uwa nashindwa kuwaamini kabisa na sitaweza kuja kupiga kura kwa mtu yoyote wa CCM wala sitaweza kuja kujitolea kwa kitu chochote kwa CCM mana ntakuwa nafanya unafiki na mimi sio mnafiki majizi yamejaaa uko kama yule wa bariadi, wale wa ESCROW, chenji ya radar, nyumba za serikali, lugumi at least wangekuwa wanayataja na mengine kama wanavyomtaja LOWASA ningekuwa na imani ila wao fisadi lowasa wakati kuna wakina lowasa umo na zaidi ya lowasa kibao.
unadadavua kwa kutumia kiungo gani cha mwili?Hakika,umenena kweli.CCM bado itaedelea kutoa viongozi mbalimbali wa nchi hii kwa karne nyingi zijazo...na hata kwa upande wa upinzani wataendelea kupata wagpmbea wa nafasi mbalimbali kuanzia mashinani hadi uraisi kutoka CCM...hili halina ubishi.