Butola
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 2,290
- 756
Kawadanganye wengine sio sisi hapa JF. Kama una uhakika kwamba mtatiro haendeshi maisha kwa kutegema siasa unabidi uthibitishe kwamba anafanya shughuli gani na policy ya cuf inasemaje kuhusu malipo ya viongozi wa kitaifa interms of malipo.
Usisahau kwamba tunayo kumbukumbu ya docs za Lwakatare alipojiengua cuf kwahiyo tunafahamu kwamba hawa wanasiasa wako kazini na wanalipwa kwa kazi zao za kisiasa.
Rais wa nchi analipwa mshahara mnono na marupurupu kedekede huku akitunzwa kwa kodi za wananchi maskini, halipi kodi na ananunuliwa kila kitu hata nguo na viatu. Siasa ni maisha, labda asiyetegemea siasa kuendesha maisha ni watu kama akina sabodo na ndesapesa kwa kutaja wachache.
Umepita kushoto kabisa.
Kuwa mtu makini, mkweli na kuweza kutembea kwenye maneno hakuhusiani na malipo wala posho, na bahati mbaya sana kwa nchi yetu, nyanja ya siasa imejaa wapiga domo tu wasio na uwezo wala ujasiri wa kutembea kwenye maneno yao, kuwa na akina Mtatiro wengi kwenye siasa ni afya kwa taifa...