Nimeikodi helikopta bila kushauriwa wala kuelekezwa na Jussa wala Hamad Rashid - Mtatiro

Kawadanganye wengine sio sisi hapa JF. Kama una uhakika kwamba mtatiro haendeshi maisha kwa kutegema siasa unabidi uthibitishe kwamba anafanya shughuli gani na policy ya cuf inasemaje kuhusu malipo ya viongozi wa kitaifa interms of malipo.

Usisahau kwamba tunayo kumbukumbu ya docs za Lwakatare alipojiengua cuf kwahiyo tunafahamu kwamba hawa wanasiasa wako kazini na wanalipwa kwa kazi zao za kisiasa.

Rais wa nchi analipwa mshahara mnono na marupurupu kedekede huku akitunzwa kwa kodi za wananchi maskini, halipi kodi na ananunuliwa kila kitu hata nguo na viatu. Siasa ni maisha, labda asiyetegemea siasa kuendesha maisha ni watu kama akina sabodo na ndesapesa kwa kutaja wachache.

Umepita kushoto kabisa.

Kuwa mtu makini, mkweli na kuweza kutembea kwenye maneno hakuhusiani na malipo wala posho, na bahati mbaya sana kwa nchi yetu, nyanja ya siasa imejaa wapiga domo tu wasio na uwezo wala ujasiri wa kutembea kwenye maneno yao, kuwa na akina Mtatiro wengi kwenye siasa ni afya kwa taifa...
 
Kama kweli mtatiro ulifanya uamuzi wa kukodisha helikopta bila kumshirikisha mwenyekiti wako prof. Lipumba kama alivyokaririwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba hana taarifa ya helikopta.

Na kama ni kweli hukushauriwa ama kushauriana na jusa pamoja na hamad rashid, na umetumia sh. 50m kukodisha chopa huku mkipata sh. 100m kwa mwezi kama ruzuku basi muda wa wewe kupoteza nafasi yako ya unaibu katibu mkuu bara umewadia.

Labda kama ni kweli gamba kuu rostam ndiye kailipia hapo utanusurika lakini vinginevyo unakwenda na maji.

50m ni pesa ndefu sana kwa CUF. Kama Mtatiro angelipa pesa hiyo bila wenye chama chao kujua, angekwenda na maji immediately baada ya kutangazwa kura zao za aibu walizovuna Igunga.
 
Heshima J Mtatiro.

Mkuu asante kwa kutoa ufafanuzi anayetaka kuelewa atakuwa ameshaelewa asitaka kuelewa kapenda mwenyewe.Hongera kijana chapa kazi ni wakati muafaka CUF ijiulize inapata faida gani kwa katibu wake mkuu kuwemo ndani ya serekali ya mapinduzi Zanzibar.
 
Helikopta tuliyoitumia kwenye uchaguzi wa Igunga nimeikodi mimi mwenyewe na wala haikumhusisha Jussa wala Hamad Rashid.
Haya masuala ya kuwa imetolewa na na ROSTAM AZIZ ni p

ropaganda zinazopigiwa debe tu kama ilivyo ishu ya CUF IMEOLEWA NA CCM, CUF NI CCM B n.k.

Hizi ni propaganda zilezile za kuiumiza CUF lakini sie kama chama tutaendelea kuwa imara na kuwaelimisha wananchi juu ya propaganda hizi ambazo zinafanywa ili kuhakikisha CUF haiungwi mkono.

Nime-attach docs muhimu ambazo nilizi-process mimi mwenyewe kupata HELIKOPTA. Chama chetu kinapata ruzuku ya TZS 100m kwa mwezi, hatuwezi kushindwa kukodi helikopta kwa TZS 50m hadi tusubiri kufadhiliwa na makada wa CCM. Na tangu nimekuwa kiongozi wa CUF sikuwahi kuona tunafanya jambo lolote kwa pesa za kuletewa na matajiri.

Kinachoshangaza ni kuwa watanzania wakiandikiwa propaganda yoyote huanza kusihabikia na kuisambaza bila kujua nani aliyeileta na ana malengo gani na ikishafanya kazi itamnufaisha nani.

Pia, Baraza kuu la CUF halina mandate za kiutendaji, masuala yote ya kuidhinisha bajeti kubwa za chama au za dharura yanafanywa na KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA na baraza kuu litakagua taarifa kama kila kilichotumiwa na kufanywa na KUT ni sahihi na kilifuata masharti ya kibajeti ya chama.

Aliyeweka thread kuwa tumehongwa helikopta na CCM asome hizi docs and details na UONGO wake hataufanya siku zote.

Mtatiro.
Mkuu hizo ndo siasa lakiani atuwe kujua kama kweli.au umechukuwa pesa kotekote kwa maliopo yaleyale.
 
alikuwa haijui jf huyu .......inaonekana wewe ndio mekodi helkopta na sio chama tena kwa hela zako........hizo risiti hata mimi huwa nikinunua pampas za mwanangu blanca huwa naandika jina langu kwenye risiti.....usitutishe kijana....kingine ni kwamba inaonekana kuna mapungufu mengi kwenye hiyo "Helicopter Confirmation, payment .......wewe ni mwana siasa mzuri lakini kuna wakati huwa unakosea sana kuna maneno huwa unatoa kana kwamba u mgonjwa.....mfano ana kuna neo ulilisema huko igunga nikabaki nakushangaa kweli!!!
 
Mtatiro mi bado nakukubali sana kwa misimamo yako tangu nakuona tukiwa chuo na naamini utendaji wako ila SEHEMU ULIPO SIO SAHIHI
Nakushauri uhame la sivyo utapotea na nguvu unayotumia kutetea maslahi ya watanzania haitaonekana kuwa na maana,sikushauri uhamie ccm maana hilo ni kaburi kwako ila anzisheni chama kipya au hamia CHADEMA
ni ushauri tu mkuu murah weito!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Pole Mtatiro,
Ukisikiliza mambo ya JF hutakaa ufanye kazi, sana utavunjika moyo
Hata wenzao kina Zitto wameacha kupost mambo yao JF.
We piga kazi majungu achana nayo.
 
Wakuu vipi hii iko sawa?

Tarehe ya kusaini so called contract

2v84wua.jpg

Tarehe ya kuomba vibali na tarehe za kutaka kutumia helkopta

20uxthx.jpg
Tulimwambia Mtatiro JF si watu wa kuwa underestimate ona sasa madudu yanayoibuliwa

Tarehe ya kuomba kibali kutumia Helkopita kutoka Mamlaka ya anga 26/09/2011
Tarehe ya kusaini mkataba na QWIK FLIGHT(wenye Helkopita) 25/09/2011

Uliwezaje kusaini mkataba wa kutumia wakati hujapewa kibali? vile vile hao QWIK FLIGHT walikubali vipi bila wewe kuwaonyesha kibali kutoka mamlaka ya anga?
 
halafu headed paper nyingine bana ..." The Civic United Front" au "Civic United Front"
 
Mtatiro mi bado nakukubali sana kwa misimamo yako tangu nakuona tukiwa chuo na naamini utendaji wako ila SEHEMU ULIPO SIO SAHIHI
Nakushauri uhame la sivyo utapotea na nguvu unayotumia kutetea maslahi ya watanzania haitaonekana kuwa na maana,sikushauri uhamie ccm maana hilo ni kaburi kwako ila anzisheni chama kipya au hamia CHADEMA
ni ushauri tu mkuu murah weito!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hapo kwenye red sidhani kama kulikua na haja ya kupaandika. Usipoteze muda kumshauri ahamie CDM kwani hawezi kupokelewa mtu wa namna ndani ya CDM. Unadhani ni jamvi la malosser? Mtatiro anaipenda siasa lakini siasa haijampenda kabisa, umma umemkataa kabisa. Mshauri aache siasa afungue biashara kama ya majembe auction mart itampa faida sana na ndiyo inaendana naye sana.
 
Yes mr Mtatiro! Kwanza pole na hekaheka za uchaguzi. Pia nilibahatika kusoma ile post yako uliyokiri kuwa mmepoteza jimbo la Igunga.
Anywayz nisikuchoshe kwa maneno marefu sana na badala yake acha niende kwenye point. Mkuu Mtatiro wewe ni mmoja kati ya wapi
ganaji wazuri sana kwenye nchi hii ambao wanataka kuikomboa Tanzania kwa mara ya pili kutoka kwa hawa wakoloni weusi! Ila tatizo lako
hiyo sehemu uliyokuwepo siyo mahala pake for sure. Amini maneno yangu CUF haitakufikisha popote,badala yake itakupotezea mda na
mvuto wako kwa watanzania. Mie ningekushahuri ni bora ukajiunga na wapambanaji wenzako ndani ya CDM. Mkuu kwa sasa watanzania
waliowengi matumaini yao wameyaweka kwa CDM....yaani wanaona atrist kidogo CDM inaonyesha uhalisia wa uongozi na utawala bora ku
pitia vikao vya bunge,kwenye media na kwenye mikutano ya hadhara tofauti na vyama vingine. Mkuu jiunge na CDM kwa faida yako na
kwa faida ya nchi yako.....na CDM watakupokea kwa mikono miwili na kwa moyo mmoja. Ninahuhakika wa 70% kama utagombea ubunge
mwaka 2015 kupitia CDM basi ni lazima uukwae ubunge....utakuwa mbunge wa kinondoni au somewhere kanda ya ziwa. Pia habari ambazo
nimezipata toka chini ya karpet kutoka kwa mtu wa jikoni ni kuwa Shyrose Bahnji yuko mbioni kujiunga na wapambanaji wa CDM ili mwaka
2015 asimame jimbo la kinondoni kupitia CDM. Ujachelewa mkuu fanya maamuzi magumu sasahivi kwa faida yako na kwa faida ya nchi yako.
Kaa chini,tafakari,kisha chukua hatua! By Najee Mshikachuma
 
Hivi we ndio yule Mtatiro wa enzi zile pale UDSM?

Kipi kimekusibu kaka?

Uhoni kama upo sehemu isiyokufaa?

Ushauri wangu:kuanza upya sio ujinga,tafuta sehemu nyingine sahihi ya kuendeleza harakati zile ulizokuwa unahubiri enzi zile,CUF apakufai wanakuchoresha na wanakurostisha tu,taifa bado linaitaji mchango wako kwenye safari ya mabadiliko
 
Hapa nana umemuiga babu yako Kinana hahaha ahahaha ahahahah!!!!!!!!!!! hizo tarehe na reference numbers mbona ziko kinyume nyume?????

2w5lfsg.jpg

2qdvccj.jpg
Nimekuaminia mkuu Nyambala yale yale ya Kinana, kama kweli katumia pesa za chama aangalie sana maana Mil.50 si mchezo nawajua wazee wa CUF-Zenji wanaweza wakachukulia advantage na kumsumbua maana hata Lipumba amesema hana taarifa za helikopita sasa kama m/kiti wa chama taifa hajui unategemea nini, Mtatiro atasalimika tu endapo pesa itakuwa imetoka kwa RA.
 
sipendi chama chochote cha siasa ila napenda baadhi ya wanasiasa!mtatiro ni miongoni mwa majembe ninayoyakubali!...........CUF mlipoteza sana mtu Tunduru,Mazee (RIP)
 
Yes mr Mtatiro! Kwanza pole na hekaheka za uchaguzi. Pia nilibahatika kusoma ile post yako uliyokiri kuwa mmepoteza jimbo la Igunga.
Anywayz nisikuchoshe kwa maneno marefu sana na badala yake acha niende kwenye point. Mkuu Mtatiro wewe ni mmoja kati ya wapi
ganaji wazuri sana kwenye nchi hii ambao wanataka kuikomboa Tanzania kwa mara ya pili kutoka kwa hawa wakoloni weusi! Ila tatizo lako
hiyo sehemu uliyokuwepo siyo mahala pake for sure. Amini maneno yangu CUF haitakufikisha popote,badala yake itakupotezea mda na
mvuto wako kwa watanzania. Mie ningekushahuri ni bora ukajiunga na wapambanaji wenzako ndani ya CDM. Mkuu kwa sasa watanzania
waliowengi matumaini yao wameyaweka kwa CDM....yaani wanaona atrist kidogo CDM inaonyesha uhalisia wa uongozi na utawala bora ku
pitia vikao vya bunge,kwenye media na kwenye mikutano ya hadhara tofauti na vyama vingine. Mkuu jiunge na CDM kwa faida yako na
kwa faida ya nchi yako.....na CDM watakupokea kwa mikono miwili na kwa moyo mmoja. Ninahuhakika wa 70% kama utagombea ubunge
mwaka 2015 kupitia CDM basi ni lazima uukwae ubunge....utakuwa mbunge wa kinondoni au somewhere kanda ya ziwa. Pia habari ambazo
nimezipata toka chini ya karpet kutoka kwa mtu wa jikoni ni kuwa Shyrose Bahnji yuko mbioni kujiunga na wapambanaji wa CDM ili mwaka
2015 asimame jimbo la kinondoni kupitia CDM. Ujachelewa mkuu fanya maamuzi magumu sasahivi kwa faida yako na kwa faida ya nchi yako.
Kaa chini,tafakari,kisha chukua hatua! By Najee Mshikachuma
Hapo kwenye red nataka ufahamu kuwa CDM sio jamvi la makapa. Wapo watu makini ambao sio maarufu lakini wanaumuhimu na wanahitajika na CDM ila sio Mtatiro na wala hakuna utaratibu wa kupokea kila anayetoka kwenye chama chake.
 
CUF wala msipoteze muda wenu, na ninawashauri wale vijana shupavu watoke huko mara moja na kujiunga na upinzani wa kweli. Kama unadhani ni propaganda za CDM dhidi yenu basi zimewazidi nguvu kabisa. Huku bara hamtakubalika tena. Nataka nikuhakikishie Mtatiro hata ukitokea uchaguzi mdogo Lindi ama Kilwa ama Mtwara na CDM ikatia mguu mtapata chini ya hizo za Igunga. Kubalini ukweli CDM iko juu sana sasa na watanzania wankitazama kama mkombozi wa nchi hii na ndivyo kilivyo. Hakuna jitihada mtakazofanya kurejesha imani kwa wananchi, labda mvunje Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inaweza kuwasaidia, lakini Chadema imewafunika kabisa.

Sasa mimi napendekeza kitu kimoja, tokeni humo enyi vijana shupavu wapenda ukombozi, jiungeni na CDM tuimalize CCM, kama mtakataa ushauri huu msije mkamlaumu mtu. Haya!!! ya Igunga mmeyaona kama msipojifunza sisi hatutakuwa na la kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom