Nimehama eneo nililojiandikisha kupigia kura, nifanyeje?

Kaduguda

JF-Expert Member
Aug 1, 2008
724
641
Wana jamvi, kuuliza si ujinga maana nataka kujifunza kama si kueleweshwa kiufasaha.

Nina shahada yangu ya kupigia kura ambayo nalijiandikisha wakati nikiwa mwanafunzi chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Sasa nimemaliza shule na nimerudi kwetu mkoani, je nawezaje kuitumia haki yangu ya kupiga kura kupitia shahada yangu? Maana sidhani kama nitakuwa na uwezo wa kurudi jimbo la Ubungo kwa mzee Keenja nikapige kura kule. Nifanyeje katika hili?

Nawakilisha!
 
swali zuri. Hata mimi ningependa kujua hilo...

Kama sikosei tume ya uchaguzi huwa inatoa matangazo ya kuandikisha wapiga kura wapya katika mikoa kila baada ya muda fulani, kuna waliotimiza umri, wahamiaji km wewe n.k. Sasa sijui mkoa wako washapita au vipi.

Ila mimi sina hakika km nitaweza kuchagua mbunge wangu (ubungo) kwa sasa nishaishi zaidi ya mikoa 5 tangu 2005 na sijui km nitatulia mkoa mmoja before uchaguzi mkuu. Ila ninavyofahamu nitaweza kupiga kura ya URAIS only
 
Ukienda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri/Manispaa/Mji/Jiji uliopo sasa utapata maelekezo mazuri tu nini cha kufanya.
 
Mwanzoni mwa mwaka 2010 Tume ya uchaguzi itaboresha daftari la wapiga kura kwa kuingiza wapya(waliotimiza miaka 18 na wahamiaji kama wewe) na kuondoa waliofariki.
Usihofu
 
Niwashukuru wadau kwa majibu hayo japo huo mlolongo mpaka nimuone huyo mkurugenzi, sijui! Maana nao wamejiweka kwnye nafasi ambazo kuwa reachable ni shughuli nyingine. Ngoja tusubiri hilo tangazo la maboresho ya daftari la wapiga kura, natumai litatangazwa kwa nguvu za kutosha ili hata wale ambao hawana njia za mawasiliano waweze basi walao soma mabango!.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom