Nimefiwa na mama yangu mzazi

Pole sana Best! Ujipe Moyo tu kwani hata sisi 2wasafiri,na 2kiwa na IMANI hakika mama ye2 2tamwona siku moja na kufurahi naye Milele.Bwana ametoa na Bwana Ametwaa,Jina lake lihimidiwe! Amennn!!
 
Pole sana rafiki yangu, naamini kabisa kuwa inauma na siku zote kifo huwa haizoeleki, ila jipe moyo hayo ni changamoto za maisha.
 
Inna LILLAHI wa Inna Ilaihi Raji'oon, Pole sana Mchaka Mchaka. Mwenyezi Mungu akupe subra.
 
Pole sana, mwenyezi ampunzishe mama kwa amani.
Ni kipindi kigumu sana, Mwenyezi akupe uvumilivu na nguvu. Amin
 
ndugu zangu jumapili iliyopita tarehe 15.5.2011 ilikuwa siku mbaya kwangu kuliko zote. Mama yangu kipenzi alitangulia mbele ya haki. Tulimzika juzi jumanne. Ila kila nikijaribu kufanya chochote nashindwa nishaurini wenzangu. Nahisi nitamfuata huko.

pole sana ndugu yangu, najuwa na kila mtu anajuwa kuwa wakati ulionao ni mgumu na adui ibilisi atataka akukatishe tamaa na hasa akiona unakwenda kinyume na Mungu. mie naomba ujue ya kuwa tatizo ulilolipata siyo dogo kuliko matatizo ya wote duniani na wala siyo kubwa kuliko matatizo ya watu wote walioko duniani. mshukuru Mungu mama kakuacha ukiwa unaifahamu na jf. naamini mtaani kweno unawafahamu waliokutwa na tatizo kama lako wakiwa wana umri mdogo sana!. nakusihi muombe mungu ili akupe faraja kwakusoma Zaburi 23 na Zaburi 91 zitakusaidia sana. Mungu akushindie katika kipindi hiki kigum.
 
Ploe sana kwa kufiwa na mama yako mzazi,Mungu amrehemu na nyie awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana Mkuu
ni vigumu kupokea lakini kwa sala na maombi yawezekana
Mungu awape faraja na amani tele katika kipindi hiki kigumu
 
Pole sana sana, naelewa hali uliyonayo, lakini jikaze, mtumaini Mungu tu, mwambie wewe ulitoa na sasa umetwaa jina lako libarikiwe. Ukifikiria sana utakosa majibu kwani mwenye majibu ya maswali yako ni Mungu pekee.Kuwaza na kulia sana mwisho utamkufuru Mungu kisha utapata dhambi bure. Jua tu hapa duniani sisi sooote ni wapitaji, kwetu ni mbinguni, na hata tukikaa hapa milele haitatusaidia, wamekufa wengi sana hii inamaanisha soote tutakufa isipokuwa wale tu Mungu aliowakusudia wasionje mauti.

Bwana akupe amani na kusahau, pole sana, pata muda wa kuomba na kusoma neno la Mungu utapata faraja, pia hakikisha usikae peke yako, jitahidi kusahau mwambie Mungu akusahaulishe
 
ndugu zangu jumapili iliyopita tarehe 15.5.2011 ilikuwa siku mbaya kwangu kuliko zote. Mama yangu kipenzi alitangulia mbele ya haki. Tulimzika juzi jumanne. Ila kila nikijaribu kufanya chochote nashindwa nishaurini wenzangu. Nahisi nitamfuata huko.

kwanza pole sana kwa lilichokutokea mana kumpoteza m2 muhmu kama huyo ni jambo gumu sana pole sana kwa kilichokutokea. Kingine ninachoweza kukwambia ndio ninajua bado unayale maumivu na unaumia sana sana ninachoweza kukwambia jipe moyo na jaribu kufikiria namna gan utakavyoweza kujifanikisha ninakutakia maisha mema na mungu akuongoze na akujaze ujasiri na umakin amen
 
Tumia muda wako mwingi katika Ibada kama ww ni Mkristo Biblia inasema " amelaniwa mtu yule amtegemeae mwanadamu" Mungu hapendi umtegemee mtu mpk upitishe kiasi, kwakuwa mtu huyo wkt wowote anaweza kufa, plz weka tumaini lako kwa Mungu, jua hiyo ni njia na kila mtu ataipitia hata ww upo nyuma yake!!!

Nimaombi yangu Mungu akutie nguvu!!
 
Mh pole sana mungu akupe nguvu na akupiganie ili usimame ukimtegemea yeye na ukiamini katika yeye yote yawezekana atakuwezesha kulipita hili.

Naungana nawe katika majonzi kuondokewa na mzazi acha tu!
 
Pole sana kwa kuondokewa na Mama kipenzi: punguza wasiwasi ni mipango ya Mungu. Ongeza sala ili Mungu aweze kumpokea vyema.
 
ndugu zangu jumapili iliyopita tarehe 15.5.2011 ilikuwa siku mbaya kwangu kuliko zote. Mama yangu kipenzi alitangulia mbele ya haki. Tulimzika juzi jumanne. Ila kila nikijaribu kufanya chochote nashindwa nishaurini wenzangu. Nahisi nitamfuata huko.
Pole sana kwa msiba huo mkubwa hata hivyo uelewe wazi kuwa hakuna mwanadamu atakayeishi milele, watu wote watakufa, wataiacha hii dunia, huna sababu kabisa ya kukata tamaa kiasi cha kudhani kuwa kufa kwa mama yako ndiyo mwisho wa kila kitu, nakiri kabisa kuwa nihuzuni kubwa kumpoteza mama, ila endelea kumshukuru Mungu hata kwa kipindi chote ambacho amemuweka mama yako hai, endelea kujitia nguvu zaidi sana mtegemee Mungu maana yeye haitatokea afariki na yeye ndiye atakayekupa faraja. Jaribu la kufiwa na mzazi ni kubwa ila nakuhakikishia kuwa Mungu hataacha kukupa faraja. Pole sana ila cha msingi ni wewe binafsi kujiandaa ili siku yako ikifika uondoke ukiwa mtu safi mwenye sifa na vigezo vitakavyofanya kumuona Mungu.
 
Pole sana Mkuu kwa msiba mkuu uliokufika. Mwenyezi Mungu amlaze mama yetu mahali pema peponi~AMEN

980.jpg
 
Back
Top Bottom