Nimefiwa na mama yangu mzazi

Pole sana ndugu, tunajua machungu uliyonayo lakini ni lazina kujipa nguvu na kuomba uvimilivu, hasa ukizingatia kuku wewe si wa kwanza kupata msiba kama huo.
 
ndugu zangu jumapili iliyopita tarehe 15.5.2011 ilikuwa siku mbaya kwangu kuliko zote. Mama yangu kipenzi alitangulia mbele ya haki. Tulimzika juzi jumanne. Ila kila nikijaribu kufanya chochote nashindwa nishaurini wenzangu. Nahisi nitamfuata huko.

inauma sana kufiwa na mtu umpendaye kama mama, pole sana mkuu kwa huo msiba. RIP mama!
 
Pole sana, Mwenyenzi Mungu akupe nguvu. Mama yako aliishi hadi Mungu aliomuita mbele ya haki,wapaswa kuiga mfano wake....Kuishi kwa kumtumaini Mungu na kumtegemea hata wakati kama huu. Kila jambo na wakati wake,Mungu akutunze!:A S-rose:
 
Pole Mkuu. Machungu ni kawaida. Thamani ya mama ni kubwa sana. Watoto wachanga pamoja na kutoweza kusema wanatambua huyu ni mama na wengine ni watu tu! Mama ni zaidi ya mama, ni rafiki, ni sehemu ya miili yetu na akili zetu. Hivyo maumivu ni kawaida kuwepo, with time utajikuta unaanza kukubali na kuzoea hali ya kutokuwepo kwake. Mwenyezi Mungu akupe faraja. Pole tena, pole sana. Waweza kusikiliza wimbo wa Rkelly - I wish kama hautakuzidishia machungu.
 
ni kweli utamfuata siku aliyoipanga Muumba. jipe moyo Mungu yuko pamoja nawe. pole kwa msiba na RIP kwa mama yetu
 
.....pole sana, Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina la Bwana lihimidiwe. Kila nafsi itaonja umauti......unaumia kuondokewa na mama lakini shukuru Mungu umeona mapenzi ya mama yako. Kuna wengine wala hawakufanikiwa kuona mama zao....shukuru Mungu kwa hilo.
 
Pole sana, hiyo hali uliyonayo kwa sasa baada ya muda utaizoea. Kama wadau walivyoshauri usikae peke yako muda mwingi na hakikisha unafanya shughuli ambayo itauchosha mwili na kufanya upate usingizi mnono.

RIP Mama
 
Pole sana kwa kuondokewa na mama yako mpendwa, kama wewe ni mkristo soma Wafilipi 4:13 Inasomeka hivi: "Nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu" Ukimtumainia Mungu na kumuachia yeye mzigo huu utapata faraja ya ajabu. Lakin pia kumbuka sote ndio tuendako huko yeye ametutangulia tu!
 
Pole sana tena sana mkuu! Mungu akupe na ndugu wengine wote nguvu na courage to go on ktk kipindi hiki kigumu sana! RIP mama
 
asanteni ndugu zangu comment zenu zinanifariji na ninajihisi ni ktk jumuiya inayonijali.
 
mungu alitoa mungu ametwa jina lake litukuzwe,mungu akujalie moyo wa uvimilivu na ujasiri katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana mchaka mchaka ndo maisha hayo jipe moyo, hivi sasa nimetoka agakhan hospital, mama wa rafiki yangu amewekewa mashine ya kumfanya aendelee kuishi ana kansa, so keep strong my friend ur not alone.
 
pole sana,Duniani sote ni wapitaji
jipe moyo,nadhani wewe pia ni nguzo ya familia na taifa kwa ujumla
mwachie Mungu ataamua kwa wakati wake.

Kuwa na moyo mkuu.
 
Pole sana ndugu! Jipe moyo na MUNGU JEHOVAH akufunge mshipi wa faraja!:A S-rose:
 
Pole sana:
Kuna neno la faraja kutoka kitabu cha Neno la Mungu!Wafilipi 4:6-7
"Msijisumbue kwa neno lolote,bali kila neno kwa kusali na kuomba na kushukuru;haja zenu na zijulikane kwa Mungu.Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote,itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu;
 
Back
Top Bottom