Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,123
Tumesikia imetokea ajali ya Hiace na kuua watu sita wanaodaiwa ni wanachama wa CCM huko Niombe.
Katika mitandao yote iliyoripoti habari hii jumbe za kebehi na kushangilia ajali hii ni nyingi. Wanaoshangilia wametoa hoja wakionyesha changamoto tulizonazo za ajira ,nishati na rushwa zimechangiwa na marehemu jambo ambalo si kweli.
Naamini hawa waliofariki siyo Sehemu ya maamuzi na ndiyo maana wamelazimika kukodi daladala iwapeleke kwenye mkutano na kuwarejesha home.
Kwa namna watu walivyocomment na wanavyoendelea kugoment inatoa picha kwamba si watu wote wanaotuzunguka ni marafiki zetu. Wapo watu wanacheka na sisi ila ni maadui zetu.
Viongozi wa kisiasa niwaombe, kama hali hii isipofanyiwa tathimini upo uwezekano mkawa na walinzi, wapishi, wahudumu na hata wenza wenu ambao ni maadui zenu. Tusipuuze hali hii nakuamini tupo salama, hapana tunachukuana kwa itikadi na sasa umaskini umewafanya watu waanze kuombeana kifo ili na wao wapate nafasi.
Tunaposherekea Mwalimu Nyerere Day tuamue sasa kurejesha HAKI NA USAWA katika Tanganyika na Zanzibar.