Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,331
- 8,254
Habari za leo watanzania wenzangu,
Mimi rafiki yenu na kijana mwenzenu nilishafungua moyo wangu kuwatumikia watanzania katika kiti cha ubunge. Kama kuna wabunge humu naomba watanishauri zaidi ila ni jambo ambalo nalipenda na nina uzoefu nalo kidogo.
Muda wangu sahihi wa kujitokeza hadharani utakua 2025 ila bado sijaweka wazi nitagombea ubunge kupitia chama gani.
Hii ndio sababu kubwa iliyonifanya nisitishe masomo yangu haraka sana ili niweze kujipanga katika hili. Nilipata kuchaguliwa kuendelea na masomo ya PhD katika chuo kimoja huko nje ya nchi. Ilinipasa mwezi wa tisa mwaka jana niwe nimeshaingia chuoni na kuanza masomo yangu.
Naombeni kuungwa mkono katika hili. Najua muda ukiwadia ipo siku nitamalizia elimu yangu. Lakini kwasasa nijapange ili kutimiza adhima yangu.
Ahsanteni jamani.