Nimeagiza projector kwa ajili ya kuwafunza wanangu kuhusu madhara ya ngono katika umri mdogo!

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
3,978
5,295
Nawasalimia!

Nimeogopa na kutishika sana kila nisomapo baadhi ya ripoti za mashirika ya kiserikali na yale yasiyo ya kiserikali kuhusu vifo vya mabinti wakati wa kujifungua kutokana na udogo wa mlango wa kizazi.

Hofu hii imesababisha niagize projector na kununua 'flash chip' maalumu kwa ajili ya kuhifadhi 'clips' za mabinti wakisimulia mikasa waliyopata ama kunusurika kwa sababu ya kushiriki ngono katika umri mdogo.

Sambamba na hili, nitahifadhi mikanda ya madhara ya ngono kinyume na maumbile, usagaji na ushoga pia.

Nitazigawanya 'clips', baadhi zitaangaliwa na vijana wangu wa kiume tu, na baadhi zitaangaliwa na mabinti zangu tu. Na ni mama yao atatakiwa kuwa mwalimu kwenye 'sessions' hizo(kwa upande wa mabinti).

NB: Natoa taarifa pia kama kutakuwa na mwenye nyongeza yoyote juu ya hili, anaweza kuchangia pia. Maneno ndani ya funga semi si rasmi.
 
Aiseee, zama hizi unafikiri utafanikiwa? Utakaa nao muda wote watakusikiliza na kuzingatia au yataingilia huku na kutokea kule?

Mfundishe mwanao juu ya hofu ya Mungu ndani yake hapo utakuwa umeweza, hata kama atafanya lakini atafanya Kwa kuwa na hofu itamsaidia kuepukana na mambo mengine yasiyo faa kama ngono kinyume na maumbile ambayo Sasa ndio inaonekana fasheni.

Asiyefanya anaonekana wa kuja ila anayefanya ndio anaonekana mjanja, zama hizi ambazo Binti kuzalia nyumbani anajiita superwoman anayezaa ndani ya ndoa anaonekana mtumwa mwenye kupelekeshwa
 
Aiseee, zama hizi unafikiri utafanikiwa? Utakaa nao muda wote watakusikiliza na kuzingatia au yataingilia huku na kutokea kule? Mfundishe mwanao juu ya hofu ...
Hofu ya Mungu ni pamoja na kumfundisha aogope hayo mambo tajwa pia.
 
Dah!
JamiiForums765265586.jpg
 
Zaman serikali ilijitahidi sna kuonyesha makal ya Ukimwi ,vipeperushi sinema na hata majarida ,tulijengwa na hofu ya kutisha kuhusu ukimwi, hii kitu imenikaa mpaka Leo hii kichwani, unaweza fikia kuchakata kabsa bila taadhari ila nikikumbuka tu naingia mitini, sijui serikal imelala wapi nawaza viongozi nao ni victim.
 
Kwamba mtoto wako wakieume unamfundisha usifanye mapenzi kinyume na maumbile yaani wanaume wenzio wasikuingilie.

Sioni kama unamfunza bali kisaikolojia umemfanya Kama yeye laini laini na anaukike kihasi cha kumpa tahadhari asiingiliwe mwanaume hapaswi kupewa maelekezo ya kike kihasi hiko Ni kuvunja EGO yake ya kiume kabla ya uwanaume unaonekana nje Kuna uwanaume wa ndani ambao ni EGO.

UMWAMBA NA ANGER ukimkalisha chini mwanaume na kumwambie angalie usije ingiliwa Happ sawa na umeuwa uwanaume wa ndani rahisi Sana kuangushwa hata uwanaume wake wa nje.

Tafuta njia sahihi ila sioni kuwa hii ni njia yaani unikalishe chini uniambie madhara ya mwanaume kuingiliwa so unamaanisha nafanana na kuingilowa una mashaka na ubabe wangu na uwanaume....INSANE
 
Back
Top Bottom