Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,150
- 10,393
Uzi huu unawalenga zaidi vijana wote (haswa wa KIUME )japo hata kina sisi sun set tunakumbushana pia.
Ewe kijana kumbuka kila jambo linatakiwa lifanyike kwa wakati na muda sahihi.
1. Kazi
Sisemi kwamba vijana ni wavivu hapana ,ila ni vyema kujitahidi na kupambana zaidi katika umri mdogo.
Hata kama kwa wazazi ni mambo safi lakini ni vyema kuomba hiyo sapoti mapema ili kujijenga mwenyewe.
2. Ndoa
(Wale timu kataa ndoa hapa hapawahusu)
Ni vyema kuoa mapema na hata watoto wapatikane mapema hii itasaidia kuwakuza na kuhakikisha wanaanza kujitegemea huku ukiwaona hii inapendeza na iko poa sana kuliko mtu una 40+ ndiyo unapata mtoto wako wa kwanza.
Utakuja kuitwa babu na wanao.na ni rahisi kufa kabla watoto hujawaachia msingi imara.(kifo kikikuita hukatai umri wowote mtu anaaga Dunia)
3. Assets
Hakuna jambo tamu na zuri kama kumiliki mali fulani ukiwa bado kijana ,yaani miaka 30 tayari una nyumba kadhaa mjini ,unafokeana na wapangaji tu. Na hata vibubu vyako vinakuwa vyema,iko poa sana maisha yatafutwe kwa wakati.
Kumiliki mali uzeeni ni changamoto hata mali zako mwenyewe baadhi unaanza kuzisahau na kujikuta unapigwa na wajanja tu.
4. Starehe
Ukiwa umejipanga vyema yaani kuanzia 1,2,3 kama nilivyoandika,
Usisahau kuishi,ishi maisha ungali bado kijana ,starehe na ulimbukeni wote fanya ukiwa kijana kwa wakati ambao ni sahihi ,maana usipofanya kwenye ujana wako ,utayafanya hayo mambo uzeeni na hapo ndipo utawashangaza walimwengu maana pengine umri wako na uyafanyayo vitakuwa haviendani.
Hudhuria klabu ,toa ushamba wote,kama kuna nafasi ya kwenda kuzurura ughaibuni,fanya sasa hivi kama maokoto yanaruhusu.
Kama ni wanawake warembo piga,narudia tena chakata hawa viumbe (jilinde na ngono zembe) huku ukihakikisha unamuheshimu mkeo na mama wa watoto wako. Siku ukizeeka utakuwa ushamaliza kazi kuliko kufia vifuani mwa watoto.
5. Jiheshimu (linda heshima)
Wakati wa wewe kuheshimiwa ni sasa,mwanaume yeyote huheshimiwa tangu anapotoka kwenye tumbo la mama yake,heshima ya mwanaume ni ya asili ,makabila mengi duniani mwanaume hupewa kipaumbele,yaani huheshimiwa.
Heshima haitafutwi,wala hailazimishwi, heshima haitengenezwi bali hulindwa ili isipotee kwani unayo tangu unazaliwa haijalishi ulikuwa na kitu au hauna ,ukiwa na vitu vitatu nimeandika hapo juu kwanini usiheshimiwe?
KAZI,
NDOA,
ASSET & LIABILITY
Ili uilinde heshima yako ambayo uliopata siku ya kwanza unaingia kwenye huu ulimwengu wa fujo unapaswa kufanya kila kitu kwa WAKATI sahihi.
Tunakumbushana tu wanajamvi.