Nimeachana na mke wangu

Maamuzi yako ni sahihi wewe ni Kama mimi sipendi vita na mwanamke kabisa ni kumuacha na kuangalia maisha mengine unaweza shikwa hasira ukafanya kitu kibaya sana
 
Acha utoto mzee, kipimo kikubwa cha uanaume na kuweza kuishi na mwanamke.Muulize baba yako, uliza wanaume mambo wanayopitia, hapo kwako sijaona issue yoyote ya maana.Ishi na MWANAMKE kwa akili...mjue mkeo na ujinga wake..then endeleeni na maisha..

Kuna huyo wako anakupigia makelele, kuna wenzako mwanamke ananuna wiki nzima..mdomo unavimba hatari...na mzigo hupati...wanaume tunajua namna ya kuhandle hawa mama zetu

RUDI KWA MKEO, MPIGIE SIMU, MJALI KWA HALI ALIYINAYO....AS long as hachepuki, hakudhuru wewe binafsi etc haiba haja ya kuachana..

Pia inaonekana na wewe unaongea sana, mnajibizana sana..hakuna mwenye maneno machache....jishushe..nyamaza vingine, usitake kupata majibu kwa kila kitu..wanawake wana mood sana..
Kila la kheri
 
Ila mkuu we na mkeo sijui mna shida gani mara asafiri safari za ghafla mara uje tena useme unamchukia mkeo

Kama mmefikia maamuzi haya ni bora ili kila mmoja aishi kwa amani
 
Wabari wakuu na wanaJF, natumaini ni wazima wacha niende kwenye mkasa.

Mke wangu ni mjamzito, sasa mwezi huu wa 11 nilipata safari ya kikazi Dodoma sasa inaenda wiki ya 3, lakini baada ya kuondoka nyumbani kwaajili ya safari hii ya kazi kiukweli hakuna amani kabisa juu ya mimi na mke wangu. Ni ugomvi, kulumbana na kugombana kila siku.

Mke wangu amekuwa na magomvi yasiyoisha sijui kwanini, lakini kila siku ni maugomvi. Kiukweli hii hali nimejitahidi sana kuiweka sawa lakini imeshindikana sababu mke wangu amekuwa kama Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Taifa kila siku kesi zisizo na msingi bila sababu.

Kutokana na hayo kiukweli ikafika hatua dada yake ikabidi aingie kati na kutuweka sawa lakini wapi, jitihada zake hazikuzaa matunda kabisa, moto ukawa ni uleule. Lakini nimejitahidi sana kuhakikisha nayakabili haya lakini ikashindikana, kila nikiwaza na kutafuta tatizo ni nini sipati jibu.

Nikimuuliza mwenzangu unataka nini ili tuyaepushe haya maisha ya kugombana hana kitu cha maana na hana sababu, kwasababu mpaka dada yake kashakaa naye na kumuuliza nini shida lakini hakuna cha maana alichosema.

Kiukweli ikafika kipindi dada yake akaamua kutuacha wenyewe na kushindwa kabisa, lakini kila nikiwaza au labda ni mimba ndiyo inamsumbua, lakini dada yake aliniambia kuwa ni wivu tu ndiyo unamsumbua kwasababu anajua upo mbali ndiyo maana kila siku anaanzisha ugomvi.

Juzi nilikuwa kazini na tulikuwa tuna kikao akapiga simu, kiukweli nilishindwa kupokea nikamtumia ujumbe kuwa nitakupigia baadae niko kwa kikao lakini hakutaka kunielewa kabisa, na kuanzisha ugomvi usiyokuwa na sababu na kusema eti namdharau sipokei simu zake.

Hivi kweli wakuu hii iko sawa, na ukizingatia niko kwa kikao na viongozi wangu? Kiukweli hii hali ikafikia hatua nikashindwa wakuu kila siku ugomvi.

Wikiendi hii nikaamua kwenda nyumbani nikaongee naye vizuri anieleze kwanini anakuwa kama mtoto kila siku ugomvi ukizingatia hata hajihurumii na hali yake, nikataka anieleze nini shida na anataka tuishije? Wakuu nilijuta kurudi nyumbani, kiukweli tuligombana sana kupita amelezo na kufikia uamuzi wa kuchana!

Kiukweli naona tumeshindwana, nimeamua kuondoka na kurudi kazini tena kuendelea na kazi nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.

Na kuna hela kwenye akaunti ambazo nimemuekea kama akiba ya dharura kutokana na hali yake, na nimeshamtaarifu dada yake kwa maangalizi, lakini kama kuna changamoto yoyote itatokea anijulishe nitampatia pesa.

Lakini sitaki amwambie mdogo wake kuwa nimempatia hela, na ninafanya hayo kwaajili ya kiumbe changu alichobeba mpaka pale atakapojifungua halafu baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.

Wakuu ni hayo yaliojiri, kama nitakuwa nimekosea wakuu mtanisamehe lakini nimeshindwa hayo maisha ya ugomvi kila siku. Hapana wakuu kama mtoto nitatimiza majukumu yangu kama baba.

Shukrani wakuu.

Pole sana kwa kweli ila hii tabia toka zamani au ni katika hali hii ya ujauzito? Kuna kitu kimoja huwa nasema mke akiwa na amani na mume anakuwa na amani na family kwa ujumla, Mke ndio kila kitu katika mahusiano anaweza kujenda na anaweza kubomoa.

Huwezi kufanikiwa katika kazi zako ukiwa na mwanamke hakupi amani nyumbani kiwango chako cha uzalishaji kazini kitapungua tu ulichofanya sawa mpe space siku aelewe kuwa kwanini umeamua hivyo.

Kwa wanawake nawashauri dawa ya Mume hata kama kakosea ukiwa mpole na muelewa nakuhakikishia unajenda uimara wa ndoa yako mume hata aende wapi atakupa heshima. Tabia ni kila kitu.
 
Naomba nikupe uzoefu wangu. Siku ya kwanza nimeenda na shemeji y'ako kupima mimba.Baada ya majibu Dr alichonieleza ..sasa unatakiwa kuwa mwanamme kamili..wanawake wakiwa wajawazito huwa na tabia za ajabu ..usikasirike we jua ni kwa sababu ya ujauzito..na kweli yalitokea mengi ya kukwaza ila niliyavumilia.

Nachoweza kukushauri mpende mkeo ...na subiri baada ya kujifungua utaona mabadiliko..
Mimba Zina shida sana..nilishawahi kuamshwa saa Tisa usiku nikatafute chipsi...na Binti analia kabisaaa
 
Mhh kwamaamuzi haya yko,kunamengi hujayasema kukuhusu pamoja na kipindi kigumu cha ujauzito anachopitia mwenzako naye anaziada inayomtesa juu ya tabia yako+ukombalinae kwa sasa hawezi kujua unafanya nini hapo ulipo.

Pili mbona unaongea kama umetake advantage ya maumivu yake juu yako,nikweli umemwacha au umeleta uzi tupotezee muda,ukweli sijaona juhudi hasa ulizofanya kumtuliza mwezio kama kweli unafwedha ungeagiza nae awepo huko ulipo japo usiku apoze moyowake kwamba uposalama na haibiwi maliyake,Ila kwakujinafasi kwamba umemwachia hela,umechukua apartment unaishi pekeyako mh.

Na pia nadhani utakuwa hujakomaa kifamilia ndugu yangu,ndiokwanza umejaribu kuoa ila ndoa imekushinda
Anyway pole yake mama k wa watu,upendowake wa kukuletea jina hapa duniani umemponza.

Hayaa
 
Naomba nikupe uzoefu wangu..Siku ya kwanza nimeenda na shemeji y'ako kupima mimba.Baada ya majibu Dr alichonieleza ..sasa unatakiwa kuwa mwanamme kamili..wanawake wakiwa wajawazito huwa na tabia za ajabu ..usikasirike we jua ni kwa sababu ya ujauzito..na kweli yalitokea mengi ya kukwaza ila niliyavumilia..
Nachoweza kukushauri mpende mkeo ...na subiri baada ya kujifungua utaona mabadiliko..
Mimba Zina shida sana..nilishawahi kuamshwa saa Tisa usiku nikatafute chipsi...na Binti analia kabisaaa


Sema kuna vingine n kama huwa wanafanya makusudi kuisingizia mimba. Kuna pisi flani hivi 2 zilishawai kuniambia zinasubiri zidake mimba zianze kunidekea

Nikawaza hawa inamaana hua wanafanya makusudi au.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Na siku nyingine usirudie tena kulitamka hilo neno kuachana kemea kabisa. maneno uumba. Kuwa mtu wa kurekebisha mambo na si kubomoa. huyo mtu ana kiumbe chako tumboni halafu unatamka kumuacha, hujui hata mtoto tumboni anawasikia mnavyochemka hapa duniani. Wenzako watoto wakiwa tumboni uwa tunaiambia mimba na kuinenea mazuri na kumnenea mtoto mema pindi atakapozaliwa. Wewe kinyume chake unatangaza kuachana na mkeo, yaani mnampa stress mtoto toka mimba. Umenikwaza sana. Rudi kamuombe radhi mkeo na umuombe radhi huyo mtoto aliyeko tumbani

Sawa mkuu nimekuelewa
 
Siku akijifungua utamkana mwenyew,utasema ni yeye kweli?,mbona kabadilika...Iliwahi kunitokea mimba hainitaki mimi,nilimrudisha fasta kwa Mother,hali ilitulia maana wazee wanajua jinsi ya kuhandle hali hizo..Alipojifungua alikuwa anahadithia na kuishia kucheka tu....

Bas naimni na mimi wangu atakuwa sawa
 
Mungu ni mwaminifu sana. Nimefurahi wengi wenu hapa mmemcrush mleta mada na kumpa ushauri mzuri. knows kama una hekima na busara basi utafanyia kazi hizi shauri.

Madhaifu kwetu wanawake yapo na mwanadam bila udhaifu jiulize mara mbili..utakuwa unaish na kijini alichokiimba mbosso. Najua unao moyo mzuri na mpaka kuamua kumuoa ina maana alikidhi vigezo vyako.

Yumkin hiyo ndo ile 20% alioikosa katika zile 100% zako kwahyo mbebe aisee. Hata wewe deep down unafaham unao udhaifu. Kama unapenda kuwa mtu wa maana hapo baadae na kuwa baba bora katika jamii futa kuachana katika akili yako. Ndoa is a struggle for both parties. Work on your marriage. Mungu awasaidie kuitengeneza familia yenu. Be blessed

Nimekuelewa mkuu be blessed
 
Back
Top Bottom